Ads Right Header

Buy template blogger

FRANK DOMAYO WA AZAM FC ATUMIWA UJUMBE HUU

FRANK DOMAYO WA AZAM FC ATUMIWA UJUMBE HUU


WADAU wa michezo wamempa neno nyota wa Klabu ya Azam FC, Frank Domayo kwa kumtaka aendelee kwenye asili yake ya kucheza soka la umakini kwa kuwa sio kawaida yake kucheza rafu ndani ya uwanja.

Kwenye mchezo uliochezwa jana, Julai Mosi mbele ya Simba, Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 ambapo Domayo alionekana akimchezea rafu beki wa Simba Shomari Kapombe.

Leo Kapombe anatarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa tatizo lake kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandnbroeck.

Kilanga Mselemu amesema kuwa soka sio vita hivyo ni lazima kuwa na umakini katika vitu ambavyo wanafanya wachezaji ndani ya uwanja na sio kutegemea kuomba radhi.

Melak Kapinga amesema kuwa Domayo ni mchezaji mzuri na jambo ambalo amelifanya jana sio kawaida yake anadhani inatokana na jazba ya mpira wa jana hivyo lazima asamehewe ili mambo yazidi kusonga mbele.

 Ushindi wa Simba unaipa tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ambayo inatarajiwa kuchezwa mwezi huu Julai.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4