MKANDARASI AAGIZWA KUPELEKA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI KWA BODI YA REA

Na Woinde Shizza,ARUSHA
MKANDARASI anayetekeleza mradi wa Wakala wa Nishati vijijini REA mkoa wa Arusha ameagizwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miezi mitatu alichoomba kuongezewa.
Agizo hilo lilitolewa na mjumbe wa Bodi ya REA Taifa Henry Mwatwinza alipokuwa akikagua mradi unaotekelezwa na Serikali kwa awamu ya tatu mzunguko wa kwanza uliotakiwa kukamilika June 30 mwaka huu kwa mkoa wa Arusha .
Aidha Mwatwinza alimtaka mkandarasi huyo kuandaa taarifa inayoeleza namna wanavyotekeleza mradi wa REA 3 mzunguko wa kwanza katika miezi mitatu walioomba kuongezewa.
"Awali mradi huu ulipaswa kukamilika juni 30 lakini ifikapo mwisho wa mwezi huu muwe mmeshaleta taarifa inayotoa maelezo kamili yanayojitosheleza namna ambavyo mmejipanga kukamilisha maeneo yaliyobaki kufikishwa umeme huu wa REA, ikiwezekana andaeni taarifa inayoonyesha kazi itakayofanyika kwa siku, wiki na mwezi ili kupima muda na kazi iliyobaki" alisema.
Alimtaka kuhakikisha kuwa taarifa hiyo imeshirikishwa Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya zote ambazo mradi huo unapita.
Aliongeza kuwa endapo mkandarasi huyo atashindwa kutekeleza mradi huo kwa muda alioomba kuongezewa ni dhahiri kuwa amejiondoa mwenyewe katika mradi wa REA kwa kuwa atakuwa ameshindwa kusimamia makubaliano.
Naye Peter Gohima mkandarasi kutoka Kampuni ya NIPO anayetekeleza mradi huo alisema kuna baadhi ya changamoto zilizokuwa nje ya uwezo wao ambazo zimefanya washindwe kukamilisha kwa wakati akitaja moja wapo kuwa ni ucheleweshwaji wa baadhi ya vifaa husika.
Mjumbe wa mradi wa Wakala wa Nishati vijijini REA HenryMwatwinza Akiongea na mkandarasi anayetekeleza mradi wa Wakala wa Nishati vijijini REA mkoa wa Arusha kutoka kampuni ya NIPO group wakati walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua kazi mkandarasi huyo alizozifanya juzi, ambapo alimtaka kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miezi mitatu alichoomba kuongezewa.(picha Woinde Shizza)
Na Woinde Shizza,ARUSHA
MKANDARASI anayetekeleza mradi wa Wakala wa Nishati vijijini REA mkoa wa Arusha ameagizwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miezi mitatu alichoomba kuongezewa.
Agizo hilo lilitolewa na mjumbe wa Bodi ya REA Taifa Henry Mwatwinza alipokuwa akikagua mradi unaotekelezwa na Serikali kwa awamu ya tatu mzunguko wa kwanza uliotakiwa kukamilika June 30 mwaka huu kwa mkoa wa Arusha .
Aidha Mwatwinza alimtaka mkandarasi huyo kuandaa taarifa inayoeleza namna wanavyotekeleza mradi wa REA 3 mzunguko wa kwanza katika miezi mitatu walioomba kuongezewa.
"Awali mradi huu ulipaswa kukamilika juni 30 lakini ifikapo mwisho wa mwezi huu muwe mmeshaleta taarifa inayotoa maelezo kamili yanayojitosheleza namna ambavyo mmejipanga kukamilisha maeneo yaliyobaki kufikishwa umeme huu wa REA, ikiwezekana andaeni taarifa inayoonyesha kazi itakayofanyika kwa siku, wiki na mwezi ili kupima muda na kazi iliyobaki" alisema.
Alimtaka kuhakikisha kuwa taarifa hiyo imeshirikishwa Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya zote ambazo mradi huo unapita.
Aliongeza kuwa endapo mkandarasi huyo atashindwa kutekeleza mradi huo kwa muda alioomba kuongezewa ni dhahiri kuwa amejiondoa mwenyewe katika mradi wa REA kwa kuwa atakuwa ameshindwa kusimamia makubaliano.
Naye Peter Gohima mkandarasi kutoka Kampuni ya NIPO anayetekeleza mradi huo alisema kuna baadhi ya changamoto zilizokuwa nje ya uwezo wao ambazo zimefanya washindwe kukamilisha kwa wakati akitaja moja wapo kuwa ni ucheleweshwaji wa baadhi ya vifaa husika.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment