Thursday, 20 March

Ads Right Header

Buy template blogger

𝐒𝐈𝐌𝐔𝐋𝐈𝐙𝐈: 𝐍𝐈𝐓𝐀𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐄𝐏.... 36 & 37




𝐒𝐎𝐍𝐆𝐀 𝐍𝐀𝐘𝐎....

Nilimvua zile nguo zangu na kuzivaa upesi za askari kisha kuisoma tena ile ramani na kuanza kutoka mule jela huku taswira ya sura ya mwanangu ikiwa inanijia machoni mwangu..

Nilitembea kwa kujiamini kama askari na kufika hadi getini bila bughuza yeyote..

Niliwaonyesha kitambulisho na kutoka bila kujionyesha sura yangu..

Nilipanda boda hadi segera stendi ya daladala..

Niliwaza niende wapi kwa usiku ule..

Niliwaza sana ila baadae niliona temeke ndio sehemu changanyikeni sana..

Sikuona daladala usiku ule..

Nilisachi ile suruali na kukuta noti tatu za elfu 40.. niliita boda boda na kwenda hadi nyumbani kwangu.. kwa RC renatus..

nilifikishwa na kulipia elfu kumi..

Niliruka ukuta kwa nyuma ya nyumba..

niliingia kwa dirishani lakini sikumuona RC, nilichukua begi langu na kufungua droo ya hela kisha kuchukua fedha za kutosha tu..

Nilizunguka nyumba nzima bila kumuona RC...

nilikuwa nina hasira sana..

Nilifika hadi getini na kuwakuta walinzi...

kwanza walishtuka sana na kuzubaa tu baada yakuona natoka ndani kwangu wakati walisikia nimefungwa kifungo cha maisha.

Baada ya kuniona tu mmoja aliruka ukuta na kusepa sijui wapi....

Mwingine alibaki akinishangaa tu na baada ya kuona namkaribia alitoa upanga wake na kuanza kunitishia..

"hahaahah. wewe mjinga hembu tupa huko panga lako hilo..

Niliongea kwa dharau sana.. na kweli yule jamaa alitupa panga chini huku anatetemeka..

"Mwambie boss wako nimerudi.. Mwambie atauonja uchungu wa leba ili ajue thamani ya mama kwa mwanae..

yeye sialijifanya mjanja kwa kukojolea mashahawa yake na hajui chochote kuanzia mateso ya kutembea na mimba miezi tisa kisha naingia leba alafu anakuja kuua tu...

Mwambie Nimerudi..

Niliongea kwa kujiamini huku navua zile nguo za askari jela kisha kuvaa nguo zangu nyingine.

yule mlinlinzi alibaki akinishangaa tu baada yakuona nimevua nguo zote hadi kubaki na chupi na kuvaa zingine mbele yake..

Nilifunga mkanda kisha akanifungulia geti.

Nilisepa kwa hasira sana na kupanda boda hadi mbagala..

Nilishukia Mbagala Chalambe.. nilipata lodge na kuchukua chumba..

Niliingia ndani na kupumzika kwa usiku ule..

"Hajra ishi maisha yako na ufanye ulichotumwa.. mapenzi yapo na utayakuta tu mama sawa...

Niliisikia ile bezi...

Nilishtuka sana na simu yangu ikaita kwa namba za yule mkuu wetu...

" Hajra nipo pamoja na wewe.. jitahidi kutomwamini mtu sawa...

Hii kazi unaiweza wewe ndio maana tukakuamini...

Anza kumuua IRENE kwasababu anavujisha siri za kiusalama kwa wauza madawa. mbinu zetu zote wanazijua..

Nakuomba fanya kwaajili ya taifa..

Huna baba, huna mama, huna Mume, huna mtoto.. sasa kwanini usilitumikie taifa lako..??

Alionga yule mzee na kukata simu bila kusubiri majibu yeyote kutoka kwangu..

Niliingia kuoga na kurudi kitandani...

Niliangalia kipande cha ngozi kwenye begi langu na kuitafuna kisha kuimeza..

Nilianza kuhisi vibaya sana.. tumbo lilivuruga ghafla na kwenda kuharisha..

Nilisikia kuchoka na kulala chini chooni...

