SEPTEMBER 1 SEHEMU YA TATU

ILIPOISHIA JANA
Ilimbidi Kaila akubali kuondoka na binti huyo, tena akampakia ndani ya gari ambayo amepewa kwa ajili ya kufanyia kazi. Angeanza kumkatalia na msichana ndiyo kageuka ruba baada ya kuona gari la kifahari alilonalo kijana huyo.Pia jina kubwa alilojitengenezea Norbert kwenye uandishi wa habari ndiyo lilimfanya aone ni bahati ya mtende hiyo, angeanza vipi kumwacha aondoke tu na alimpa ahadi tamu kipindi anaongozana naye.
ENDELEA NAYO SASA.....
Yakijiri hayo, waziri wa ulinzi nchini Tanzania alifika kituo cha mwisho cha treni zenye kiwango cha kimataifa ambacho kimekamilika kikisubiri kufunguliwa tu ndiyo kianze kutumika. Alifikia kukagua na kujiridhisha mwenyewe kuwa kazi imekamilika, kutokana na jukumu hilo kukabidhiwa JWTZ ambalo lipo chini ya wizara yake. Yeye ndiyo aliwajibika kuja kuona sehemu ya kazi hiyo na si mtu mwingine.
Muda mchache baadaye kiongozi huyo alipanda helikopta maaluma ya kijeshi, alifikishwa hadi jijini Dar es salaam ambapo aliendelea na shughuli nyingine ikiwemo kuhakikisha maandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa treni unafanyika ipasavyo. Kufikia siku hii tayari wanausalama walishaanza kufika kwenye kituo kikubwa cha rali hizo kilichpopo jijini eneo la Pugu.
Siku ambayo ilitakiwa kuzinduliwa, Rais wa jumhuri ya muungano wa Tanzania. Ndiyo angepanda chombo hicho ambacho kingeenda hadi jijini Mwaza iwe sehemu ya kutimiza uzinduzi wake. Ndiyo maana walifika mapema kwenye eneo husika, walihitaji haswa kuona usalama wa Amiri jeshi unakuwepo kama ambavyo wajibu wao unavyopaswa.
Majira hayo wakiendelea na kukagua na kulinda pia kuweka makazi jirani na kituo cha kikuu cha usafiri wa SGR. Tayari vichwa na mabehewa yalishawasili bandarini, huku vingine vikingojewa kwa hamu kubwa kufika siku za usoni vije kupunguza kero ya usafiri na pia kutumia kitambo kifupi kufika jijini Mwanza kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Hekaheka hizo vituo mbalimbali vya televisheni vilionesha, huku watanzania wakishangilia mno huku wakisubiri kwa hamu kubwa siku ya siku waweze kutumia aina mpya ya usafiri wa haraka kutoka Dar es salaam hadi Mwanza.
Norbert hakuwa na jinsi, alihakikisha Halima amepata chakula cha mchana, ndipo alipoweza kuagana naye. Hakutaka siku hiyohiyo aweze kutumia kitanda kimoja naye, kwani mwenye kazi nzito iliyopo mbele yake. Alihitaji muda wa kutulia baada ya kuachana na binti yule, ili ajue anaweza kuanzia wapi kwenye kufanya utafiti wa kina juu ya jukumu alilopewa.
Alipohakikisha yupo peke yake, ndipo alipotoka na kurejea ofisini kwake ambapo hutambulika kama ni makao ya mwandishi wa habari. Alifika hapo akamkuta katibu muhtasi akiendelea na majukumu mengine, Kaila alimsabahi binti huyo ambaye anaujua mwili wake kisha akaingiza mizigo hadi ofisini mwake na kujifungia.
Ndani aliweka picha mezani na kuanza kuzitazama moja baada ya nyngine, kisha akafungua faili lile alilokabidhiwa na kuanza kulisoma kwa kina hadi akafikia mwisho wake.
Kitendo cha kupitia mwanzo hadi mwisho, kwa jinsi akili inayofanya kazi kwa upesi. Alishamaizi wapi kwa kuanzia kwenye kazi hiyo, alifikiri mahali ambapo wengi hawakuwa wamedhani kama ndiyo kungeweza kumpa mwangaza.
Kanali Seba, ndiyo jina lililomjia kichwani mwake majira hayo. Alihitaji haswa kuonana na mtu huyo, tena bila ya kumpa taarifa ya kufikia kwake. Akifikia uamuzi huo alishapanga tayari namna mabvyo angeweza kumwingia, afisa wa jeshi aliyehitaji kumwona.
Hatimaye alifunga faili hilo pamoja na picha zote, akafungua saraka maalum iliyopo humo ndani kwenye moja ya kabati la kuweka mafaili. Aliweka humo vitu vyote kisha akalifunga kwa namba maalum, humo aliamini rekodi hizo zipo mahala salama hakuna ambaye ataweza kuzifikia.
Alipotimiza hayo moja kwa moja alikimbilia simutamba yake, aliipekua akionekana ni mwenye kutafuta kitu. Hatimaye aliiweka sikioni na kutulia kwa sekunde kadhaa halafu akasema, "Belinda nahitaji kujua nyendo zote za Kanali Seba, kila anapotoka ofisini hapo makao makuu. Naamini ni mwenye utaratibu maalumu aliyojiwekea kila atokapo hapo Ngome................nipo kazini Belinda ni muhimu kulijua hilo haraka iwezekanavyo naamini yeye ndiyo wa kuanza naye kwenye kazi yangu........................nashukuru sana, pamoja na kuwa afande mwenye cheo kikubwa bado unajua nyendo za wa chini yake. Mumeo ninahisi unataijua kila hatua yake hata chooni kakaa mkao gani kwenye haja.....................(huku akicheka) sawa niite nyau, ila ulitegemea nimtanie nani kama siyo wewe. Tuzime hii kama vipi baadaye, ninaingia kazini hivi sasa".
Kaila alikata simu na kusema, "hekoo!". Kwa haraka aliuchukua mkoba wake wa namba na kuingia nao kwenye chumba kilchopo humo ofisini. Dakika kumi baadaye alitoka akiwa na nguo nyingine, nadhifu. Shati jekundu juu, shini akiwa na suruali nyekundu pamoja na viatu vyenye rangi nyuesi na nyekundu sehemu ya pembeni. Hakika alipendeza mno kwa mavazi hayo, huku machoni akiongeza miwani ambayo ilimwoneshakama vile ni matatizo ya macho.
Norbert alitoka kwa mara nyingine, alifika hadi nje na kuingia garini mwake akiwa amejua ni wapi pa kuanzia juu ya upelelezi wake. Aliondoa gari mahala hapo, akichukua uelekeo wa Upanga.
**
Kanali Sebastian Mwende maarufu kama Kanali Seba, ni mzee wa makamo aliyetumia muda mrefu akiwa jeshini kwenye majukumu mbalimbali ya kikazi. Hadi kufikia majira hayo alielekea umri wa kustaafu na akiwa na miaka miwili jeshini, pamoja na hilo bado aliendelea na utumishi wake mkubwa huku baadhi ya wakuu wake wa kazi wakimpongeza kwa kazi kadhaa alizowahi kuzifanya.
Utumishi wake jeshini wengi waliujua, haukuwa wa kubeza na alishapatiwa pongezi kadhaa ambazo huonekana kwenye vazi lake kila alivaapo. Ameshiriki operesheni nyingi za kijeshi nje ya nchi, kazi aliyoifanya huko haikuwa ya kuikashifu kabisa.
Muda ambao Kaila anatoka ofisini kwake, yeye alishapanda gari lake la kazini. Aliongoza moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake, afisa huyu aliishi Mbezi kwa muda mrefu tangu ana cheo cha chini hadi kufikia huko na hakuwahi kubadili makazi. Hadi majira hayo ni mkazi wa huko, kutoka kazini ni mwenye kufuata ulekeo huo.
Alipofika Mbezi luxury, dereva wake aliingiza gari ndani ya uzio wa 'luxury pub' ambayo kuna eneo lenye kujificha na watu hupendelea kunywa. Alifikia kwenye meza iliyopo chini ya mti, hapo alianza kuagiza kinywaji akiendelea kupoteza mdua kabla hajaelekea nyumbani kwake.
Muda mchache baadaye, kiti cha jirani naye kilivutwa na kupelekea atazame ni nani huyo anayekaa hapo. Hakuwa na kawaida ya kukaa na mtu akifika, ndiyo mana akatoa macho kushangaa. Alikutana na sura ambayo haikuwa ngeni kwake, hii ilimfanya aachite tabasamu .
"Ohoo! Norbert Kaila mwanahabari bora wa mwaka, karirbu sana", Alimlaki mgeni wake.
"Shukrani sana Kanali Seba, nimeshakaribia ingawa mimi si mkaaji wa eneo hili. Nimepita mara moja tu ndiyo nikaona gari yako hapa. Nikaona kukupita bila hata kukusalimia haitokuwa vizuri", Norbert alisema huku akiketi.
"Na kweli ungenipita tu hapa ningekulaani mpaka nakufa kama ningekuona, nisingekuona jua mzimu wangu ungekuandama hadi unaingia kaburini. Ungekuwa hujafanya haki kabisa"
"Ndiyo na mzimu wangu mimi ukanifanya nisimame hapa, nilipokuwa natoka nyumbani kwa Luteni Mfuruki", Kauli hiyo ilimfanya Kanali Sea akae vizuri kitini kisha akatupa jicho kwa umakini.
"Mfuruki kijana hodari sana kutoka bomb squad mwenye degree ya engineering"
"Huyohuyo yaani nimeenda walua kujua chochote, si unajua kazi yetu hii ni ya kupekua. Aisee inasikitisha sana kamanda kwa nilichokisikia huko, tena kwa rafiki yake wa karibu"
"We Kaila unajua jambo unalolifuata si la mchezo kabisa, lipo ndani ya jeshi wewe kama mwandishi ulifumbua kwa jamii kabla ya msemaji mkuu hajalisema. Utajipalia makaa kijana wangu"
"Siko kwa ajili ya kulifunua afande, kama unavyojua sisi vijana wa kusaka habari hata kama hatuna haja ya kuianika tunapenda tu kujua vitu. Yaani upekuzi upo kwenye damu unanichemka mno"
"(Akitabasamu) Unajua wewe ulifaa kabisa kuwa mpelelezi, ila ndiyo hivyo umeangukia kwenye uandishi. Ndipo ndoto zako zilipofikia, haya niambie kijana mwenye kujua kupekua na kukimbia kipi ulichokinusa huko"
"Ebwanaeh! Afande nasikia kuna mmoja kati ya wakubwa zake ndiyo wasaliti, habari hii ndiyo niliyoinasa. Hadi kupotea kwake na maafisa wengine wa ndani ni sehemu ya hila ya ofisa huyo, anashirikiana na na wahalifu", Norbert aliposema hayo, Kanali Seba alikuwa akinywa bia iliyopo kwenye bilauri. Kusikia habari hiyo kulimfanya anusurike kupaliwa.
"(Akiwa bado kashikilia bilauri) Kaila are you sure? Hii ni serious ishu ujue hadi raia wa kawaida huko anaijua"
"Ndiyo hivyo Afande hata mimi nimeshangaa hii ni habari ya ndani kaijua vipi huyo na nasikia ni wengi mno wanijua"
"Sasa sikia nikwambie kijana wangu, hii habari iishie kwako. Nikitoka hapa nawasiliana na wakuu nijue ni jinsi gani tunaweza kuitatua"
"Hakuna shaka Afande, wacha niwahi nyumbani mara moja nina kiporo cha kazi nimekiacha kinahitajika kuchapishwa mwezi Septemba tu"
"Hakuna shaka Kaila, ila sijapenda kabisa himahima hivi hata kinywaji hujaagiza"
"(huku akiinuka) Nahitaji kufanya kazi nzito ndiyo maana ikawa hivi. Usihofu muda mwingine tukikutana nitaagiza na mimi ninywe"
"(Wakipeana mikono) Hakuna shida" Kaila aliondoka mahala hapo, huku akimwacha Kanali Seba akiwa na mawazo mengi juu ya taarifa ile. Pamoja na kutumia kilevi haikuweza kumfanya aondokwe na kumbukumbu hadi kushinda kulitafakari hilo. Siri ya ndani ya jeshi kutoka nje kirahisi namna hiyo, ilihali alikuwa na uhakika kwa asilimia mia moja mwandishi huyo hakuwa akijua chochote.
Hakujua hisia za namna hiyo juu ya kupotea kwa maafande wenzao zimetoka wapi, zimesababushwa na nini hadi mtu kuweka mawazo namna hiyo kiasi cha kuyaweka kwa wengine. Pasipo kutambua analichafua jeshi, hakika lilimkanganya mno hata pombe yenyewe ikawa haina maana kuendelea kunyweka.
**
Norbeert baada ya kuondoka Mbezi, alifika hadi Ubungo ambapo alinyoosha barabara ya Morogoro na akaja kutokea Magomeni. Hapo alikata na kuingia kwneye barabara iendayo Kigogo. Alienda na njia hiyo akavuka njia panda ya Kigogo, hadi alipofika Ilala kwenye jengo la
UWT.
Kaila aliingia upande wa kushoto wa barabara hiyo, akaingia mitaani ambapo alienda moja kwa moja hadi akaja kusimama jirani na kilabu cha kunywea pombe kilichopo karibu na ukumbi wa chama cha siasa ambao hutumika sana na wacheza 'karate'. Hapo aliweka gari mahali salama na kisha akaingia ndani ya kilabu hiko, akiwa ni mwenye mwendo wa madaha alienda kuketi kwenye kiti ambacho meza yake imejitenga.
Aliagiza kinywaji na kutulia mahala hapo, alifika hapo akiwa na lengo maalum ambapo aliona bado muda mwafaka wa kutimia kwake haujafika. Majira hayo ya jioni alikata kinywaji chake kisicho na kilevi, huku akiperuzi kwenye simu mara kadhaa na hata kutupa macho eneo ambalo yupo kwa usalama wake. Macho yake hayakutulia hata, kama ambavyo inamtaka jasusi kutotuliza mboni yake kwa usalama wake.
Masikio aliyeweka tayari mithili ya popo anafuata sauti yake kipindi cha usiku ili imwongoze asijigonge kwenye giza. Kaila kila mlango wake wa fahamu ulikaa kinamna ya kipekee, hii ndiyo kawaida yake aliyoizoea hakuwa mwenye kujiamini kupitilzia na kujiona yupo salama kila muda.
Muda mchache baadaye, mezani hapo walifika mabinti wawili waliyovaa magauni mafupi na kuomba kuketi naye. Hakuwa na ajizi zaidi ya kukubali hilo, maana hakuwa na mgeni yeyote aseme angewazuia kuketi. Wasichana hao walipoketi tu walianza kuagiza vinywaji, ambapo wote waligiza vilevi. Norbert kufikiwa na wageni hakuwa na budi kuongea nao tu, ingawa bado akili yake ipo makini kutafakari mambo na macho yake hayatulii. Hakuna mtu aliyemwona kama ni mwenye kuzungusha mboni, kutokana na miwani aliyoivaa ilizuia macho yake majira hayo giza likiwa limeanza kutamalaki.
Majira ya saa moja ikielekea saa mbili, alishuhudia wanaume wanne wakiwasili mahala hapo. Hawa walivaa mavazi tofauti, na walifika pamoja ila katika kuketi kwenye viti walijigawa na kila mmoja kachukua uelekeo wake na walionekana kama wasiyojuana.
Norbert alitazama hao hadi mahali walipoketi na kisha akaendelea na kinywaji chake, muda mchache baadaye alimaliza chupa moja. Akawa na nyingine ambayo haijafunguliwa, mzee wa kazi hakutaka iwekwe wazi pale mhudumu alipofika kutimiza jukumu lake. Alimwambia mpaka arudi ndiyo itakuwa wazi, alipoacha maagizo hayo aliinuka na kuwaomba warembo wale wamtazamie kiti halafu akatoka nje ya kilabu hicho.
Alifuata barabara iendayo bonde la mchikichini, alitembea kwa tahadhari huku akigeuka nyuma na kutazama yeyote kama anakuja. Kuzurura kwake hatimaye alikuja kufikia kwenye mteremko uendao kwenye mabanda ya walimu wa ziada mchikichini. Alitembea kwa kasi kubwa, ila alipofika kwenye kona iliyopo jirani na njia iendayo kwenye banda la mwalimu maarufu wa hesabu. Jirani na ukuta kuukuu uliyochoka. Alijikuta akiwa yupo katikati ya watu wanne, ambao si wageni machoni mwake na kila mmoja majira hayo alionekana akiwa ni mikono mitupu.
"Whats wrong jamani, naombeni njia", Kaila alisema huku akiwa hana wasiwasi.
"Norbert Kaila wewe si unajua kunusa sana, sasa hapa ndiyo uitatueleza nani huyo aliyekwambia kina Mfuruki wametekwa", Mmoja wa watu wale alisema na kupelekea Kaila aachie tabasamu kama vile wanafanya mzaha.
"Hivi majamaa kweli mpo serious nyinyi, hebu wacheni zenu majamaa nawahi kuwapelekea unga mapusha. Nipisheni"
Kauli hiyo ya Kaila akiitoa, macho yake yalicheza na kutazama kila mmoja wao yupo kwenye mkao gani. Alitaraji haswa kupokea shambulio la nyuma, kwani waliyopo pembezoni wasingeweza kufanya hivyo. Hawa watu alitambua ni wenye kumfuata na kumuhitaji akiwa mzima, hadi kufikia kujua aliyempa habari ile ambayo alimweleza Kanali Seba. Alihisi ni lazima huyo aliyepo nyuma yake angeweza kuleta pingamizi, akili ya kimakabiliano iliamka.
Kweli hakuwa tofauti na hisi zake zilivyo, mtu aliyepo nyuma alileta konde la kisogoni na kumpelekea ayumbishe shingo kwa haraka kuelekea kushoto. Ngumi ya mtu ile ilipopita tu na aliudaka mkono wake, kitendo cha haraka aliunvunja na kupelekea mpinzani huyo atoe yowe la maumivu. Wa upande wa kulia naye hakulaza damu, alileta teke ambalo lilikuwa likija usawa wa mbavuni mwake. Loh! Alidhani angeweza kumpiga ila haikuwa hivyo, Norbert alimgeuza yule aliyemvunja mkono maana bado hakuwa amemwachia, alimpeleka upande huo. Teke likampata yeye katikati ya mfupa wa mgongo.
Kitendo cha kumuweka upande wake wa kulia yule aliyevunjika, alimwachia kwa upesi baada ya kukutana na mateke mawili yakija. Moja ya aliyekuwa kushoto, jingine la yule aliyeonekana mbele yake kabla hajageukia huko. Alibonyea chini kwa haraka, akiwa huko alitulia kwa viganja vya mikono pasipo makalio kugusa chini, miguu alifyatua kuelekea mbele ambapo ilitua kwenye magoti ya warusha mateke hao. Doh! Kila mmoja alivunjwa mguu aliyosimamia, pindi anarusha pigo lake na hapo ndipo wakasalimiana na ardhi.
Norbert akiwa chini akitumia mihimili ya viganja, aliinua mkono wa kushoto kisha akauleta mwili upande wa kulia. Aligeuka na kutazama ardhi huku mgongo ukiwa juu kama vile ni mwenye kutaka kupiga 'pushapu'. Tendo alilifanya kwa upesi kukwepa pigo ya yule aliyempiga teke mwenzake kimakosa, na alipotua namna hiyo alitumia nguvu nyingi za mikono kujisukuma juu na hatimaye akasimama wima na kutazamana adui yake. Hakuchelewa alimletea mapigo ya karate mfululizo, hadi akamchakaza kwa muda mchahetu. Alipoanguka chini alimmaliza hapohapo, hakulaza damu aliwafuata na wale wengine waliyovunjika miguu akawamaliza.
Alibaki na mmoja pekee ambaye alivunjwa mkono pamoja na kuteguliwa mgongo, huyu alimvuta na kumtupia upande wa ukuta mchakavu sehemu ambayo kuna uwazi. Kaila alikamilisha kazi yake pasipo kuonekana na kiumbe wa aina yeyote, kukatika kwa umemem eneo la
Mchikichini ikawa ni faida kubwa kwake. Aliruka ukuta huo na akatoke upande ambao yupo majeruhi wake, bado hakuwa ameinuka na alimburuza hadi kwenye mti na kumuegemeza.
"Katika watu wapumbavu duniani basi nyinyi ni miongoni mwao, nilipoleta taarifa kwa Kanali Seba haikuwa ya kweli na wala sikuwa nimefika mtaa anaoishi Luteni Mfuruki. Nilicheza kamari, mtu kama Afande Seba ni mwenye kutoa taarifa upesi na yeye ndiyo alikuwa karibu na baadhi ya maafisa wa Bomb squad. Nilijua kuna msaliti ndani sasa ndiyo kawaagiza nyinyi", Norbert alisema.
"Norbert unacheza na moto usiyouweza, fikiria utaishi vipi hapa jijini. Utawindwa tu hata kama utatuua sisi", Mtu yule alisema huku akihema kwa tabu.
"Ndiyo mtaanzia wapi, kwanza nani aliyekuagiza mahala hapa"
"Usitegemee kama nitakuwa mwepesi kufungua mdomo wangu, umechelewa Kaila nishalamba kola yangu", Mtu huyo aliposema hivyo aliegemeza kichwa upande wa kushoto, hiyo ni ishara tosha ameshakata kauli.
"Shenzi!", Norbert alisema, halafu akaanza kumpekua mtu yule kwenye nguo zake. Cha muhimu alichokichukua ilikuwa ni simu pamoja na pochi ya mtu huyo baaada ya kuhakiki haina hatari yeyote ile. Aliondoka humo ndani kwa kutokea upande mwingine wa uzio, huko alitembea hadi akafika eneo ambalo kuna kituo kidogo cha shirika la umeme Tanzani.
Norbert eneo hilo ndipo alipojihakiki na kuona kama alichafuka, mikono pekee ndiyo aliiona ina vumbi ambapo aliishia kununua maji alipofika kwenye kibanda kilichopo jirani na ukuta wa kiwanda cha bia cha TBL.
Alipohakikisha yupo nadhifu ilevil,e alijifuta jasho na kuisafisha miwani yake halafu kule kilabuni alipokuwa hapo awali. Aliwasili na kuwakuta warembo wale bado wapo mezani, wakiendelea kunywa.
"Mkaka sisi tulitaka kuondoka ujue, sijui hapa mezani ingekuwaje", Mmoja wa vipusa wa wale alisema.
"So sorry cutes, nilifika kule Ilala Boma kuna rafiki yangu tulienda kuonana naye mara moja. Hata mimi si mkaaji, nabeba kinywaji changu hiki niondoke", Norbert alisema.
ITAENDELEA
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment