RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU OINTI TATU ZA NDANDA KESHO
RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU OINTI TATU ZA NDANDA KESHO
UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa maandalizi ya mchezo wao kuvaana na Ndanda kesho Uwanja wa Mabatini yapo vizuri.
Kesho Ruvu Shooting itakuwa na kibarua cha kumenyana na Ndanda FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Meja Mstaafu, Abdul Mingange.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa utapigwa mpira kama Barcelona vile ili kupata pointi tatu muhimu.
"Tupo vizuri na kila mchezaji anatambua kwamba ni lazima apambane ili kuipa ushindi timu yake, tutaendelea kupiga mpira kama Barcelona kwani kasi yetu inajulikana," amesema.
Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 30 kibindoni ina pointi 40.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment