Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

CHADEMA yawataka kujitokeza ugombea nafasi ya urais wa Zanzibar


Naibu katibu Mkuu wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA, Zanzibar Salum Mwalimu amewataka wanachama wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar  katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu 2020.

Wito huo umetolewa leo  katika Ofisi Kuu za Chama hizo kwa Zanzbar, zilizopo Kisiwandui Mjini Unguja, Salum Mwalimu kila mwanachama ambaye anahisi anasifa ya kuogombea nafasi hiyi ni vyema kujitokeza kuwania nafasi hiyo.

“Kuanzia leo Juni sita (6) tunatangaza nafasi kuwa wazi kwa yule yoyote ambaye anataka kutangaza nia ya kugombea Urais wa kupitia tiketi ya chama chetu cha CHADEMA,”alisema Salum Mwalimu.

Aliongeza kueleza kwamba hadi sasa nafasi hiyo haina mtu hivyo kwa mwenye nia ya kutaka kugombea kujitokeza kuanzia leo Juni 6 hadi Juni 15, 2020.

“Sasa basi wenye nia ya makusudi wanatakiwa kuleta barua kwa katibu Mkuu wa Chama kupitia ofisi za Naibu katibu Mkuu Zanzibar kwa ajili ya michakato ya ndani huku akiwa ameambatanisha taarifa fupi za maisha yaani CV, na wale ambao wpo mbali Pemba na sehemu nyingine wafanya mawasiliano na ofisi ya katibu Mkuu Zanzibar iki kuweza kukamilisha kusudi lao,” alisema  Salum Mwalimu.

Hata hivyo Salum Mwalimu alisema kwamba anaamini ushiriki wa chama chake katika kila hatua za Uchaguzi Mkuu zitakuwa za Amani na bila ya kufanya vurugu y aina yoyote.

“Kuanzia hatua hii ya kutangaza nia hadi katika kinyanga’nyiro cha  uchaguzi Mkuu chadema hatuta fanya vurugu ya aina yoyote ile tutaendesha kwa amani na utulivu,”alisema Salum Mwalimu.

Aidha alisema kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamefanikiwa kuandaa mipango maalumu iliyoleta maboresho kupitia Ward,Majimbo na Mikoa kwa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA, Zanzibar.

Alieleza kwamba hadi sasa jumla ya watu 180 walijitokeza kugombe nafasi mbalimbali ya Ubunge,Udiwani,Uwakilishi kupitia chama hicho.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4