Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Serikali na wadau wahimizwa kuendelea kutoa elimu ya unyanyapaa kwa walemavu wa ngozi(Albinism)




Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Ikiwa tunaelekea katika kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi Duniani(albinism) ambayo huadhimishwa juni 13 kila mwaka Duniani kote, inaelezwa kuwa bado tatizo la unyanyapaa na uelewa wa ulemavu huo miongoni mwa jamii hasa maeneo ya vijijini bado ni mdogo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo juni 6, 2020 jijini Dodoma Muasisi wa shirika lisilokuwa la kiserikali  la  foundation for disabilities hope(FDH) Michael Silali, amesema pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na seriakali pamoja na wadau mbalimbali kuwapa uelewa jamii na kupungua kwa tatizo hilo lakini bado kunachangamoto miongoni mwa jamii.

Amesema maeneo mengi bado kunauelewa mdogo wa maswala ya ulemavu wa ngozi albinism na hawajajua namna ya kuishi na watu hao na kupelekea kuwanyanyapaa walemavu hao.

“kutokana na maadhimisho tunayofanya kila mwaka yamesaidia kuongeza uelewa  hapa tulipo kwa sasa ni nitofauti na mwanzo kabisa elimu imewafika jamii lakini kuna baadhi ya maeneo unyanyaa paa na ukatili bado upo na jitihada za makusudi zinahitajika” amesema Silali.

Amesema kutokana na maadhimisho na hamasa wamefanikiwa kuibua na kuzitatua changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amebainisha kuwa tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwakumba walemavu wa ngozi ni tatizo la salatani ya ngozi na limekuwa ni tatizo ambalo limekuwa likichukua maisha ya walemavu wa ngozi wengi na kubainisha kuwa katika maadhimisho hayo hutumia kuongeza uelewa kwa wazazi juu ya ugonjwa huo kwa walemavu wa ngozi.

“Niombe serikali na wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia kuondoa tatizo hili la salatani ya ngozi kwa walemavu ili waondokane na tatizo hilo” amesema.

Ameomba Serikali kusaidia kuagiza mafuta kinga ya ngozi kupitia bohari ya dawa(MSD) badala ya kuacha mafuta hayo kuagizwa na watu binafsi ambapo inapelekea kuwa na bei kubwa na baadhi ya watu kushindwa kumudu gharama hizo na wengi wao kupata kirahisi salatani ya ngozi ambayo huwatesa sana watu wenye ulemavu wa ngozi.

Ameongeza kuwa “serikali iliagiza kila halmashauri kutenga fedha kwa ajiri ya mafuta kinga kwa walemavu wa ngozi lakini kuna baadhi ya halmashauri hazitengi bajeti hiyo naiomba serikali kuzifuatilia halmashauri hizo” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo Bi Epiphania Kabunduguru, amesema shirika hilo lilianzishwa mwaka 2016 na kupatiwa usajili wake mwaka 2019 na limekuwa likijishuhurisha na utetezi wa haki na usawa makundi mbalimbali ikiwamo walemavu, na husaidia makundi hayo katika afya, ujasiliamali na utetezi wa haki za walemavu.

Nae Katibu wa shirika hilo frank sakindi amesema katika maadhimisho hayo watatumia kuwakutanisha watu wenye ulemavu wa ngozi ili kuwapa faraja na wao wajione kama watu wengine, na ili kuwezesha shughuri hiyo wameomba wadau mbalimbali kujitikeza kusaidia chochote ili kuwezesha shughuri hiyo itakayofanyika katika hotel ya morena Dodoma kwa kutuma mchango wao, CRDB 0133480838100 na tigo pesa 0655910114.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4