Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Jamii yatakiwa kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kujikinga na malaria


Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman ameitaka jamii kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kujikinga na malaria kwa kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa.

Hayo ameyasema huko katika  Shehia ya Sogea Wilaya ya Mjini  wakati alipokuwa akizindua ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa vikiwa na lengo la kujikinga  na malaria kwa  wananchi katika baadhi ya shehia zenye maambukizi.

Amesema Wizara ya Afya  ikishirikiana na Serikali za Wilaya itaendesha zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa katika baadhi ya shehia ambazo zinaonekana bado zinamambukizi ndani ya Wilaya ya Mjini, Magharib A na Magharib B. 

Hivyo amewaomba wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kwa lengo la kujikinga Malaria na kuacha tabia ya kuvitumia kwa mambo mengine ikiwemo kuzungushiwa bustani za mboga mboga.

“Tunawajibu wa kuthamini juhudi za Serikali zinazofanywa kwa wananchi wake ili wawe na afya bora na kutokomeza kabisa maradhi ya malaria kwani iwapo tutakuwa na mashirikiano na kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya Zanzibar bila ya Malaria inawezekana,” alisema Naibu wa Afya.

Amesema wananchi katika shehia nyengine  wataendelea kupata vyandarua  kwa utaratibu wa kuchukua kuponi kwa masheha wao na kwenda katika vituo vyao  vya afya kupatiwa vyandarua.

Pia amesema wagawaji wa vyandarua watazingatia taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa  corona wakati wa zoezi hilo kwa kuvaa barakoa , kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa glove wakati wote.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas amewaomba masheha kuhakikisha vyandarua hivyo vinawafikia walengwa kwa mpango uliyowekwa na kuwataka wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kama vilivyokusudiwa na Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Kinga na elimu ya Afya Dk. Fadhil Mohammed amewataka wananchi kufuata miongozo ya Wizara ya Afya kwa kuweka mazingira safi  ili kuepuka  mbu wasizaliane.

Nae Sheha wa shehia ya Sogea Abdullah Mohamed Abdullah na Diwani Mohamed Said Mohamed wamesema watahakikisha wananchi wanavitumia vyandarua hivyo  kujikinga na ugonjwa wa malaria.

Jumla ya vyandarua 197,000 vitagawiwa kwa  kaya 90,000 za wilaya zote tatu  katika shehia 52 zikiwemo shehia 32 Wilaya ya Mjini, shehia 10 Wilaya ya Magharib A na Shehia 10 Wilaya ya Magharibi “B”.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4