Chanjo za Ebola zaanza kutolewa Congo
Wahudumu wa afya kaskazini magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza kutoa chanjo baada ya mlipuko wa 11 wa Ebola kutangazwa wiki iliyopita.
Waziri wa Afya Eteni Longondo ameliambia shirika la habari kutoka Mbandaka kuwa zoezi la utoaji chanjo lilianza Ijumaa, na tayari wahudumu wa afya wameshapata chanjo hiyo, pamoja na watu waliokuwa karibu na visa vilivyothibitishwa vya maambukizi.
Amesema wana dozi 1,500 na wameagiza nyingine 8,000 zaidi ili kuwahudumia watu wengi wa Mbandaka. Zaidi ya watu 300,000 tayari wamepewa chanjo ya Ebola katika mlipuko uliotokea mashariki mwa nchi hiyo.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Leave Comments
Post a Comment