MABINGWA WA LIGI KUU BARA KUREJEA LEO DAR ES SALAAM
BAADA ya jana, Juni 28 kulazimisha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, leo Simba inarejea Dar es Salaam.
Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa na mechi sita mkononi baada ya kufikisha jumla ya pointi 79 ikiwa imecheza mechi 32.
Pointi hizo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi, Yanga ikiwa nafasi ya pili ina pointi 60 ambapo ikishinda mechi zake itafikisha pointi 78 na Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 59 ikishinda zote itafikisha pointi 77 zote zikiwa zimecheza mechi 32.
Leave Comments
Post a Comment