Ads Right Header

Buy template blogger

PROF NDALICHAKO AKABIDHI VYEREHANI 10 KWA WAHITIMU WA MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MPANDA

PROF NDALICHAKO AKABIDHI VYEREHANI 10 KWA WAHITIMU WA MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MPANDA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametimiza ahadi ya kutoa vyerehani 10 kwa wanafunzi waliohitimu​ mafunzo ya ushonaji kutoka Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi​ Mpanda​ wanaotoka katika mazingira magumu.

Akizungumza katika halfa hiyo Mkoani Katavi, Prof Ndalichako amesema ahadi hiyo aliitoa​ mwaka 2018 baada ya kuwakuta vijana wadogo wamemaliza masomo ya darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari​ na kujiunga na mafunzo ya ushonaji katika chuo hicho kupitia msaada wa kanisa.

​“Mwaka juzi nilifika katika chuo hiki na kuwakuta hawa vijana wawili wadogo wakiwa katika mafunzo ya ushonaji na nilipozungumza nao niligundua kuwa wametoka katika mazingira magumu, hivyo kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari, ndipo nilipowaahidi kuwapatia vyerehani watakapomaliza ili viwawezeshe kujiajiri.​ Hata hivyo, nimetoa vyerehani 10 ili na wengine wenye mazingira ya namna hiyo waweze kupata,” amesema Waziri Ndalichako.

Aidha, Waziri huyo amemuagiza Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Mpanda kuona namna ya kuwapatia nafasi ya kuendelea na ngazi nyingine ya mafunzo watoto hao​ ili kuwawezesha kuwa mahiri katika ushonaji na kuhakikisha anawasimamia na kuwashauri popote watakapokuwa wanafanya shughuli zao.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Mpanda Elisha amemshukuru waziri kwa kutimiza ahadi aliyoitoa mwaka 2018 kwani inakwenda kuinua watoto wanaotoka katika familia masikini, na kuahidi kuendelea kuwasimamia ili cherehani hizo ziwe na manufaa kwa watoto wenyewe na familia zao.

Mmoja wa wanafunzi waliopatiwa cherehani Gift Giles amemshukuru Waziri kwa kuwapatia cherehani hizo ambazo zinakwenda kubadili maisha yao kwani zitawawezesha kupata fedha ambazo zitawasaidia kujiendeleza katika masomo
​​
Naye mmoja wa walezi wa wanafunzi hao Bibi Flora Cosmas amemshukuru Mhe. Ndalichako na kuahidi kuwasimamia ili waweze kutumia machine hizo vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza zaidi kiujuzi.

"Sisi walezi wa vijana hawa tunamahukuru sana Mhe. Waziri​ kwa kuguswa kwake kuamua kwa moyo wake kufanya jambo hili kubwa maana anakwenda badili naisha ya vijana hawa ambao hawakuwa na uwezo wa kununua hizi cherehani" amesema bi Cosmas.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi fedha taslimu kiasi cha Sh. 500,000 kwa mmoja wa wanafunzi wa VETA Mpanda aliowapati cherehani  kwa ajili ya kununulia vifaa vya kuwawezesha kuanza kushona ili waweze kujiingizia kipato.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja  na wanafunzi wa VETA Mpanda wanaotoka katika mazingira magumu mara baada ya kuwakabidhi cherehani alizoahidi kuwapatia
 Mhitimu wa mafunzo ya Ushonaji kutoka VETA Mpanda Gift Giles (miaka 16) kutoka katika mazingira magumu akionesha chereheni aliyokabidhiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4