Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

WANANCHI WAFURAHIA UPATIKANAJI WA MAJI MIHAMBWE

WANANCHI WAFURAHIA UPATIKANAJI WA MAJI MIHAMBWE

Na Mwandishi wetu, Mihambwe.

WANANCHI, wamefurahia upatikanaji wa maji safi na salama ambapo wameaswa kuilinda na kuitunza miradi ya maji iliyopo na itakayoanzishwa kwa manufaa ya sasa na ya baadae kwa kuwa Maji ni uhai, Maji ni maisha.
 
Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kwenye
ziara yake ya kukagua miradi ya maji kwenye Tarafa yake ambayo
imesaidia kupunguza tatizo la maji.

"Serikali ya Rais Magufuli inajitahidi kuleta huduma za Maji mpaka
maeneo ya vijijini.. inaleta furaha kwa jamii. Leo nimetembelea miradi
ya maji kwa kata mbili tu, nimejionea ilivyo mkombozi wa kero ya maji
iliyokuwepo awali. Wananchi wanaendelea kunywa Maji safi na salama
yanayopatikana muda wote. Niwaase miradi hii ya maji itunzwe vyema kwa
manufaa ya sasa na ya baadae" alisema Gavana Shilatu.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa tatizo la maji lilikuwa kero kubwa kwa Wanawake ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kusaka maji usiku na mchana.

"Tunaishukuru Serikali kutupatia mradi huu wa maji, hatupati tena
shida kama awali. Tunaomba miradi hii idumu na tuzidi kuboreshewa
huduma zaidi." Amesema Bi Zuhura Mohammed Kwambika mkazi wa kijiji cha
Mwenge B kilichopo kata ya Kitama.

Katika ziara hiyo ya Gavana Shilatu aliambatana na Maafisa maendeleo
kata, Watendaji vijiji pamoja na uongozi wa kamati husika za maji
ambapo alitembelea miradi ya maji iliyopo kata ya Kitama na kata ya
Mihambwe ambayo inahudumia zaidi ya vijiji 13

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4