Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

STORY: PENZI GUMU EPISODE 06


Top 7 African songs to woo your love this Valentine - Face2Face AfricaZikko alinipita kwa kasi ya ajabu sana na moja kwa moja mpaka pale alipo kuwa amesimama kelvy maana kelvy alikua amesimama mlangoni. Zikko bila kuuliza alifika na kumtandika kelvy ngumi moja ya uso kitendo ambacho hakuna alie tegemea. Kelvy alikosa balance na kuanguka chini. Zikko akabaki amesimama nlisogea mpaka pale na kumshika zikko "Vipi mbona unampiga mgeni wangu" watu wakawa wamekusanyika pale si unajua tena nyumba zetu za uswahilini kelvy alivo inuka aliniangalia na kuniuliza "Huyu nani?" Nikamwambia "anaitwa zikko" akasema "sijauliza jina huyu nani kwako?" Kabla sijajibu Zikko alimkunja na kumwambia "We nani mpaka uulize maswali? Kwanini ulimpiga? Umepata wapi mamlaka ya kumpiga?" Kelvy akamtoa mikono akasema "Ni mwanamke wangu kwaiyo sina mamlaka nae?"  Zikkoa akanyanyua mkono kesha kunja ngumi tayari ampige tena nikamwambia "Zikko kwanini?" Zikko akamsukuma kisha akapita kuingia ndani maana funguo ingine ya ndani anayo.

Huku walimwengu sasa ndo wamepewa mada ya kuongelea mala wanagombania mwanamke..Wengine oh nimefumaniwa yani kila mtu anaongea lake. Kelvy aliniangalia tu na kuamua kuondoka bila kusema kilicho mrudisha mimi ikabidi niingie ndani maana zikko kwakweli nilishindwa kumuelewa hasira alizo kuwa nazo. Nilimkuta amesimama kwenye friji anakunywa maji nikamuuliza "Vipi zikko mbona una hasira sana?" Akasema "Hajakutolea mahari wala barua kwanini akupige? Hata angekua amekuoa mamlaka ya kukupiga yeye hana..Akipige kama nani na kwanini?"
Nikamwambia "Sawa amekosea pengine labda ndo mana alirudi baada ya kujua kosa lake kwanini sasa wewe umpige tena mbele za watu zikko hivi unapenda watu wanavo ongea ongea?" Zikko akaweka glasi ya maji juu ya friji na kunigeukia akaniangalia kwa macho ya kutisha kidogo akasema "Asia kwanini unapenda kuishi kwa kuangalia watu? Kabla ya leo hawajawahi kukusema? Kuna kitu utachofanya waache kusema hata usipo fanya chochote wata tafuta tu cha kusema ni hivi sitaangalia mtu yoyote akikuonea" nilikosa cha kusema nikaenda kukaa kitandani na kuchukua simu ili nimtafute kelvy nilimtumia msg "Naomba tuongee" akajibu "Sema" nikamwambia "Samahani kwa kilicho tokea leo" akasema "Okay"  lakini bado moyo wangu haukuwa na amani sikujua nitaelezea vipi mahusiano yaliyopo kati yangu na zikko ili aelewe ila nilipata wazo la kumpangia zikko chumba kingine maana sikutaka aone kama namfukuza.

Nilitafta chumba na kuanza kununua vitu vya muhimu na hatimae nikamwambia Zikko na hakuwa na shida tena alifurahi.. Zikko alihamia kwake na mimi sasa nikawa huru kazi zetu ziliendelea kama kawaida chumba cha zikko hakiko mbali sana na kwangu kwaiyo hata chakula nlikua napika tunakula pamoja mie siku zote sikuwa najua kilichopo akilini mwa zikko wala kelvy.

Siku moja kelvy alinitoa out ilikua ni katikati ya wiki sikuwa na mood kabisa ya kunywa pombe lakini kelvy alinibembeleza sana nimpe kampani na hataki kunywa peke ake basi nikasema nitaonja tu weeh kuonja ndo kuonja si ndo nikajikuta nanogewa nikanywa mpaka nikajikuta nimelewa tena nimejiachia kabisa si niko na baby bwana.. Nika banwa mkojo nikamwambia kelvy "naenda choon" nikabeba mkoba wangu kwa ajili ya kutoa toilet paper sikuona kama ni Sawa kutoa pale na kutembea nayo mpaka chooni..tena choo chenyewe kipo pembeni kidogo na pale tulipo kuwa tumekaa basi hakua na shida nikaenda chooni. Nikiwa chooni nimeshajisaidia nimemaliza nikaskia mdada mmoja anaongea kwenye simu "Wewe yule Kelvin uliomsemea si ni mrefu mrefu hivi mweusi?... eh eh ana pua ndefu hivi.. Kha basi ndo nimemuona hapa weeh yani nimeshtuka sana.. Sijui yuko na nani leo Mungu wangu hapa miguu yote ina tetemeka..Shogaaa yani naongea nipo chooni nikitoka tu hapa nduki yani sjui leo nna mkosi gani"

Mmgh yale maneno yalinishtua maana huyo mtu anae mzungumzia mbona kama ndo kelvy wangu Mungu wangu??



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4