Niliamka asubuhi na kujikuta chooni.. Nilikuwa nimechoka sana... nilijitazama nakuona nimerudi kwenye sura yangu ya utotoni..

HAJRA.. umekuwa salama na kwenye hali yako..

Nilioga na kuvaa vizuri suruali japo baadhi zilikuwa kubwa kidogo ila nilikuwa na mkanda..

Nilienda kunywa supu na kutoka kwenda hadi kwa MR Amiri..

Nilikuwa nimewamiss sana..

Niliwakuta wamekaa wanapiga story kwasababu ilikuwa ni juma mamosi na Amiri hakwenda kazini...

***

walifurahi sana na kunipeleka sebuleni kisha wao wakaingia chumbani..

Baada ya muda amiri alitoka na kupiga story nyingi sana..

Baada ya mda mke wa amiri alitoka pia na mwanae njee.. mtoto alikuwa mkubwa sana na anatembea kabisa...

Nilikumbuka nilimwacha mjamzito..

Nilimshika yule mtoto huku tunapiga story.

Baada ya muda amiri aliomba kutoka...

Alitoka na kuniacha na mke wake...

story zilikuwa nyingi ila mke wa amiri hakunichangamkia kabisa..

Nilikaa na kusinzia kwenye kochi kwa uchovu wa kutolala vizuri usiku.. lakini kwambali nilisikia mke wa Amiri anaongea na kaka yake kwenye simu ambaye ni RC renatus..

"Kaka hajra amerudi na siulisema unataka kumuua.??

Nipo namzubaisha na story nakuomba uje na askari wengi sana....

Aliongea mke wa amiri..

Baada ya kumaliza yale maongezi alikuja na kukaa karibu kunipigisha story..

Nilimtazama yule mama kwa hasira sana na sikuamini kama ni mbea kiasi kile..

Niliinuka na kumvunja shingo bila kuongea nae..

Nilimshika mtoto na kumbusu kisha kumkalisha chini na kusepa..

Nilipanda taxs na kujiondokea zangu..

nikiwa njiani niliona gari kama sita za polisi zinaenda kwa Amir..

nilitazama tu na kuvaa earphone zangu kusikiliza mziki..

 Nilifika lodge nilipochukua chumba na kuoga baada ya hapo nilipanda kitandani na kutoa simu yangu.. nilimtumia ujume RC kwa hasira sana.

"RC renatus.. Mimi ndio usalama.. kama unayo team ya usalama wambie wakulinde.. leo lazima nikuue.

Nilituma ule ujumbe ili kumuuogopesha renatus na aende mbali kidogi ili niwezi kwenda kwenye kasino yake kumua IRANE..

Nilizima simu na kulala mchama ule...

****

Nilishtuka saa 12 jioni.. nilioga na kuvaa vizuri kisha kutoka..

nilielekea kwenye Casino ya RC iliyopo posta na kuingia...

Kulikuwa kumepoa sana kwa usiku ule...

Niliingia hadi ndani kwa sura  yangu halisi..

Nilifanya makusudi ili niweze kumjua Irene ni yupi...

Tulivyotoka urusi tulibadilishwa sura hivyo kujuana ni ngumu ila IRENE angenikumbuka kwasababu mimi nisharudishwa kwenye sura yangu ya Mwanzo yaani Hajraa kamili siyo feki...

Niliingia na kuketi kisha kuagiza kinywaji..

Wasichana walikuwa wengi sana..

Lakini kuna mmoja alikuwa akinitazama sana na kuanza kuhama viti taratibu ilimradi afike tu karibu anione vizuri..

alidhani sikumuona kumbe na mimi nilikuwa namchora tu..

Alijitahidi na kuja hadi karibu kabisa.

baada ya mda alitoka...

Nilitulia tu.. na kuendela kunywa..

Ghafla walikuja mabaunsa wawili na kunishika..

Niliwatazama na kwenda walipotaka kunipeleka japokuwa hapakuwa na baunsa yeyeto wakuniweza pale.

Niliingia kwenye hicho chumba na kumkuta yule msichana aliekuwa akiniangalia amekaa kwenyekiti..

"karibu hajraa... habari za tangu urusi.??

aliongea yule mwanamke na nikajua fika alikuwa ni IRENE...

