Siku ya chai ya fikra
Siku ya chai ya fikra,weka chai yako nzuri nzito ya maziwa km hubby wako anapenda chai ya maziwa.
Km hapendi chai ya maziwa mpikie ile chai anayoipenda.
Muhimu iwe kidogo vikombe viwili tu.
Iwe nzuri iliyopikwa ikapikika,
Viungo vibalance vizuri kiasi isijulikane viungo gani na gani vilivyotiwa.
Kama mumeo hapendi chai muandalie juice nzuri ya mchanganyiko wa matunda anayoipenda.
Kisha andaa kitafunwa chako kimoja tu kizuri.
Yaweza kuwa sambusa,catles,kachori,kabab,bagia,cake nk
Kisha chukua tray maalum ambayo haitumiki siku zote
Weka kithermos chako kidogo,kisahani kizuri weka vitafunwa vyako
Weka vikombe vyako viwili.
Kisha iweke juu ya kitanda kilichotandikwa vizuri, kisha ifunike na upande mmoja wa kanga zile ulizozivundika.
Kujipamba na kujipodoa
Wewe mwenyewe unatakiwa uoge vizuri kwa maji yenye kunukia na sabuni ya oud.
Kisha ujipake lotion ya usiku alfitna ujitie manukato kila sehemu.
Valia nguo yako nzuri ya kumpokelea bwana.
Vaa hereni,cheni,bangili kikuku cha mguu na shanga hususan ukiipata ile iloandikwa *YOTE YAKO*
Kisha kaa kwenye dressing table ujipambe vizuri.
Kisha ukae tayari kumpokea laaziz.
Huku chumba chako ukiwa umekifagia vizuri na kukitandika shuka zuri.
Umekideki na oud wa kudekia.
Umekifukiza vizuri shurti kinavutia na kunukia.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment