Ads Right Header

Buy template blogger

WARWANDA WANAHAHA KUIPATA SAINI YA KAGERE

WARWANDA WANAHAHA KUIPATA SAINI YA KAGERE


MEDDIE Kagere, mshambuliaji namba moja wa Simba bado Klabu ya APR ya Rwanda imekomaa kuisaka saini yake kwa ajili ya msimu ujao.

APR inaamini kwamba ikimpata Kagere itakuwa na nafasi ya kupeta kwenye michuano ya kimataifa kutokana na uzoefu wa nyota huyo kwenye mechi kubwa na ngumu.

Kagere aliweza kutimiza majukumu yake vema msimu wake wa kwanza 2018/19 na timu yake ilitinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi  ya Mabingwa Afrika jambo linalowafanya APR wazidi kuhaha kuipata saini yake.

"Mpango mkubwa wa APR inahitaji kupata saini ya Kagere na inahitaji pia kumboreshea zaidi mkataba wake ili iwe ngumu kumtoa akishasaini pale," ilieleza taarifa hiyo.

Eto Mupenzi, wakala anayewauzia wachezaji APR amesema kuwa:"Kuna mpango wa kuboresha thamani kwa wachezaji watakaotua ndani ya APR hivyo ishu ya Kagere bado sijajajua ipoje lada tusubiri," amesema.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4