"naona umekuja kuniua.... alizidi kuongea irene..

"Hapana irene nimekuja kukusalimia tu shostiangu.. mbona ni mda mrefu hatukuonana...

Niliongea ila kabla sijamaliza kuongea niliona kivuli cha baunsa mmoja kainua rungu lake juu na kutaka kunipiga shingo..

Niliinama na kuishika ile rungu..

Nilimpokonya na kumpiga teke la nguvu kwenye misuli ya mapaja..

wakati anaugulia nilimpiga yule mwenzie rungu la kichwa na kudondoka chini...

Niliinuka kwa hasira na kutazama mbele yangu lakini sikumuona IRENE na mlango ulikuwa wazi...

𝐍𝐈𝐓𝐀𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔

𝐄𝐏.... 37



Nilitoka njee na kuangalia kila pande kwa umakini sana..

nilikuwa nikijihami kwasababu irene pia alikuwa na mafunzo na istoshe alikuwa ni mwanajeshi kabla ya hata kwenda kwenye mafunzo kule urusi.

Nilitembea kwa kunyata na kuanza kupita kwenye chumba moja baada ya kingine...

hadi nilimaliza vyumba vyote sijamuona irene..

Nilisimama na kushusha pumzi..

Nilitoka na kuangalia getini nikaona geti lipo wazi pia..

Duuuhhhh.. Ameshakimbia mbwa huyu...

Niliongea na kuitupa chini rungu niliyoishika na kuanza kutoka nje ya geti..

"Mbona unakimbia hajraaa.???

Nilisikia sauti ikiongea nyuma yangu..

kwa hofu niligeuka nyuma na kumuona Irene kasimama mlangoni..

Nilirudi ndani kwa mwendo wa kasi sana lakini sikumuona tena..

"hajra nenda ukarudie mafunzo haupo makini..

Nilisikia tena sauti ya Irenee.

" Mafunzo ya nini mama.. Kama unataka ngumi njoo siyo unaanza kuniletea hadisi za sungura na fisi hapa..

Nilimjibu kwa hasira sana.. Nilimfuata kwenye kona aliyojificha na kumrushia ngumi..

Aliikwepa na kunishika mkono na kuuzungusha.. Nilisikia maumivu makali sana..

Nilijitahidi hadi nikanasua ule mkono alioushika..

Nilirudi nyuma nikiwa naugulia maumivu..

Nilienda tena kwa mwendo wa kasi lakini alinikwepa tena na kunipiga makofi mawili mgongoni..

Kabla sijageuka alinikanyaga teke na kunifanya nidondoke chini..

Aliniwahi na kuanza kunishambulia mangumi ya usoni...

Nilijitahidi kukwepa lakimi wapi..

Nilizidiwa kwa kila namna na kubaki nalia tu kuugulia maumivu.

Nilikuwa nimechoka sana na kuanza kutokwa na damu puani na mdomoni..

Irene alinishika shingo na kuanza kininyonga..

Nilikuwa nimezidiwa na sikuwa na jinsi.. Mwili ulishaisha nguvu kabisa na kubaki kurusha miguu tu.

"Irene unaniua mimiiiiihhhhh... Uuuuuuuhhhhhhh... Niliongea kwa shida sana lakini bado aliendelea kuninyongea chini..

"Hajra remember your promise. This is your responsibility. Please do not give up ..." ("Hajra kumbuka ahadi yako.. Hili ni jukumu lako.. Tafadhali pambana usikate tamaa..."

Nilisikia bezi la yule mzee ikiongea kwa lugha ya kiingereza..

Ghafla nilihisi kama nguvu imenijia maradufu.. Niliinua shingo kwanguvu sana na kumng'ata mkono wake hadi kumng'oa kipande cha nyama..

IRENE aliniachia kabisa na kuushika mkono wake kuzuia dam zilizokuwa zinatoka kama bomba la maji lililo toboka..

Kabla hajamaliza kuugulia nilimrukia na kumkanyaga kifuani..

Alidondoka chini kama gunia la chumvi..

Nilimshika na kumvunya shingo.. Sikutaka kutumia nguvu sana kwasababu na mimi nilikuwa nimeumia sana..

Nilitoka upesi  lakini niliogopa kulichoma lile jumba moto kwasababu kulikwa na makazi ya watu wengi jirani na baadhi ya ofisi za serikali..

Sikutaka kuua dam zingine zisizo na hatia.. Nilitaka kupambana na wahusika tu..

***

***

Kuishi hotelini kulikuwa kunanipa hasara sana na kuamua kwenda kupanga nyumba kigamboni..

Nilinunua gari jingine la kawaida tu IST na kufungua duka dogo kariakoo ilinisionekane kama mtu nisiye na kazi pale mjini..

Maisha yakikuwa ni mazuri sana kwasababu nilikuwa nina pesa nyingi sana nilizopewa na Benki ya dunia kwaajili ya kupambana na hili janga..

Nilimuajiri mtu kwaajili ya kusimamia duka langu.. Alikuwa ni kijana mdogo tu aliyehitimu chuo..

Nilimnunulia spacial ndogo pia kwaajili ya kwendea dukani..

Hakujua rasmi kazi yangu ni nini kwasababu alikuwa akiondoka na kuniacha nyumbani kila siku na akirudi jioni huwa ananikuta..

Siku hiyo akaamua kunitolea uvivu kwa kuniuliza maswali mengi sana..

"Booss kwani kazi yako ni nini.?? Maana huwa nakuona tu nyumbani..

Aliuliza Edwin au ED nilizoea kumuita hivyo..

Alivyoniuliza lile swali niliinuka na kuingia ndani kisha kumtolea vyeti vyangu..

Aliviangalia na kubaini kweli kuwa mimi ni msomi...

" Unasikia mdogoangu edy.. Mimi nilikuwa nikifanya kazi kwenye hospitali moja kubwa sana..

Na nilikuwa kwenye kitengo nyeti sana...

Nilihudumu kwa miaka kama minne hivi na baadae nikapata kazi urusi..

Kule niliingiza fedha nyingi sana na ndio maana unaona hadi sasa nimemaliza mkataba wangu kule lakini ninao uwezo wa kuishi..

Kwasasa ni hospitali nyingi sana zinanihitaji lakini nimeamua kupumzika kidogo..

Niliongea huku najitapa ili asije kuniona mtu wa kawaida. Nilitaka aendelee kuniheshimu..

Sikutaka aanze kuniletea mazoea yakijinga..

Japokuwa mimi mwenyewe kuna muda nilikuwa nikimuonaga akipita sebuleni tumbo njee na kifuachake kilichojaa nywele nilikuwa nikimfananisha sana na RC alienitoa bikira yangu..

Tulipiga story nyingi kwa siku hiyo hadi muda wa kulala na mimi nikaenda ndani kwangu..

Usiku mvua ilinyesha kubwa sana..

Joto la dar liligeuka kuwa baridi..

Nilijifunika blanket lakini haikusaidia chochote.

Hadi nilikuwa nikihisi mwili wangu unatoa mvuke..

Niliingia bafuni na kujaza maji kwenye sink na kujilaza.

Maji yalikuwa ya vuguvugu, nilikuwa nikihisi raha sana japokuwa kukaa kwenye maji kunachosha sana..

Nilirudi kitansani ila baridi ilizidi..

Hadi niliogopa..

Nilikumbuka sikuzima AC.. Kumbe baridi lote liliongezwa na AC.. Hali ya hewa ilikuwa baridi na kuongeza AC tena ndio ikawa balaa..

Baada ya kuzima AC hali ya hewa ndani ikawa nzuri..

Nilikaa sana bila usingizi ila hisia pia zilizidi kunisumbua kwasababu ilishapita karibu miezi miwili nipo tu nyumbani bila kukutana na mtu..

"au niende kwa Edy...??? Nilikuaa nikijiuliza maswali huku nainuka kitandani nilipolala na kufunga mtandio.. Nilisogea hadi mlangoni na kuwaza sana nini chakufanya...

" lakini ataniona mpumbavu sana.. Yaani boss kama mimi nianze kumtamani tena huyu mtoto..

Nilikuwa nikiongea mwenyewe huku taratibu nafungua kitasa cha mlango..

Nilitembea hadi karibu na mlango wa eddy nikiwa natetemeka sana...

ITAENDELEA..


Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4