Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 11 & 12 (Return Of Olivia Hitler)



ILIPOISHIA
“Baba amekufa au?”
Xaviela alizungumza huku wasiwasi ukimuisha moyoni mwake kwani kama ni mkataba wake wa upendo na baba yake alisha ufuta toka jana.
“Hapana baba amempiga mama hadi amepoteza fahamu”
“NINI…………!!!???”
Xaviela aliuliza kwa mshangao huku akivuta ya taswira ya baba yake, huku moyo wake mmoja una mshauri kwenda kumuua baba yake huku nafsi yake nyingine ikimshawishi awahi kwenda hospitalini kwenda kumuona mama yake.
ENDELEA
“Ndio, amempiga leo asubuhi”
“Haki ya Mungu huyu mwana haramu nitamuua”
Xaviela alizungumza huku hasira ikizidi kuchachamaa mwilini mwake.
“Usifanye hivyo Xaviela”
“Funga bakuli lalo wewe. Amempiga mama, yaani amevuka mipaka yake. Nitamuua haki ya Mungu siwezi kumuacha”
Xaviela akakata simu, akavua gauni lake la kulalia na kuvaa suruali pamoja na tisheti. Akavaa raba za michezo na kutoka ndani humo huku akizibana nywele zake vizuri.
“Xaviela una kwenda wapi?”
Frank alimuuliza Xaviela anaye toka mlangoni kwa mwendo wa haraka. Frank ikamlazimu kutoka ndani na kumkuta Xaviela akihangaika kufungua mlango wa gari lake.
“Pumbavu. Niletee funguo nimeziacha huko ndani kwangu”
Frank akarudi chumbani kwa Xaviela na kuchukua fungu hiyo ya gari na kutoka nje.
“Sikupi funguo hadi uniambie una kwenda wapi?”
“Wewe fala nini, gari la kwako hili hadi usinipe funguo?”
Kauli ya Xaviela ikamfanya Frank kutabasamu japo ni kauli ya dharau.
“Sawa mimi ni fala ila siwezi kukupa funguo ya gari ukaondoka bila ya mimi kuweza kufahamu ni wapi una kwenda. Kumbuka kwamba upo nyumbani kwangu”
“Asiisee Franka tafadhali, kichwa changu kime vurugwa, mama yangu yupo Bombo hospital na amelazwa kwa ajili ya kupigwa na baba hadi kupoteza fahamu. So umesha jua wapi nina kwenda?”
“Ndio, ingia kwenye gari nita endesha”
“Nini wewe, nipe funguo yangu niondoke bwana”
“Ingia kwenye gari sitaki ubishi”
Frank alizungumza kwa kufoka na kumfanya Xaviela kuwa mpole kwani ana zitambua hasira za mwalimu wake huyo. Frank akafungua geti na kulitoa gari hilo, kisha akashuka na kulifunga, akarudi ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea hospitali ya Bombo. Simu ya Xaviela ikaita, akaitazama na kukuta ni namba ya mdogo wake.
“Vipi?”
“Upo wapi?”
“Nina kuja hospitalini”
“Ohoo asante Mungu”
“Vipi mama ana endeleaje?”
“Bado madaktari hawajamtoa katika chumba cha matibabu”
“Sasa mbona ume sema asante Mungu?”
“Nilihisi una kwenda nyumbani kwa baba.”
“Yaani nina kuja hapo kisha huyo baba yako nita dili naye baadae”
Xaviela akakata simu ili asiweze kupata ushawishi wowote kutoka kwa mdogo wake huyo.
“Kurwa”
Frank alimuita Xaviela jina ambalo mara nyingi ana lipenda sana. Xaviela akamtazama Frank pasipo kuitikia.
“Kuna nini kinacho endelea kwenye familia yako?”
“Sijui”
Frank hakuona haja ya kuendelea kumuhoji Xaviela. Wakafika hospitali ya Bombo, kitendo cha waandishi wa habari kumuona Xaviela wakajikuta wakimkimbilia pasipo kufahamu kwamba huyo ni pacha wa Xaviena.
“Nini?”
Xaviela alizungumza kwa hasira huku akiwatazama waandishi hao wa habari ambao wengi wao wamejawa na tabasamu wakihisi kwamba ni wakati wa wao kumuhoji miss Tanga.
“Ni nini kinacho endelea hapa miss Tanga?”
Muandishi mmoja limuhoji Xaviela. Xaviela akaachia msonyo mzito na kuwasukuma baadhi ya waandishi wa habari na kupita katikati yao.
“Naombeni mumsamehe hayupo sawa”
Frank alizungumza huku naye akiwapita waandishi hao.
“Wewe ndio boy friend wa miss Tanga?”
Swali hilo likamfanya Frank kusimama na kugeuka nyuma.
“Ndio”
“Tuambie una jisikiaje kuwa na mwanamke mzuri na mrembo kama Xaviena Eddy?”
“Ninajisikia furaha na ninajiona ni mwanaume mwenye bahati kuwa na mwanamke kama yeye. Asanteni acheni nimuwahi mama watoto ndani”
Frank alizungumza huku akiwaacha waandishi hao wa habari. Xaviena mara baada ya kumuona Xaviela akamkimbilia na wakakumbatiana. Hapa ndipo baadhi ya manesi wanao katiza kwenye kordo hiyo ndipo walipo weza kugundua kwamba Xaviena ana pacha wake ambaye wana fanana sana.
“Mama hali yake sio nzuri”
Xaviena alizungumza huku akilia.
“Mungu ata mponyesha. Hembu niambie ilikuwaje kuwaje hadi baba aka mpiga mama”
Xaviena akamuachia Xaviela taratibu, kisha akaanza kumuelezea kuanzia mwazo ni kitu gani ambacho kilipelekea wazazi hao kugombana.
“Kwa hiyo baba amemsaliti mama na ana mwanamke mwengine?”
“Ndio”
“Huyo mwamke ni nani?”
“Sijamjua”
“Haki ya Mungu nina kwenda kuwa ua wote wawili. Haiwezekani mama yangu ateseke kwa ajili ya wajinga hawa”
Xaviela alizungumza kwa hasira huku machozi yakimbubujika. Mlango wa chumba alicho ingizwa mama yao uka funguliwa. Akatoka daktari mmojaa aliye valia vazi la kijani, kofia ya kijani kichwani mwake, pamoja na kitambaa cha kijani maeneo ya mdomoni mwake. Daktari huyo akafungua kitambaa hicho na kuwatazama Xaviena na Xaviela.
“Hivi nyinyi mupo mapacha?”
“Ndio”
Xaviena alijibu huku akiwa na shahuku kubwa ya kuhitaji kufahamu ni hali gani inayo endelea kwa mama yao.
“Baba yenu yupo wapi?”
Xaviena akamtazama Xaviela anaye jikaza sana kuzungumza kauli mbaya kuhusiana na baba yake.
“A…ana dharura kidogo”
“Okay, basi nina weza kuwapa majibu ya awali ya mama yenu?”
“Tupatie tu dokta”
“Wewe kijana una husika na hawa?”
Daktari alimuuliza Frank ambaye yupo karibu nao huku masiko yake akiwa ameyatega kusikiliza ni nini kinacho endelea. Xaviena akamgeukia Frank na kumtazama, hakuweza kumfahamu kwani Xaviela haja mtambulisha na hata katika kuingia eneo hilo, Frank alikuja dakika mbili mara baada ya Xaviela kuingia ndani humo.
“Hatupo pamoja naye”
Xaviena alijibu.
“Basi sogea niweze kuzungumza na hawa vijana”
“Sogea”
Xaviela alitilia msisitizo swala hilo na kumfanya Frank kusogea eneo ambalo hato weza kusikia kinacho zungumziwa na daktari huyo.
“Hali ya mama yenu sio nzuri. Eneo la fuvu lake kwa pembeni upande wa kushoto, limeweza kuweka crake ambayo itatupelekea tuweze kumfanyia upasuaji haraka iwezekanavyo. Hivyo basi tuna hitaji mutie saini kwenye fomo ya kuruhusu kwamba aweze kufanyiwa upasuaji na mukubaliane na terms zilizopo kwenye fomu hiyo. Kwani kwenye upasuaji kuna mambo mawili yanayo weza kutokea kwa mgonjwa. Kufa au kupona”
Kauli hiyo ikamnyong’onyeza Xaviena na kumfanya apepesuke huku akihisi kizunguzungu kikali sana. Xaviela aka muwahi na kumkalisha katika moja ya viti vilivyopo katika eneo hilo. Kisha akamtazama dokta huyo.
“Nitatia saini”
Xaviela alizungumza huku akimkazia macho dokta huyo hadi akamfanya daktari aanze kupatwa na hofu.
***
Kauli ya Xaviena ikazidi kujirudia rudia kichwani mwa Eddy. Akatafuta chupa ya wisky na kuanza kuigwida huku hasira ikimtawala moyoni mwake.
“Huyu mwanamke ame wafundisha wanaye kiburi ili wanichukiiee eheee”
Eddy alizungumza kwa sauti ya kilevi sana.
“Hadi Xaviena kweli, ana nifokea? Haahaa kweli Eddy nime expire date”
Eddy alizungumza huku akiendelea kunywa pombe hiyo kali. Simu yake ikaanza kuita, akajipapasa kwenye mifuko yake ya pensi aliyo ivaa na kuitoa. Akaitazama simu hiyo huku akiona maruwe ruwe, akaipokea namba hiyo ya Olvia Hitler.
“Niambie baby”
“Safi mume wangu, upo wapi?”
“Nipo nyumbani, nina hamu sana na wewe mpenzi wangu. Una weza kuja?”
“Nyumbani kwako? Mke wako akinikuta je?”
“Ahaa sasa hivi yupo hospitalini bwana, hawezi kukukuta, ameondolewa hapa nyumbani na machela.”
“Weee ana sumbuliwa na nini?”
“Ahaa nime mvutua kidogo, ame anguka na kupoteza fahamu. Yaani jana ame nipiga teke la mashine na kunikimbia. Hembu njoo kwanza nyumbani niii test mashine yangu kama bado ni nzima”
Eddy alizungumza kwa sauti ya kilevi huku akiwa amekaa chini, pembezoni mwa kitanda chake.
“Ni hakikishie kwamba upo peke yako nyumbani?”
“Nipo peke yangu, wewe wasiwasi wa nini mama. Njoo, tena nataka kukupa vitu vitamu zaidi ya jana”
“Jamani Eddy usiongee hivyo. Yaani hapa una nifanya kisim** changu kuanza kucheza cheza kwa hamu”
“Njoo nikinyonye kisim** chako na kukisugua na kichwa cha mbo**”
“Sawa nina kuja mpenzi wangu”
“Nakupenda Olvia wangu”
“Nakupenda pia Eddy wangu”
Eddy akakata simu hiyo na kuitupia kitandani. Akaendelea kuinywa pombe hiyo kwa fujo. Baada ya dakika ishirini, simu yake ya ikaaita. Akaipokea na kuisikilizia.
“Nipo getini walinzi wako wana nikataza kuingia”
“Mpe mmoja simu”
“Haloo”
“Wewe fungua getiii hiloooo”
“Sawa sawa mkuu”
Mlinzi huyo alijibu kwa kubabaika kwani hakuwahi kuisikia sauuti ya boss wake akifoka. Olvia akapaki gari lake kwenye maegesho. Akaingia sebleni na kumkuta Eddy akiwa amesimama kwenye ngazi. Taratibu wakakumbatiana na kuanza kunyonyana lipsi zao. Wakaingia chumbani na Eddy aka mlaza Olvia Hitler kitandani na kuanza kumchojoa nguo moja baada ya nyingine.
***
Daktari bila ya kipingamizi, akamkabidhi Xaviela fomu ya kusaini, ili mama yake afanyiwe upasuaji.
“Dokta sikia. Nahitaji mama yangu apone. Akifa basi wote mulio husika kwenye upasuaji huo basi hesabuni na yinyi mume kufa kwa maana sinto muacha hata mmoja wenu akiwa hai”
Xaviela alizungumza maneno yaliyo mshangaza sana daktari. Akamkabidhi fomu hizo kisha akamsogelea Xaviena aliye jiinami.
“Wewe Frank njoo”
Frank akawafwata sehemu hiyo.
“Muangalie mdogo wangu. Ole wako apate tatizo. Nina kuja, nipe funguo”
Jinsi Xaviela anavyo zungumza, Frank hakuwa na ujanja wa kumzuia, akamkabidhi Xaviela funguo ya gari lake kisha akaondoka na kuwaacha Xaviena na Frank wakibaki wameduwaa. Xaviela hakuhitaji kuzungumza na muandishi yoyote wa habari. Akaingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi eneo hilo la hospitalini. Ndani ya dakika chache akafika nyumbani kwa baba yake, akasimamisha gari getini na kuingia kwa kupitia geti dogo huku akiwa amefura kwa hasira. Hakuitikia salamu ya mlinzi hata mmoja na wala hakuzisikia. Akafika sebleni na kutazama nyumba yao hii ambayo ni kubwa sana. Akaanza kupandisha ngazi za kueleka gorofani.
Akaanza kupiga hatua za kujiamini huku akielekea mlangoni mwa chumba cha baba yake. Jinsi alivyo zidi kuusogelea mlango huo ndivyo jinsi alivyo anza kusikia miguno ya kimahaba inayo ashiria baba yake ana mwanamke mwengine tofauti na mama yao. Xaviela akasimama mlangoni mwa chumba hicho huku hasira ikizidi kumpagawisha, akapiga teke mlango huo na kwa habati nzuri haukufungwa kwa ndani hivyo ikawa ni rahisi kwa mlango huo kufunguka na akaingia ndani.

TANGA RAHA  12 

ENDELEA
Eddy na Olvia wakastuka sana na kuutazama mlango huo. Wote hawakuamini kumuona Xaviena aliye simama akiwatazama. Kitu kilicho mshangaza Eddy ni kumuona Xaviela akiendelea kutazama tazama chumbani humo, akionekana hawaoni kabisa kitandani hapo. Xaviela akaingia bafuni huku akishangaa kuto kumuona mtu yoyote ndani humu.
“Yupo wapi huyu mshenzi lazima nita muu”
Xaviela alizungumza huku akitoka bafuni humo. Akachungulia chini ya kitanda wala hakuona mtu yoyote. Akatazama kitandani hapa wala hakuweza kumuona mtu yoyote. Akatoka ndani humo na kuelekea chumba kingine huku akimtafuta baba yake.
“Ume fanya nini mbona haja tuona?”
“Eddy mpenzi wangu, una jua mimi ni nani, si rahisi kwa mwanadamu kufanya hivi ninavyo vifanya”
“Imefikia hatua huyu mtoto ana hitaji kuniua. Mshenzi sana”
“Heii baby, huyo ni mwanao anacho kizungumza ni kutokana na hasira ya kumpiga mama yao. Ila hana uwezo wa kufanya hivyo. Hembu endelea kunipa raha mpenzi wangu”
“Atarudi tena”
“Hata akirudi hato weza kutuona.”
Olvia Hitler alizungumza huku akimnyonya Eddy lipsi zake na kumfanya aendelee na mtanange huo wa kukata kwa shoka. Xaviela kaingia kila chumba ndani ya jumba lao, ila hakuweza kumuona kabisa Eddy.
“Nimechanganyikiwa ehee?”
Xaviela alijiuliza huku akizikumbuka sauti za miguno ya kimahaba zilizo kuwa zinatokea chumbani kwa baba yake.
“Haiwezekani bwana. Nimesikia kila jambo ina kuwaje nisiwaone?”
Xaviela alizidi kujadili maajabu aliyo yasikia, hakuweza kuamini moja kwa moja akaamua kuanza safari ya kurudi tena chumbani kwa baba yake.
***
“Hei una jisikiaje?”
Frank alizungumza huku akimtazama Xaviena aliye jiinamia.
“Sipo poa”
“Uisjali, mama ata kuwa salama”
“Una mfahamu mama yetu?”
“Yaa nina wafahamu nyinyi nyote”
“Wewe ni nani?”
“Naitwa Frank, ni mwalimu wa kareti, taikondo na ndiye ninaye mfundisha dada yako maswala hayo”
“Ahaaa….kwa hiyo unaweza kupigana?”
“Kiasi sio sana”
“Kwa nini ume amua kumfundisha dada yangu mambo hayo?”
“Aha…ni maamuzi yake, aliniomba niweze kumfundisha hivyo na nikafanya hivyo”
“Una jua Xaviella ni mtu mmoja mwenye hasira za karibu sana. Pia ana maamuzi ya haraka haraka sana, hanaga kufikiria jambo mara moja na kulipambanu. Yaani pale ulipo muona amekwenda nyumbani na sijui akimkuta baba itakuwaje, ana weza hata kumuu”
Frank akastuka kidogo huku akimtazama Xaviena usoni mwake.
“Ndio anaweza hata kumuua baba. Kwani toka jana wao hawana maelewano kabisa na jana aliondoka nyumbani na sijui ni wapi alipo kuwa amekwenda”
“Ahaa sasa napata picha kamili”
“Picha gani?”
