Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

DK.MAGUFULI AINADI ILANI YA UCHAGUZI MKUU 2020 YENYE KURASA 303 ZINAZOZUNGUMZIA MAENDELEO

DK.MAGUFULI AINADI ILANI YA UCHAGUZI MKUU 2020 YENYE KURASA 303 ZINAZOZUNGUMZIA MAENDELEO

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Igunga

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema kwamba Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 inakurasa 303 ambayo imeagiza mambo mengi ya kufanyiwa kazi kwa maendeleo ya Watanzania wote.

Amesema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika leo Septemba 2,2020 mkoani Tabora ambapo amepata fursa ya kunadi sera na Ilani ya Uchaguzi katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida pamoja na Wilaya za Igunga na Nzega mkoani Tabora.

“Ilani ya mwaka huu ina kurasa 303 na imeagiza mambo mengi sana ya kufanya.Tunaamini zaidi ya CCM hakuna anayeweza kufanya, kwanza hawajui hela inatoka wapi, wanaamini hela inatoka Ulaya wakati hela iko hapa,”amesema Dk.Magufuli alipokuwa na maelfu ya wananchi akiwa mkoani Tabora.

Akiwa wilayani Igunga Dk.Magufuli pamoja na mambo mengine amesema kwa mambol makubwa ya maendeleo ambayo yamefanyika kwa kipindi cha miaka mitano ni imani yake wananchi watamchagua tena kuongoza kwa miaka mitani na hatarajii wamnyime kura.

“Nimekuja kuomba tena kwa Watanzania kwani sitaki kuona Taifa hili linaangamia au likaingia kwenye mikono ya watu matapeli na waongo.Tunataka liendelee kubaki kwenye mikono salama ya Serikali ya CCM.”

Pia amesema hataki kufanya dhambi ya kusema uongo mbele ya Watanzania na hasa wazee kwani anachotamani ni kuona hata siku moja akienda mbinguni Malaika wawe sehemu ya kuelezea mambo mazuri aliyofanya.”Ikiwezekana wanipe hata Uwaziri.”

Hata hivyo amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi kuleta maendeleo yakiwemo yanayoonekana katika mkoa wa Singida na Tabora.”Najua wapo watu wenye maneno matamu wataahidi kila kitu, hata sisi wanaume huwa tunadanganya.

“Niwaombe mtuamini viongozi wa CCM , nichagueni mimi, nichagulieni wabunge na madiwani wa CCM.Wananchi wa maeneo haya naomba tuangalie mahali mlipotoka, tangu historia ya Rais wa kwanza wa Taifa letu hadi leo hii, kuna mabadiliko makubwa sana,maendeleo yamefanyika na tutaendelea kufanya mkitupa nafasi,”amesisitiza Dk.Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo wa Igunga kuwaliuza kwani amefanya nini baya.”Nani hajui yaliyofanyika , hakukua na barabara hapo awali, lakini leo zipo kila mahali.Tabora ninyi mnafahamu hali iliyokuwepo hapo zamani.”

Pia ameomba Watanzania kuendelea kuliombea Taifa ili livuke salama katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu huku akiwaomba viongozi wa dini zote kuendelea kuliombea Taifa letu libaki salama.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4