Mshukiwa mkuu katika mauaji ya Floyd afikishwa mahakamani
Derek Chauvin, polisi wa zamani ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya George Floyd, amewekewa dhamana ya dola milioni moja. Chauvin mwenye umri wa miaka 44, aliunganishwa na kikao cha mahakama kwa njia ya video akiwa gerezani, mjini Minneapolis, jimbo la Minnesota.
Aidha haruhusiwi kufanya kazi katika nafasi yoyote kwenye idara ya usalama. Polisi wengine watatu wa Minneapolis walifikishwa mahakamani wiki iliyopita wakikabiliwa na mashitaka ya kusaidia katika mauaji ya Floyd. Wote wanne wamefutwa kazi.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Leave Comments
Post a Comment