SEPTEMBER 1 SEHEMU YA SABA.

TULIPOISHIA SEHEMU ILIOPITA.
Mtoto akilia wembe we mpe tu, sasa kapewa kweli na umemkata. Yaani hata nafasi ya kujuta kwa kujiingiza kwenye mambo yaliyomzidi uweozo hatokuwa nao. Ndiyo kwisha habari yake, mpumbavu sana yule jamaa. Sasa tunamtoa sadaka halafu tuone huyo mwenye kumlinda hadi kamwacha akalipukiwa na gari atafanya nini", Besi alijitapa baada ya kukamilisha kazi yake haramu.
ENDELEA NAYO SASA...
Mkuu gari ya N001 imelipuka muda mfupi uliyopita, hivi sasa ipo pale daraja la salenda ikiwa imegonga ukingo wa daraja", Afisa mmoja wa EASA alifikisha ujumbe harakaharaka kwa mkuu wake wa kazi, ambao haukufika kwa Katibu muhtasi kuhofia angeweza kumtia kihoro.
"Unasema! Tafuteni haraka alipo N001 naomba chipu yake itafutwe ilipo kama nayo imeharibika na mlipuko huo au bado ipo kwenye movement.
Nachohitaji ni kujua kijana wangu kama yupo salama au lah!", CE alipopokea taarifa hiyo alibonyeza simu yake ya mezani wka haraka kisha akaongea, muda ambao bado aliyeileta hajaruhusiwa kuondoka.
"Mkuu bado ipo kwenye movement sasa ivi inaonekana ipo Magomeni", Sauti kutoka kwenye simu ya mezani ilisikika. Hii ilimfanya CE aachie tabsamu la ahueni kwa kujua N001 bado yupo kazini, hakuwa amekumbwa na mlipuko ule. Alisema, "huyu anakuja ofisini hivi sasa nafikiri anahitaji huduma nyingine zaidi, kafika sehemu gani hivi sasa?"
"Keshavuka magomeni hivi sasa yupo Kigogo akielekea Ilala................Amefika Ilala hivi sasa tujiandae ndani ya muda wowote anaweza kufika ofisini hapa....................................Yupo juu kwenye mlango wa kuingilia, ndiyo anaingia ndani", Sauti ya mtu aliyepo chumba maalum cha kufuatilia vifaa vilivyo miilini mwa wapelelezi, ilisikika ikitaja kila kituo alichofikia N001. Ilifanya hivyo kwa dakika kadhaa baada ya kuiona ikiwasili, CE alitulia kimya asikiliza hadi mdua ambao amesikia amefika mlango wa kuingilia ndiyo akakata simu na kusimama wima.
"Wewe kazi yako imeisha hivi sasa, rudi
kitengo chako N001 nitamsubiri mwenyewe hapo kwa hawara wake", CE alisema huku akisimama, kijana aliyemletea taarifa naye aliinuka na wakatoka pamoja hadi walipofika ofisini kwa Norene. Kaila walimwona ndiyo anaingia amechafuka vilivyo, na miguu yake inanuka kutokana na kukanyaga maji machafu. Norene hali hiyo ilimshangaza mno, akaona mpenzi wake aliponea kwenye tundu la sindano huko atokapo.
"Naona mwenye masters leo umekutana na wenye PHD hadi wamekufanya hivyo, najua umeumia ila nahitaji maelezo ilikuwaje hadi gari lilipuliwe na bomu", CE alisema huku akifumbata mikono kifuani mwake. "Mkuu ukae utambue hapa nchini kuna injinia hatari kuliko wote wa umeme, gari liliingiliwa system nzima ya uratibu wake. Likawekwa bomu ambalo lilihesabu dakika kupitia kwenye screen ya redio ya gari, nikapewa onyo ukisimama umekufa na ukipunguza mwendo hutopona. Ndiyo nikaamua kuchoropoka baada ya kujua kuna udhaifu mmoja, haikuweza kuzuia mlango usifunguke hiyo system", Norbert alieleza huku akimtazama mpenzi wake kwa kuibia, aliuona uso wa binti huyo ulivyoingiwa na uoga.
"Hongera kwa kutumia akili vizuri, pia nikupongeze kwa kunibadilishia harufu ya ofisi na kuwa kama ya sewage system. Norene mchukue mtu wangu akasafishwe huyo kama ana tatizo atibiwe huko, nahitaji akitoka hapa arejee kazini", CE aliongea na alipomaliza alirejea ofisini akimwacha N001, Norene na yule kijana aliyekuja kutoa taarifa.
"Leo wamekuweza jamaa yangu, yaani ungechelewa kidogo tu tungekuja kuokota minofu yako ikiwa imeivaa kama mishikaki", Kijana aliyekuja kutoa taarifa alisema huku akicheka kama vile kumetokea jambo la kuchekesha, hata Norene naye alicheka kwani walishazoea kuwa namna hiyo mwenzao akipona kwenye tukio zito.
"We bwana kunuka hebu kwanza twende huku, hapa pua zangu zinakaribia kuharibika kabisa kwa hiyo harufu", Norene alisema huku akisimama..
"Na leo utageuka bibi kunuka nakwambia, yaani nakukumbatia hapahapa na mavumbi yangu haya na mijasho hii. Hadi harufu ya maji machafu ibaki mwilini", Norbet alisema huku akimkaribia Norene, akiwa ametanua mikono kabisa kujiandaa kumshika mwilini.
Binti wala hakuonesha kumhofia alibaki akimtazma tu huku akicheka, alipokaribiwa kufikiwa kwa wepesi wa hali ya juu. Alimpiga judo moja Norbert akaenda mzimamzima chini, kijana waliyebaki naye mahala hapo alicheka kwa nguvu mno huku akimtazama Kaila aliyenguka kifua.
Norbert alijikuta akikumbwa na kicheko naye, pamoja na kuangushwa kwa mtindo wa judo. Hakuona la kumfanya achukie ilihali alimfuata kizembe mwenyewe, huku akijua wazi wazi anayemwingia ni mwenye kuucheza mchezo kama yeye. Mambo yakuwa na mpenzi mwenye kufanya kazi inayofanana, ndiyo hayo yamemtokea hadi akaangushwa chini. Alijiinua wima huku akiendelea kucheka, muda huo Norene alishaanza kupiga hatua kuelekea ulipo mlango wa kutokea ofisini humo.
Naye alimfuata akiwa ameongozana na yule kijana, walitoka humo na kuingia kwenye eneo lenye ofisi nyingi kukiwa na wanausalama tofauti wakifanya kazi zao. Kila mmoja aliyemwona Kaila na kuisikia harufu anayoitoa, alibana pua huku akicheka kwa nguvu kwani alijua wazi huko alipotoka alikutana na kioja cha mwaka.
Norbert aliongozwa na hadi kwenye vyumba vyenye mabafu maaluma ya kuogea, huko alioga kuondoa uchafu wote pamoja na harufu ya mwilini. Alipomaliza alipatiwa nguo ya ndnai tu, pamoja na taulo ambalo alilijifunga kisha akaongozana na binti yule hadi kwenye chumba kingine chenye kufanana kila kitu na wodi ya hospitali. Humo ndani kulikuwa na kitanda katikati sambamba na vifaa mbalimbali vikiwa vimepangwa kwa utaratibu maalum.
"Laza mwili hapo, uniwekee mgongo juu", Norene alimwambia huku akivaa glovu za kitabibu.
"Ukinibaka je? Marinda yangu nayapenda" Kauali hiyo ilimfanya Norene acheke, hata mpira wa mkononi mmoja ukamponyoka na kuanguka.
"Mwone kwanza, akili zako fupi kama kidole chako cha mwisho cha mguu", Norene alisema.
"Ndiyo hizihizi umedata nazo hadi ukanipenda na kunizalia mtoto na miaka yote upo na mimi. Wacha ziwe fupi namna hii, zisiwe ndefu wala nyembamba sana kama ming'oko ya wamwera", Norbert alisema huku akijilaza kifudifudi kwenye kitanda, mikono aliweka makalioni na kumfanya Norene acheke zaidi.
"Tahadhari kabla ya hatari, wewe tibu hayo majeraha pembeni huko mgongoni. Ila huku wacha
nipazibe tu maana judo ile uliyonipa pale. Si bure una jinsia mbili wewe", Norbert aliposema hayo, mlango wa mahala hapo ulifunguliwa kwa ghafla. Jambo hilo lilimfanya atoe mikono upesi makalioni, huku Norene akiwahi kuchukua dawa na pamba baada ya kumaliza kuvaa glovu.
CE alionekana akiingia na alifunga mlango, aliwatazama wapenzi hao wenye kuonesha wapo kwenye kuhudumiana kisha akaachia mgumo. Pamoja na hayo alisema, "N001 kuna chochote ulichokiacha eneo la tukio ambacho kinaweza kuwa alama ya shirika letu? Najua kwa jambo la haraka namna ile wewe ni binadamua pia, unaweza kusahau kitu ili kujiokoa"
"Pamoja na kuwa ni binadamua bado akili yangu ilizinduka kutoka kwenye uoga. Nikaweza kuchukua kila cha umuhimu na kukiweka kwenye begi langu ambalo ni madhubuti", Norbert alijibu.
"Safi sana, umakini wa namna hiyo ndiyo ninautaka. Ukitoka hapa utapatiwa gari nyingine kama ile", CE alisema kumpongeza Norbert na aliuliza, "Waliyofanya jambo hilo una uhakika hawakuacha alama yeyote ile ambayo ingeweza kukujulisha mahali walipo?" "Wameacha simcard na chipu ndogo sana, vyote vipo ndani ya begi langu. Nikitoka hapa nitahitaji majibu yake. Muzo amevichukua kwa ajili ya kuvitafiti", Norbert alijibu na muda huohuo alijikuta akishtuka na kuuma maneno yake kisha akamtazama Norene aliyekuw aakiendelea kumtibu. Alimwambia, "we mwanamke utanishonaje bila ya ganzi, ushaona ngozi ya robokopi hii. Nina neva za maumivu kama wengine"
CE alijikuta akitabasamu na alisema, " ndo uanaume huo uchomwe ganzi usubiri iingie hadi uje ushonwe hapo begani ulipopasuka kidogo itakuwa ni saa ngapi ukimalizwa na unahitajika kurudi kwenye misheni. Kabla ya septemba tatu kazi iwe imeisha hii, okoa muda. Ngoja niwaache"
Mkuu wa kazi alipotoka Norene alisema, "Nyoo yaani uweze kuvumilia maumivu ya kuchomwa kisu cha paja ulipojifanya umekufa kule Somalia ndiyo uje useme unaumia kwenye kitu kidogo kama haki"
"Kwenye kujiokoa na kifo unafikiri kuna nani anakumbuka kama anaumia, we sikia tu siku ile ningemwacha mwanangu yatima niliachiwa kwa majaliwa ya Mungu tu. Kuna mjinga mmoja alisema wanijaribu kwa risasi kama nipo, mwingine ndiyo akakataa na kunichoma kisu kile kilichoniachia alama hadi leo. Ukikumbuka kifo maumivu unayasahau hata"
"Haya mimi nishamaliza kazi yangu, wewe nenda chumba cha mavazi ukajichagulie nguo mimi naenda kuchukua funguo za gari utanikuta kwenye yard ya chini nakusubiri", Norene alisema huku akivua mipira aliyoivaa.
"Kwanini tusiende wote ukanivalisha, tupige kwata kulekule kabla hujatoka"
"Nor hapana unaingia kazini wewe ukumbuke"
"Si nabusti mishipa ya fahamu kidogo, hujui supu bila ya ndimu ni juisi ya moto tu itakuwa"
**
Habari ya kulipuka kwa gari la Norbert ilileta furaha kubwa mno kwa akina Huze. Wakabaki wakijiandaa kwa lolote kuanzia muda huo, hawa kwenye maeneo ambayo kuna sehemu zao maalum kwa ajili ya kuandaa kazi zao. Walijua lazima huyo mtu afike eneo ambalo kuna kituo cha kutengenezea simu za mikononi, kwani kitu pekee walichohofia kingeweza kubaki kwenye mlipuko uole. Ni masalia ya simutamba ile tu, si kingine.
"Sasa tumtarajie anaweza kufika kwa Mbiku kuanzia muda wowote ule huyo mpelelezi, simu ile haiwezi kulipuka yote. Pia ina alama ya kiwanda chetu cha kufufua simu zilizokufa", Huze alisema.
"Sasa huko ndiyo nimeshaagiza vijana wa kazi wakae mkao wa kula kwani atafika muda wowote baada ya kujua hilo. Lazima tumnase huyu", Watson alisema.
"Jamani naona tunafika mbali sana, kabla ya kupanga mipango hiyo yote hebu tufanyeni jambo moja. Tupate uhakika wa kifo cha Kaila, tumelipua ndiyo na hata kwenye vyombo vya habari wametangaza hilo. Ila haipaswi kujiamini namna hiyo", Besi alisema.
"Besi kijana wangu mbona hii ishu imeisha tayari, unataka uthibitisho gani mwingine. Hujui kama ndani ya gari kumetolewa mwili mmoja, hata raia wameshuhudia hilo. Unafikiri ndani ya gari lile kulikuwa na kiumbe gani kama si Kaila", Watson alisema.
"Kama ni hivyo basi mchezo umekwisha, anzeni mpango haraka sana ninavyowajua wapelelezi hawalazi damu. Msije mkakaa hapa msubiri uchunguzi wajue simu imetoka kule, kumbe keshaingia na kusababisha mengine na akatoka. Hawa watu wanafanya kazi upesi kama kompyuta ya mamlaka ya hali ya hewa. Wahi upesi sasa hivi, tena Huze ningependa uende kule kuifanya kazi hiyo mwenyewe. Mimi narejea ofisini hivi sasa, waziri wa nishati na madini pia ananihitaji hivyo lazima niende huko"
"Ok hilo suala niachieni mimi", Huze alisema.
**
Muda mchache baadaye Norbert alishavaa nguo nyingine, akiwa ameshakabidhiwa gari mpya kwa ajili ya kuingia kazini kwa mara nyingine. Majibu juu ya chipu ile aliyoikuta ndani ya simu, yalitoka akawa na karatasi zenye kuonesha kila kitu kuhusu kifaa kile. Alibaki mwenyewe kwenye yadi ya gari, akiwa yu ndani ya motokaa yake akipitia ripoti ile iliyotoka chumba maalum cha wataalamu wa tarakilishi.
Maandishini aliweza kuona kifaa kile ni mali ya kampuni yenye kutengeneza magari ya kuchezea watoto ambayo hupatikana Mikocheni. Huko ndipo alipopanga kuanzia kwenye shughuli yake baada ya kutoka hapo ofisini. Yaani ni tofauti kabisa na kule ambapo kina Huze walidhani jasusi anayewatia hasara angefika, akili zao ziliwaaminisha kuwa mlipuko ule umeharibu chipu iliyopo ndani ya simu na vifa pekee vya simu ndiyo vitasalia.
Hawakujua mwenzao ameruka tayari, na ripoti ya kuonekana kwa mwili mule ndani haikuwa sahihi yote ni njama ya EASA kuweza kumuhadaa adui. Nao wameingia mkumbo uleule. Hakika walipumbazwa haswa kwa kuweka ulinzi kwenye kiwanda kingine, kumbe mzee wa kazi kalenga pengine.
Norbert alipomaliza kupitia ripoti nzima, aliiweka kwenye saraka ndani ya gari. Aliingiza namba maalum za siri za motokaa ile, kisha akaiwasha. Muda lango maalum la kutokea humo lilishafunguliwa, alikanyaga akselereta kutoka humo ndani. Aliingia kwenye njia ya chini ya ardhi yenye kuzunguka kupanda kuelekea juu. Muda mfupi baadaye alitokea kwenye maegesho ya ghorofa la hoteli ambalo limebeba ofisi zao. Aliingiza gari barabarani na kuondoka, huku akiwa amejua ni wapi pa kuanzia.
**
Habari ya kulipuka kwa gari ambalo analitumia Norbert zilizagaa jijini, kwa mfululizo wa matukio yaliyotokea kwa kipindi kifupi kilichopita. Wengi waliona ni sehemu ya mwendelezo wa matukio ya kigaidi, hofu ilitanda na hata wengine wakagoma kupanda magari haswa ya jumuiya. Hata wale wenye kupenda kuegesha maeneo ya wazi walihofia kutegewa bomu, hali hii ilipelekea kuibuke kwa taaswira nyingine nchini.
Jambo hilo likitokea mheshimiwa Waziri wa ulinzi, alikuwa kwenye kikao kifupi na wakuu wa majeshi. Yaani mkuu na manadhimu wake walikuwa kikaoni ofisini kwake, yote ni kuelekea siku muhimu maana siku zilibaki chache ndani ya mwezi agosti. Hivyo mambo yalihitaji kukamilika mapema. Dhima ya maandalizi ilipangwa na wanajeshi, huku mhandisi mzawa akateuliwa kwa ajili ya kazi maalum maana mifumo yote ndani ya chombo cha usafiri katika uzinduzi kilihitaji umeme ili kifanye kazi.
"Mnajua muda huu wa kupotea maafisa wetu na pia kutokea kwa amtukio mfululizo wa milipuko naanza kuona kunahusiana ", Waziri alisema.
"Hata mimi hilo nimeliona Mheshimiwa, ila tuliache wenye kufa ya utafiti wapo kazini naamini watakamilisha kila kitu. Tujadili juu ya siku hii muhimu", Mkuu wa majeshi Jenerali Marwa alisema.
"Mheshimiwa waliyopewa kazi hii naamini hawawezi kutuangusha kwenye hili, Afrika ya mashariki hivi sasa tuna intelijensia imara mno. Nadhani ni muda wa sisi kuendelea na mengine. Maneno ya raia wanaona kama serikali inafanya uzembe wakati wangeachiwa wao hii kazi wasingeiweza. Tuyaache yasituchanganye, sisi tuwe upande wetu na wengine wa kwao. Tusiingilie majukumu ya watu, kuhusika na usalama wa raia ni kazi ya polisi na kutafiti mambo kama hayo kiintelijensi ni kazi ya EASA na TISS. Hebu nao watimize jukumu lao, tayari taasisi mojawapo hapo ipo kazini", Luteni jenerali Belinda alisema.
"Ok, sasa jamani nadhani ni muda wa kukagua vitu vyote kabla ya kuzinduliwa kwa safari hiyo. Tayari hivi sasa nimezungumza na Babu, wizara yake imeshampaa mtu wa kufanya kazi hiyo, reli imekaguliwa bado kifaa chenyewe atakachopanda Mheshimiwa kifanyiwe hivyo. Maafisa wote wa ngazi ya juu ndani ya jeshi, wawepo siku hiyo. Wote tutaenda na treni ya majaribio hadi Mwanza, mabehewa yatawekwa ya kutosha.Ishu hii ilitakiwa kuwekwa watu wachache kwenye uzinduzi.Ila Mheshimiwa kapendekeza atembee na wananchi wake siku hiyo, tukae tukijua mabehewa yatafungwa mengi. Upande wa nyuma watawekwa wananchi wenye kusafiri kuelekea Mwanza tena bure.
Hivyo kunahitajika behewa la mwisho wakae vijana wenu.
Mbele kwenye kichwa kutakuwepo dereva na
Mheshimiwa na maafisa wa TISS pamoja na nyinyi", Waziri alisema.
"Sawa Mheshimiwa kazi hiyo naiacha kwa Belinda chief of staff, ataamua kuongea na members of staff juu ya hili", Jenerali Marwa alisema.
"Hakuna shaka ilimradi ulinzi uwepo, jeshi la polisi watahusika katikati ya mabehewa tu kwa kujichanganya na raia. Askari kanzu watawekwa humo, ili usalama wa raia uwepo. Safari hii nahitaji iwe ya kihistoria, iende na kumalizika kwa usalama mkubwa bila ya kukumbwa na lolote"
ITAENDELEA
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment