Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SEPTEMBER 1 SEHEMU YA NNE


A Walk to Remember – Movie Recommendation | Bullies2Buddies
ILIPOISHIA JANA.

Mkaka sisi tulitaka kuondoka ujue, sijui hapa mezani ingekuwaje", Mmoja wa vipusa wa wale alisema.
                    "So sorry cutes, nilifika kule Ilala Boma kuna rafiki yangu tulienda kuonana naye mara moja. Hata mimi si mkaaji, nabeba kinywaji changu hiki niondoke", Norbert alisema.

ENDELEA NAYO SASA......

Mkaka sisi tulitaka kuondoka ujue, sijui hapa mezani ingekuwaje", Mmoja wa vipusa wa wale alisema.
                    "So sorry cutes, nilifika kule Ilala Boma kuna rafiki yangu tulienda kuonana naye mara moja. Hata mimi si mkaaji, nabeba kinywaji changu hiki niondoke", Norbert alisema.
**
 
                     "Hebu Huze waulize hao vijana tayari wameshafika huko godauni, huyu  Kaila nataka nimpoteze mwenyewe  akishataja ni wapi ametoa habari hizo. Tena kijana alivyo mjinga anabwabwaja tu", Watson alisema.
                    "Ninawatafuta naona hata simu  yenyewe hawapokei, sijui wapo wapi hawa", Huze alisema huku akijaribu kupiga simu kwa   mara nyingine, kama anaweza kuwapata vijana aliyowatuma. Muda akihangaika hivyo, Kail ndiyo anajiandaa kuondoka klabuni pale tena akiongozana na warembo wale.
           Alijaribu kupiga simu kwa  mara nyingine, safari hii ilipokelewa. Huze alijikuta akiongea, "Enhee! Niambieni kazi imekwenda  vipi...........hongereni sana niwakute njia panda ya Kigogo mtanikuta nimevaa nguo koti la jeans juu,  chini nina suruali ya jeans. Mtaniona  pembezoni   tu ya barabara". Huze alipokata simu alimgeukia Watson na kumwambia, "Kaila tayari yupo nguvuni mwao, ndiyo wanatoka kule Mchikichini walipomnasa. Nasikia walivamiwa na wahuni wa huko walipokuwa kazini"
                      "Siyo mbaya ilimradi ameweza kumpata, huyu kijana ninamjua jinsi alivyo ni hatari akitoa habari. Anaaminiwa na  watu mno, itakuwa  mbaya  hii", Watson alisema.
                      "Hebu tujiandae  twondoke mahala hapa,  tuwahi kule. Wewe utabaki kwenye gari mimi ndiyo nitakaowasimamisha na kuingia  garini mwao. Utafuta nyuma Watson"
                      "Hakuna tabua juu ya  hilo"
      Watu hawa kwa  pamoja walitoka ndani ya nyumba waliyopo, ambayo haikuwa mbali kutoka ilipo shule ya sekondari Loyola. Waliifuata njia kwa pamoja hadi wakaja  kutokea Kigogo kwa Luhanga, napo walinyoosha moja kwa moja hadi walipofika mzunguko wa magari Kigogo. Watson aliegesha ari kando, Huze  ndiye pekee aliyesimama upande wa  ambao magari yenye kutoka Ilala hupita. Alisubiri hapo kwa muda mrefu  hadi akachoka,  hakuona dalili ya kuja  vijana wao. Mwishowe aliamua  kuwapigia simu lakini  haikuwa ikipatikana, alitukana tusi  zito kwa tukio hilo ana akaendela kusalia  wima kama mlingoti  wa bendera.
 
 
      Huze alichoka kusubiri,  aliamua kuondoka hapo na kuelekea mahali alipo Watson akimsubiri. Alifika na kuingia garini huku akiwa haelewi ni kitu gani kimetokea, alitarajia angeweza kuwaona vijana aliyowatuma mahala hapo ila ndiyo hivyo amechomeshwa mahindi. Alikaa kwenye kiti akiwa na hasira kuu, hakujua ni  kitu gani kimewakumba watu wale wake.
                    "Haijawahi kujitokeza hii, yaani wanipe ahadi kama wanakuja halafu nisiwaone  hadi muda huu. Kibaya zaidi simu yao haipatikani",  Alilalamika huku akimtazama Watson.
                      "Kipi kilichowapata hawa, hawajawahi kushindwa kazi kwa mtu mdhaifu kama yule. Imekuwaje hadi yakatokea haya?", Watson naye aliuliza maswali ambayo alifahamu fika Huze asingeweza kuyajibu.
                      "Yaani maswali hayohayo unayoniuliza ndiyo yapo kichwani mwangu, nilitamani hata nikuulize wewe. Norbert yupo wapi, au wamevamiwa kwa  mara nyingine. Na anayefanya kazi hii ya uvamizi ni nani, yupo kwa ajili ya nani?"
                      "Nahisi huyu Kaila kwa kukisia kwake jambo hilo, wakubwa wameamua kumpa ulinzi kwa haraka. Maana wamehisi kama kuna msaliti anaweza kumfuata kwa nyuma, nahisi Kaila analindwa"
                       "Watson kwa sasa hatuwezi kuweka uhakika asilimia mia moja kwenye ishu hiyo, washa gari twondoke hapa kama wamevuka muda sidhani kama watafika hawa. Washakatwa kauli", Huze  alimwambia  Watson akionesha kuchanganyikiwa haswa, Watsona hakuwa  na hiyana aliwasha gari na kuanza kutembea kwenye njia ya pembezoni mwa   barara hadi alipoingia njia kuu. Alinyoosha moja  kwa moja kufuata njia iendayo kwa Luhanga, huku akiwa na mawazo tele juu ya jmabo lililojiri. 
**
 
      Jambo ambalo hawakulijua kina Huze ni kwamba, simu waliyowapigia vijana wao na kuongea nao walikosea haswa kwenye mpango wao. Daima wao hutumia watu wenye kutambuana kwa ishara maalum, ila kwenye kazi hiyo wamewaagiza wa kawaida tu ambao hupigiwa simu  bila ya kuwa na ishara. Dharau  zao juu Kaila, ndiyo   imeleta haya laiti kama wangeweza kutilia maanani basi wangelimaizi mapema kama mambo yameviza.
     Alipiga simu majira ambayo Norbert yupo na warembo wale garini, aliipokea na kutulia kimya  bila ya kuongea chochote. Hakujua huo ni sehemu ya mtego aliyowekewa, yeye akaongea kwa papara na hapo ndipo Kaila akajua sehemu ya mpango  ilikuwa  vipi. Aliamua kutunga uongo papo kwa hapo na kumweleza, hapo ndipo alimfanya  mtu yule amweleze hadi jinsi alivyovaa na mahali ambapo anamsubiri.
     Kaila alipomaliza hilo, aliichukua namba ya simu ya mtu yule halafu akazima simu ya  mtu aliyejiua kule Mchikichini. Alimpita maeneo ya Kigogo, ambapo alimshuhudia vyema jinsi alivyo  na  pia aliweza kumtambua kwa kuwahi  kukutana naye. Alibaki akishangaa ni jinsi gani  mtu yule yupo  kwenye mnyororo huo, alimtilia  shaka ni wa kwanza kuanza kupelelezwa kwenye kazi yake ambayo imeanza kuzaa matunda siku hiyohiyo.
    Warembo wale alifika nao  hadi maeneo ya Magomeni mapipa, hapo  mmojawapo alishuka na mwingine akasalia garini. Bwana huyu jinsi alivyo na tamaa, alianza kupanga shambulizi  la kinywa lenye kulegeza misimamo ya kinadada. Majira hayo yupo barabara ya Morogoro, alienda hadi alipovuka Manzese kwa mbele alikata kona na kupita njia ya  mkato ambayo ilimpelekea kuja kutokea Buguruni.
     Binti naye kwa jinsi pombe zilivyomkolea kichwani mwake, hata hakukumbuka kama msamiati wenye neno kukataa kichwani mwake. Alikubali moja kwa moja na hata humo ndani ya gari alianza kufanyiwa utalii  wa viganja, mwishowe kwa pamoja waliangukia kwenye hoteli ya kisasa iliyopo jirani  na kituo cha daladala cha Rozana.
 
**
 
    Asubuhi na mapema, eneo la Mchikichini, kulijaa maaskari haswa  baada ya kukutwa miili mitatu  ya watu wasiyofahamika. Watatu wakiwa wapo barabarani mwingine akiwa yupo majanini ndani ya uzio.
   Tukio hilo lilipelekea wanafunzi wanaofika mahala hapo kwa ajili ya kusoma, wasipate huduma hiyo kwani maaskari waliziba njia  wakifanya utafiti wao. Watu walikaa mbali kutazama  miili ile ambayo majira hayo, ilifunikwa mashuka meupe. Hakuna aliyethubutu kusogea karibu na hapo, waliishia kutazama tu wasielewe baadhi ya mbinu za kitafiti zilizokuwa zikifanywa na maaskari hao.
     Kutoka kona moja  kwenye njia inayoelekea ulipo mtaro wa maji machafu yatokayo kiwanda cha bia. Huze alisimama akiwa pekee na macho yake yote yakiwa upande  eneo  ambalo wanausalama wakifanya kazi yao. Asubuhi hii aliamua afike hapo akiamini angeweza kunasa  mawili matatu, eneo hilo la uswahilini aliona ingekuwa ni vigumu kwa mtu  kufanya tukio lile na asionekane. Loh! Hakujua siku iliyopita kama ilipooza baada ya kukatika kwa umeme, hivyo wengi walisogea eneo la juu kufanya  biashara zao  na hata harakati zingine ikiwemo biashara. Maeneo ya uswahilini asilimia kubwa huchangamka usiku kukiwepo na umeme, lakini giza likianza basi watu asilimia kubwa hubaki  majumbani mwao au wanasogea mahali pengine. Muda uliyofanyika tukio  hilo, vijana wenye kuweka kijiwe huko, hawakuwepo walishatoka muda mrefu sana.
 
      Aliendelea kusalia mahali alipo, hatimaye akapiga hatua kwa taratibu hadi akasogea mbele ambapo kulikuwa na kundi la  vijana waliyoweka kikao wakiongea. Alijikuta akiangukia hapo  na kusikiliza huenda angeweza kupata fununu ya kile kilichotokea. Huze akiwa hapo ndipo alipomsikia kijana mmojawapo akisimulia tukio lile, huyo alieleza kwa kina juu alichokishuhudia. Tena aliongea kwa sauti ya chini akihofia huenda maaskari wangemfikia na kumtaka awe shahidi, au kumuweka ndani kwa usalama wake.
       Kijana aliyefahamika kwa jina la Rambo alieleza yeye alishuhudia watu wale wakimvamia mtu mmoja  ambaye aliwekewa silaha kichwani mwake. Alisema ilibaki kidogo wamchukue, ila kuliingia watu wawili wenye  gwanda za   mabaka ambazo hakuwahi kuziona,  tena wakiwa hawana  kofia.
                  "Rambo mtu wangu uliweza kuwaona vipi hizo nguo wakati umeme ulizima huku?", Kijana mmojawapo alimuuliza.
                   "Majamaa nyinyi acheni tu mimi nilikuwa natokea huku chini napandisha juu, sasa si wakanipita huku wanakazana yaani mijibaba hiyo imeenda hewani. Fikiri hapo kunipita namna hiyo ningewezaje  kutowaona. Basi majamaa si nikawapotezea na  kuchapa lapa kuelekea hukohuko wanapoelekea, kufika hapo kona si ndiyo nikawaona wakimsevu  jamaa aliyejikunyata katikati ya mtu nne. Yaani mtu nne kwa mtu mbili, ulitembezwa mkono acheni tu, ila majamaa najiuliza zile gwanda ni za wapi?", Rambo alieleza.
                    "Si hazifanani kabisa za jeshi ila ni mabaka?", Mwingine aliuliza.
                    "Hizohizo mtu wangu", Alijibu.
                    "Man  hao ni usalama tu hakuna jingine, hii ishu ni  nzito majamaa tujikataeni hapa kama wamefika huku jueni kuna kesi nzito. Majamaa tena tuhame kijiwe kwa mwezi hivi, huku  bondeni si mnajua kuna mapusha  kibao"
                     "Hapo umenena, sasa hivi tukasizi  jangwani kule", Mwingine alitoa rai, vijana hao walipokuwa wakiongea hao hawakujua kama mmojawpao hakuwa mwenzao kajipandikiza tu. Naye alipopata habari aliondoka upesi, aliwaacha watu wale wakiamka mmoja baada ya mwingine na kuhama eneo hilo.
      Huze alitembea kwa taratibu akaingia kwenye vichochoro mbalimbali, alienda kutokea lilipo jeno la klabu  ya  Yanga eneo la jangwani. Hapo aliingia kwenye gari aina ya toyota alteza iliyopo pembezoni mwa barabara, aliketi kiti cha upande wa pili baada ya dereva kisha akatazama mahali ambapo yupo mshika usukani wa humo ndani.
                       "Watson ndiyo nini hii, hivi unashindwa kujua kama makirikiri wanamchunga Kaila. DG Moses Gawaza si mtu wako wa karibu lakini, ulishindwa vipi kutojua hili?", Huze alilalama kwa maswali mfululizo.
                        "Unajua  hapa nilipo hata sielewi ni kitu gani unachokiongea wewe, hao watu uliyowataja mwenye kutoa kibali chao ni DG Gawazza au Sponsor pekee. Hivi itawezekana vipi jambo la kupewa kibali iwe haraka namna hiyo, hili suala halijafika TISS lipo mikononi mwa JWTZ. Sasa hao watakuwa vipi wanamlinda", Watson alisema.
                         "Unabisha nini wakati mimi ndiyo niliyekuwa eneo la tukio, ninachokwambia shuhuda yupo ni teja mmoja hivi. Yaani yeye kaeleza vijana wetu walishafanikiwa kumfikia Kaila, ila  ndiyo wakaingia makirikiri wawili wakawamaliza wote. Hivi unajua wale ni mafala sana, tumewakataza kutumia silaha kwenye  kazi hii ila ikibidi, tena tukaambia wanapaswa kuziacha tu na hiyo kazi waicheze kiakili tu.  Nasikia walikuwa na silaha"
                         "Ila nafikiri huyu Kaila si mtu wa kawaida, ni  TISS atakuwa na si vinginevyo. Huyu kafanya hivi  kwa  makusudi kuwaingiza mkenge, kuhusu silaha wala tusiwalaumu kwa  kweli"
                        "Come on Watson! Yaani mtu alivyo mwoga kama kunguru  hadi akajikunyta chini hadi walipofika wale majamaa. Kaona wakipigwa watu wetu ndiyo Kaila kapata upenyo kakimbia, utasemaje huyu ni mmoja wao. Anafuatiliwa nyendo zake tu hakuna jingine, hii ishu inabidi ujue ni namna gani ikatokea jambo kama hili, ili tujue tutajipanga namna gani. Ila Kaila hapaswi kuwa hai"
 
**
 
         Huze alipoondoka na watu wote kutawanyika kule bondeni,  vijana nao kuchukua njia yao hakujua kama amechezewa mchezo kwa mara nyingine. Mtu mwenye kutumia akili nyingi, nguvu kidogo amefanya kazi yake. Aliamini amepata kile alichokuwa kikitaka kuhusu tukio la vijana wake, ila hakujua kama ni sehemu ya hadaa amewekewa.
        Rambo pamoja na mwenzake yule ambaye alishauri wahame kijiwe kwa mwezi,  waliondoka kwa pamoja na kujichanganya mitaani hawakwenda  upande ambao mateja wengine wameelekea. Wao waliingia kwenye lango  kubwa  la nyumba mojawapo ya kupanga, huko walipitiliza uani ambapo kulikuwa na vyumba vingi na wanawake wengi wakiongea mambo mbalimbali. Hawakuonesha hofu yeyote  zaidi ya kupita na kuja kutokea mlango wa nyuma wa uzio ndani ya jengo hilo, huo waliufungua ambapo waliiona gari ya  Norbert ikiwa  ipo   karibu kabisa na mlango wa nyuma upo wazi. Waliingia ndani moja kwa moja wakafunga, gari ilianza kuondoka eneo hilo  upesi.
                   "Kazi imeendaje?", Kaila aliyekuwa yupo kwenye usukani aliwauliza.
                   "Mkuu kama ulivyotupa ndiyo imeenda namna ileile, yaani tumefanikiwa kuwaonesha ni namna gani tukio lilelimetokea. Mwenzangu hapa Muki ndiyo kaamua kawatajia wale ni wanausalama na kuwashauri mateja wahame kijiwe", Rambo alieleza.
                    "Vizuri sana, yule mtu ambaye mlimwona  pale alifika kujiunga na nyinyi", Kail aliuliza.
 
                     "Yaani kama ulivyosema atakuja, na kweli kaja kusikiliza na kuondoka mahala pale", Muki alijibu.                       "Vizuri sana vijana EASA  haikukosea haswa kuwapandikiza eneo lile muishi kama mateja. Nadhani umuhimu wenyewe ndiyo huu, kazi yenu imeishia hapa, mzigo wenu ushaingia kwenye akaunti zenu, ofisi imejua kama mmetumika kwenye misheni hii kwa ghafla"
                      "Tunashukuru  Bosi"
 
ITAENDELEA


  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4