STORY: PENZI GUMU EPISODE 04
Asubuhi nilivo amka zikko hakuwepo alikua tayari kesha ondoka na sio kawaida yake huwa tunaondoka pamoja na mara chache mimi ndo huwa nawahi na nikitoka lazima nimuage kwamba mie ndo naondoka..
Basi nikajiandaa nikaondoka zangu kwenda kazin..
Mchumba wangu anaitwa Kelvin..alinambia kwamba anataka kujua nnapo kaa lakin hakujua kama naishi na mtu nilikubali bila tatizo kwa mawazo yangu kwamba akisha fika nyumbani ndo namuelezea mazingira ya pale kwangu kwamba naishije na nna ishi na nani hilo ndo lilikua akilini mwangu sikujua kama mwenzangu nae ana mipango yake mingine kichwani..
Basi kweli alivotoka kazin kwake alikuja mpaka kazin kwangu na kunichukua kwakweli sijui mpenz wangu anafanya kazi gani kabisa ila alinambia tu ni mfanya biashara na biashara zake anafanya kati ya China na Tanzania sikutaka kuuliza sana nikijisemea mwenyewe nitamjua zaidi huko mbele kwa mbele basi nilimtumia Zikko msg kwamba "wahi kurudi nyumbani leo kutakuwa na mgeni" akasema "Sawa" basi tukaenda mpka nyumbani huku njian tukipiga story za hapa na pale akasema "Unakaa uswahili mammy" nikawambia "Ndo mazingira yangu babe" akasema "Fanya mpango uhamie sehemu za hadhi yako mm nitagharamia kila kitu we tafuta tu chumba maeneo mazuri kidogo wangu sawa?" Nikamwambia "Tafikiria maana huku mie nimekuzoea" akasema "Swala si kupazoea mimi sijapapenda huku macho mengi sana" nikamwambia "Mmgh macho mengi hata hatujafika my?" Akasema "Uswahilini ni uswahilini tu" nikanyamaza baada ya muda kidogo tu tukawa tumefika..
Nikafungua mlango zikko alikua hajafika kisha nikamribisha ndani nikamwambia "karibu ndani" akanifata nyuma gari tuliliacha mbali kidogo maana njia ya chocho kwangu gari halipiti hivyo tulilazimika kutembea kidogo.. Nikamwambia "Hapa ndo kwangu nimepanga chumba kimoja" akasema "Chumba kidogo ila kiko na mpangilio mzuri kama wewe" sasa ndo nataka kumwambia kuwa kuna mtu naishi nae na kumweleza juu ya uhusiano ulipo kati yetu akawa amenishika kiuno na kuanza kunipa denda nikamwambia "Mmgh hata hatuja kaa chini tukazungumza kidogo?" Akasema "Badae tutaongea" kisha akaendelea na shughuli yake aliyo kuwa anafanya nikashindwa kukataa maana mtu mwenyewe anaonyesha ana hasira ni mwepesi wa kuchukia. Ila moyoni mwangu nawaza hivi zikko akija hapa jamani ataona picha gani? Atajiskiaje?
Basi mchumba wangu Kelvin aliendelea kunikiss ila sikuwa na amani moyoni nawaza tu akija zikko muda ule tena ukizingatia kaninunia si ndo ataona kma namfanyia kusudi kabisa? Ila sikuwa na namna Kelvin alikua ananikiss huku ananisogeza mpka tukafika kitandani na kuangukia pale yeye akiwa juu mimi nipo chini nikamsukuma kifuan kdg akauliza "nakuumiza?" Nikamwambia "Tuongee kwanza mpenz usiwe na haraka" kabla hajajibu mlango ukafunguliwa tukiwa katika hali ile ya mahaba..
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment