Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Wapalestina waandamana dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi



Makumi ya Wapalestina wanaoishi katika mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wameandamana kupinga mpango wa utawala wa Kizayuni ambao unalenga kuteka ardhi zaidi za Wapalestina katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa, Wapalestina waliokuwa na hasira pamoja na viongozi kadhaa wa makundi ya Kipalestina siku ya Jumatatu walishiriki katika maandamano makubwa katika Medani ya Al Manar katikati mwa Ramallah na kubainisha upinzani wao dhidi ya mpango wa utawala wa Kizayuni wa kukalia kwa mabavu eneo la Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa Wasl Abu Yusuf, mwanachama wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO), taifa la Palestina limeungana katika kupinga mpango wa  Wamarekani-Wazayuni wa eti 'Muamala wa Karne' na kuunganishwa ardhi zaidi za Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.


Naye Mahmoud Al Aloul, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Palestina pia amesema taifa la Palestina halikubali mapatano na utawala wa Kizayuni huku akisisitiza kuendelea mapambano ya kisheria kwa ajili ya kukombolewa Palestina na kuundwa serikali huru ya Palestina.

Kwa mujibu wa mpango wa Wamarekani-Wazayuni wa 'Muamala wa Karne', utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kuteka asilimia 30 ya ardhi  za Palestina kuanzia Julai Mosi kwa himaya ya Rais Donald Trump wa Marekani.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4