LITTLE YAPANUA WIGO WAKE WA UTOAJI HUDUMA YA USAFIRI KATIKA MIJI YA DODOMA, ARUSHA, MWANZA
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KAMPUNI ya Tax ya kimtandao LITTLE inayotoa huduma za usafiri kwa wateja sasa imepanua wigo wake wa huduma rasmi katika Jiji la Dodoma, Arusha na Mwanza,hiyo ni kutokana na ongezeko kubwa la uhutaji ,
LITTLE ilianzisha huduma zake katika Jiji la Dar es salaam nchini Tanzania mwaka 2019, ilikumuhakikisha urahisi mteja ambaye atapaswa kulipia Sh. 500 kwa kilomita na Sh. 80 kwa dakika atakazotumia.
Akizungumzia upanuzi huo,Mkuu wa Operesheni Little Tanzania Eddsteve Mwangalimi amesema kuwa maono ya LITTLE ni kuwa mtoa masuluhisho ya usafiri barani Afrika.
"Tumeshuhudia ongezeko kubwa la uhitaji wa huduma zetu katika nchi mbali mbali Tanzania ikiwemo , hii imepelekea kupanua wigo wa huendeshaji Dodoma , Arusha na Mwanza kutokata na uhitaji mkubwa wa huduma,"amesema.
Ameongeza kuwa LITTLE inatoa fursa kwa madereva taxi kujiongezea kipato zaidi na tayari wameshasajiri madereva taxi zaidi ya 100 kila mkoa wakiwa wamekwishapatiwa mafunzo katika viwango vyetu vyaki kampuni ili kuhakikisha ubora wa huduma unazingatiwa.
"Kampuni ya LITTLE ni ya Kiafrika iliyoanzia Kenya katika Jjiji la Nairobi, kampuni ipo katika nchi nne sasa ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, na Zambia.
"LITTLE inaendelea kutoa masuluhisho ya changamoto mbalimbali kwa aina ya kipekee na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma iliyo bora, rahisi na unafuu , Little App inapatikana Google play store na App Store,"amesema Mwangalimi.
Leave Comments
Post a Comment