“Xaviela jana alikuja kwangu na mabegi yake. Nilipo jaribu kumuuliza habari za nyumbani, hakuweza kunipa jibu la ujakika zaidi ya kunijibu short, kutokana nina mfahamu vizuri, basi sikuona haja ya kuendelea kumuhoji”
“Ahaa ila huja mfanyia dada yangu jambo lolote”
“Una maanisha nini?”
“Huja lala na dada yangu?”
“Hapana sijalala naye, nilimpatia chumba chake kwa maana nyumba yangu ni kubwa kiasi.”
“Vizuri”
Xaviena alizungumza kwa msisitizo kwa maana ana mpenda sana dada yake na hapendi kumuona na pitia matatizo.
“Ehh Mungu nakuomba msaidie mama yangu”
Xaviena alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Kisa ni nini cha baba na mama kugombana?”
Frank alizungumza huku akimtazama Xaviena kwa umakini sana.
“Ni ishu za kifamilia hivyo siwezi kuzizungumza kwa mtu baki”
“Ahaa samahani”
“Usijali. Nasikia hapo nje kuna waandishi wa habari?”
“Ndio wapo wengi na walidhani kwamba Xaviela ndio wewe”
“Afadhali, sinto toka hadi niweze kufahamu hali ya mama ina endeleaje”
***
Xaviela akiwa karibu na chumba cha baba yake akasikia tena miguno hiyo ya kimapenzi. Akaanza kunyata ili kudhibitisha kwamba ana ona kitu kinacho endelea. Akafika karibu kabisa na chumba hicho na kuchungulia ndani, ila hakuweza kuona chochote, ila miguno hiyo ya kimahaba ina endelea.
“Nini kinacho endelea Mungu wangu?”
Xaviela alizidi kupagawa. Woga sasa ukaanza kumtawala, maajabu kama hayo hakuwahi kuyaona kwenye nyumba yao wala kwenye maisha yake. Akatoka ndani humo huku akikimbia, walinzi wa getini walipo muona Xaviela ana kuja kwa mwendo wa kukimbia wakajiandaa huku wakihisi kwamba kuna tatizo limejitokeza ndani.
“Kuna nini Xaviela?”
Walinzi hao waliuliza huku wakijaribu kusimama mbele yake. Xaviela akawapita huku akiwasukumiza, akatoka nje na kuingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi sana katika eneo hili.
“Huyu msichana ame changanyikiwa ehee?”
“Hata mimi sielewi. Si una ona jinsi alivyo kuja pasipo kutusemesha chochote kisha ameondoka kwa mtindo huo huo”
“Mmmm ila sijui kuna nini kinacho endelea ndani ya nyumba hii, naona katika siku mbili hizi watu wame vurugwa”
“Ni kweli….!! Ngoja kwanza, au ame mfumania mzee wake kwa maana si umeona yule mwanamke mrembo aliye kuja hapa?”
“Hata mimi nahisi kwa maana si kawaida mzee kuto kwenda hospitalini ikiwa mke wake ni mgonjwa”
“Hembu kachungulie ndani?”
“Baba nina penda ajira yangu. Jukumu letu ni kulinda mambo mengine tuwaachie wenye pesa zao”
Xaviela akazidi kuongeza mwendo wa gari lake huku akijihisi kuto kuwa sawa kiakili. Kile alicho kisia chumbani kwa baba yake ni tofauti kabisa na alicho kiona.
“Imekuwaje eheee?”
Xaviela alizungumza huku akiupiga piga msikani wake. Akafika kwenye mataa ya Toyota na kusimama. Foleni ya magari hiyo ikamfanya azidi kutafakari hali halisi ya nyumbani kwao. Gafla kioo cha pembeni yake kikagongwa kidogo na kumfanya atoke kwenye dibwa hilo la mawazo. Akamtazama mee anaye omba msaada.”
“Khaa ujana wenu mulikuwa wapi hadi musitafute pesa?”
Xaviela alizungumza kwa hasira huku akishusha kioo cha gari upande wake.
“Binti naomba msaada”
Xaviela akamkazia macho mzee huyu, kisha akajipapasa mfukoni mwake na kutoa noti ya shilingi elfu tano na kukabidhi.
“Asante sana binti yangu. Ila una matatizo makubwa sana kuna jini ume kutana naye leo”
Mzee huyo alizungumza huku akimtazama Xaviela usoni mwake. Maneno ya mzee huyo yakamstua sana Xaviela, honi za magari ya yaliyo simama nyuma yake, yakamfanya Xaviela airudishe akili yake barabarani, huku akiona taa ya kijani ikiwa imesha ruhusu magari ya upande wao.
“Binti jini atakusumbua sana, atakusumbua”
Mzee huyo alizungumza huku Xaviela akiondoka gari lake kwa spidi ili kuziwa hitaa hizo, zinazo waka kwa dakika chache sana.
Akafika hospital ya Bombo, akasimamisha gari lake kwenye maegesho huku hali ya mawazo ikizidi kukisumbua kichwa chake. Dirisha la kioo chake likagongwa tena na kumfanya astuke sana, akamtazama ni nani aliye gonga na kumuona Olvia Hitler akiwa amesima huku ana tabasamu.
“Mbona ume stuka Xaviela?”
Olvia Hitler alizungumza mara baada ya Xaviela kushuka kioo chagari lake.
“Olvia”
“Niambie mwamangu”
“Hembu ingia kwenye gari”
Olvia Hitler akazunguka upande wa pilia wa gari na kuingia. Xaviela akapandisha kioo huku akimtazama Xaviena usoni mwake.
“Mbona una onekana ni mtu mwenye mashaka. Mtu ambaye umepoteza matumaini yako, hembu niambie kuna nini kinacho kusumbua?”
“Yaani nina mawazo mengi sana. Mama yupo chumba cha upasuaji, anafanyiwa matibabu. Leo asubuhi baba ame mpiga hadi madokta muda ule waliniambia kwamba fuvu lake lime pata kiji nyufa kidogo.”
“Weee poleni sana, kwa nini sasa alimpiga?”
“Kwa maelezo ya dogo, ana dai kwamba baba jana alirudi usiku sana, huku akiwa ametoka kwa mwanamke mwengine. Sasa leo nimekwenda kwa baba, nikakuta gari ambalo si letu, nikaingia ndani nikasikia miguno ya kimahaba chumbani kwa baba ila nilipo ingia sikuweza kuona chochote na mbaya tv ime zimwa.”
“Yaani ulisikia miguno na hukuona chochote?”
“Ndio, na nimerudi kwa mara ya pili, nikasikia miguno kabisa kitandani ila sioni watu. Sasa nipo pale njiani kwenye hayo mataa hapo Toyota. Kuna mzee akaanza kunieleza kwamba sijui leo nimekutana na jini jini yaani nikijumlisha yale niliyo yaona nyumbani na kile alicho nieleza yule mzee haki ya Mungu nimejikuta nikichanganyikiwa sana.”
Olvia Hilter akatabasamu huku akimtazama Xaviela kwa maana leo ameweza kuichezesha akili ya binti huyo.
“Pole sana mwanangu. Sasa baba yako yupo wapi?”
“Najua basi, yaani leo ningemkuta nyumbani haki ya Mungu ninge muua”
“Ungemuua!! Kwa nini?”
“Baba ame zingua sana na amenifanya nijawe na hasira sana dhidi yake. Nina mchukia sana”
“Usifanya hivyo, mzazi na mtoto hawawezi kugombana”
“Olvia hujui ni jinsi gani ninavyo mpenda mama yangu. Yule mzee kitendo cha kumpiga mama amefika mbali sana na nilazima nita dili naye”
“Xaviela”
“Bee”
“Kwenye maisha yako ulisha wahi kupenda?”
“Ndio nina mpenda sana mama yangu na mdogo wangu kuliko kitu chochote”
“Sijamaanisha kumpenda ndugu. Maana yangu umesha wahi kumpenda mwanaume?”
“Hapana sijawahi kumpenda mwanaume yoyote na sinto kuja kumpenda yoyote”
“Xaviela nakuomba unisikilize kwa umakini.”
Olvia Hitler alizungumza huku akimtazama Xaviela kwa umakini sana.
“Nina mpenda sana baba yako na nipo tayari kuhakikisha kwamba nina mrudisha Eddy mikononi mwangu, tafadhali nina kuomba usidhubutu kumdhuru Eddy wangu kwa maana mimi leo ndio nilikuwa chumbani na baba yako. Hivyo kuwa makini dogo”
Mara baada ya Olvia Hitler kuzungumza maneno hayo akashuka kwenye gari hilo na kumuacha Xaviela kijawa na mshangao ulio mnyong’onyeza mwili mzima.
ITAENDELEA

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4