STORY: PENZI GUMU EPISODE 05
Nilishtuka sana kuona mlango umefunguliwa na nilimsukuma kelvin na kukaa vizuri pale kitandani kelvin alisimama na kuangalia alie ingia ni nani. Alikuwa ni zikko alikua amebeba mfuko wa matunda ila alipigwa na butwaa kwa kile alicho kiona pale kitandani nilishindwa jinsi ya ku react nikajifanya tu natengeneza nywele. Zikko aliingia akaweka ule mfuko juu ya meza kisha akasema "Samahani kwa usumbufu na kuondoka" yani wakati anasema maneno hayo macho yake yanaonyesha kbs kuchukia sijui nisema kuchukia au kuumia sijui namna ya kuelezea hapo.
Wakati anatoka mimi nilinyanyuka ili nimfate ila Kelvin alinivuta mkono na kuniuliza "Huyo nani?" Nikamwambia "Babe subiri nakuja" nikawa natoa mkono wake ili nimfate zikko kwa haraka akanivuta tena kwa nguvu na kunikalisha kitandani kwa hasira akaniulza "Una akili wewe?" Nikamwambia "Una maana gani?" Akasema "Yani uniache mimi hapa umfate mwanaume nje?" Nikamwambia "Hapana huyo si mwanaume" yani mm nlitaka kumaanisha si mwanaume kama wangu kama anavyo dhani ila sikuweza kuweka kauli yangu vizuri akaniuliza "Kumbe yule ni mwanamke au shoga yule eeh?" Nikamwambia "Kelvy hivi mbona una panic vitu vya kipumbavu? Nlitaka tuongee ulinipa nafasi ya kuongea?" Kelvin alinipiga kibao ambacho nilihisi naona na nyota nyota kibao kili niingia na kiliuma haswa nikawa nimeshika tu shavu akasema"Wewe ni mwanamke kwaiyo angalia majibu gani unanijibu sawa?" Nilikaa kimya kuskializia maumivu ya lile kofi wallah liliuma usiombe upigwe kofi ukiwa katikati ya mazungumzo kibao ambacho hujakiona kina kuja yani kile cha kushtukizaa dah unaweza hisi mdomo umekufa ganzi.
Nilitoka alama za vidole na sikumjibu chochote kelvin aliamua kuondoka wakati anatoka akapita karibu na kabati alafu akaifungua akakuta nguo zangu humo na nguo zingine za kiume mashati suruali tishet pensi akanigeukia kisha akaondoka bila kusema chochote mimi nilibaki nimekaa pale kitandani tu huku nna hasira sana pia nawaza zikko kaenda wapi kwakua ilikua ni mapema niliona bora tu nitoke niende dukani nikiongea na wateja wawili watatu hasira zitaisha.
Nikatoka kuelekea dukani.. Nilipofika dukani nikakuta duka limefunguliwa na zikko anafanya kazi kama kawaida tena akiwa anatabasamu kama kawaida nilikua namwangalia sana mpaka nikafika alivyo niona alinichangamkia tu tofauti ambavyo na mimi nilitegemea maana nlijua atakua kanuna au kunichukia kabisa lakin alikua na furaha zake kawaida tu. Nikaingia dukani nikimsemesha kitu anajibu vizuri yani hakuna tofauti yoyote nikamwambia kaa upumzike akija mteja mimi tamhudumia basi akaja mteja ile nageuka kumhudumia mteja zikko akaona ile alama shavuni kwangu mteja alipo ondoka akaniuliza "Umefanyaje hapo shavuni?" Nikamwambia "Mwenzangu we acha tu" akasema "Umefanyaje?" Nikamwambia "Si nimepigwa kofi na kelvy sijui anahisi we ni mtu wangu kha yule mwanaume si kwa hasira zile ana hasira kama kanitolea mahali.." zikko akasema "Yani kakupiga kwa mkono wake?" Nikamwambia "Ndio" akasema kwa hasira "Ndo mana nakwambia uachane na hayo mambo huskii" nikamwambia "Ahh sa na we mbona una panic tena" Ghafla simu yangu ikaita..
Kuangalia ni Kelvin anapiga nikasema "Ndo anapiga hapa" nikapokea akasema "Uko wapi?" Nikamuuliza "Kwani we umeniacha wapi?" Akasema "Nlipo kuacha kuna kufuri" nikamwambia "Nipo dukani" akasema "Fasta nakusubiri" alafu aka kata simu nikanyanyuka nikamwambia zikko "Wenzang muda ukifika utafunga mie kanipigia cm eti ana nisubiri nyumbani" zikko hakunijibu mimi nikafunga nikatoka kuelekea nyumbani maana si mbali sana.
Kufika nyumbani namkuta kweli kelvy amesimama mlangoni ananisubiri tena mnavo jua nguo zetu za uswazi kuna watu kibao mie tena yule mdogo mdogo naenda. Sa nikahisi kama nyuma yangu kuna mtu tena kama anakuja kwa kasi ile nageuka si ndo zikko huyu hapa spidi anayo kuja nayo ndugu yangu sio ya kawaida yali kama kuna kitu muhimu ana wahi sana nikiwa nataharuki jamani nlishangaa snaa kwa kilichotokea maana ni kitendo ambacho sikukitegemea..
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment