UBALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA WAZUNGUMZIA SIKU YA KIMATAIFA YA MCHEZO WA YOGA ULIMWENGUNI KOTE, WAANDAA SHINDANO MAALUMU KUELEKEA JUNI 21,2020
Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya kimataifa ya mchezo wa Yoga ulimwenguni ambayo hufanyika kila Juni 21 ya kila mwaka ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha Watazania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili.Wengine ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto) na Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(kulia).
Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akifafanua jambo kuhusu Siku ya kimataifa ya Yoga ambayo hufanyika kila Juni 21 ya kila mwaka. Wengine ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto),Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(aliyevaa suti ua bluu) na kulia ni Katibu Raj Ganger.
Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(kushoto) akizungumza kuhusu Siku ya kimataifa ya Yoga ambayo inaratajia kufanyika Juni 21 mwaka huu.Kulia ni Katibu wa Pili katika ubalozi huo Raj Ganger.
Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli akizungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuuweka mwili katika hali nzuri kiafya huku akiwa amekunja mguu kama ishara ya kuwa vizuri katika eneo la mazoezi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto)akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kushiriki mashindano ambayo yamedaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kuelekea siku ya kimataifa ya mchezo wa Yoga.Wengine ni Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli, Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa India nchini Tanzania R.Chandramouli(kulia), na mwisho kulia ni Katibu wa Pili katika ubalozi huo Raj Ganger.
Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(katikati) akielezea jambo kuhusu siku ya Yoga leo Juni 17,2020 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli(wa pili kushoto waliosimama juu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandhishi wa habari waliosimama chini pamoja na maofisa wengine wa ubalozi huo nchini.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja(kushoto) akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu siku ya kimataifa ya Yoga ulimwenguni.Kulia ni Balozi wa India nchini Tanzania Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIKA kuelekea Siku ya Kimataifa ya mchezo wa Yoga ulimwenguni kote ambayo ni Juni 21 mwaka huu, Ubalozi wa India nchini Tanzania umewahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazeozi kwani yanafaida kubwa mwili ikiwemo ya kuongeza kinga ya mwili.
Mbali na kuhamasisha watu kufanya mazoezi , Ubalozi huo umeeleza ili kufanikisha siku hiyo ya Yoga wameandaa shindano la mazeozi pamoja na kuhamasisha Watanzania kushiriki kwa kutuma video fupi fupi zinazoonesha wakifanya mazoezi na washindi watashinda fedha taslimu ambazo zitatolewa na Balozi wa India nchini Tanzania Sanjiv Kohli,
Hata hivyo kwa safari hii katika kuadhimisha siku hiyo ule utaratibu wa maelfu ya watanzania kukutana na viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam na kushiriki mchezo wa Yoga kwa pamoja hautakuwepo kutokana na janga la Corona ambalo limesumbua duniani kote.Hivyo safari hii Yoga itafanywa na watu katika maeneo yao yakiwemo ya nyumbani.
Akizungumza leo Juni 17,2020 ,Balozi wa India nchini Sanjiv Kohli ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa mchezo wa Yoga ambao kila ifikapo Juni 21 ya kila mwaka huadhimisha katika mataifa mbalimbali duniani."Niendelee kutoa rai kwa wananchi wa Tanzania kuungana na wananchi wa India kushiriki kwenye mchezo huu ambao umejizolea umaarufu mkubwa duniani kote tangu ulipoanzishwa.
"Katika kipindi hiki ambacho Dunia inapita kwenye kipindi cha janga la Corona, mazoezi ni muhimu sana na uanasaidia kuongeza kinga za mwili na hivyo mwili kuna na uwezo wa kukabiliana na magonjwa na hasa yanayoshambulia kinga za mwili,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Swami Vivekananda Santhoth Raja amefafanua zaidi kuwa washindi watakaopatikana watapata fursa ya kushindanishwa kidunia.Shindano hilo litaendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwamo ukurasa wao wa Facebook, Twitter na Instagram.
Raja ametaja kusara za mitandao yao ni https://www.facebook.com/IndiaIntanzania/,https:www.facebook.com/swami-Vivekananda-cultural-centre-Dar-es-Salaam-582559985117910.
Akielezea zaidi kuhusu shindano ya mchezo wa Yoga, Raja amesema kwamba washiriki ni watu wa rika zote na jinsia zote, hivyo jukumu lao litakuwa ni mshiriki kutuma video fupi ya dakika tatu ambazo zitakuwa zinaonesha wanavyofanya mazoezi wakiwa nyumbani.
Ameongeza kuwa shindano hili linatarajia kufanyika Jumapili ya Juni 21 mwaka huu na nchi mbalimbali duniani zitashiriki."Hivyo tunaomba Watanzania kushiriki kwa wingi , zawadi mbalimbali na hasa za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi.Kutokana na ukubwa wa siku ya kimataifa ya Yoga , mataifa 177 yamefadhili mashindano hayo,"amesema.
Kuhusu zawadi za kwa washindi , Raja amesema kuwa washindi watapata fedha kuanzia Sh.200,000 hadi 300,000 kulingana na rika na kutakuwa na mshindi wa kwanza hadi wa tatu kila kundi kutokana na video fupi zitakazotumwa.
Wakati zawadi kwa washindi wa pili watapata fedha kuanzia Sh. 150,000 hadi 250,000 kulingana na kundi huku washindi wa tatu kwa kila kundi watapa fedha Sh. 100,000 hadi Sh.200,000.
Leave Comments
Post a Comment