STORY: PENZI GUMU EPISODE 07
Nilitoka chooni ila moyoni nilikua naogopa sana yule dada alikua na maana gani? Basi nikarudi nikakuta kelvy kamaliza kuongea na simu akasema "Si tunaondoka wote leo" nikasema "Hapana labda next time" akasema "Aah amna bhana it must be today" mmh hapo nikaanza kujiuliza kunani taa nyekundu inawaka lakini Sijui ni pombe nilishindwa kubishana nikamwambia "Okay"
Tulikaa pale kwa muda mchache kisha akasema tuondoke lakini muda wote alikua busy sana na simu kitu ambacho kilinipa wasiwasi nikammuuliza "tunaenda wapi?" Akasema "Utapajua tukifika" kwakweli niliogopa mno.. nikijumlisha na yale maneno ya yule dada kule chooni naona hapa mbona kama sielewei
Tukiwa njiani alianza kuniuliza kuhusu Zikko na nilimuelezea uhusiano uliopo kati yetu aliniuliza "Je hivo unavo fikiria ndivo naye anafikiria?" Nikasema "Ndio" akasema "Sidhani yule anaonekana ana mawazo tofauti" mimi nikawa nacheka tu ila kiuoga siunajua pombe tena..
Njia nzima alikua akimuongelea zikko anamchukia hapendi ukaribu uliopo kati yetu basi nikamwambia "nikipata mtu mpya tamuweka" akasema sawa kinachonitia hofu kufika hatufiki yaani safari ni ndefu tumesha acha balabala ya rami naona kama tunaenda porini wakati huo wote tupo kimya mimi nikajifanya pombe zimenizidi nimelala..
Simu yake ikaita akawa anaongea na simu mimi najifanya nimesinzia tena na ku koroma nakoroma..ila hapo moyoni nna hofu ya hatari. "Hallo.. sasa sie ndo tupo njiani vipi kuna mpya? Anhaa kama anasumbua si umchome ile dawa? Ah haha hamna amesinzia usiwaze.. hahaha haiwezekani bwana nakuja mko wa ngapi? Aya poa poa" maongezi yakawa yameishia hapo sikuweza kumskia wa upande mwingine ila haya nilio yaskia yalizidi kunitisha na niliogopa zaidi nikajisemea moyoni ukiskia kufa ndo huku yani leo nakifata kifo Asia mimi jamani sikua na namna zaidi ya kuanza kumuomba Mungu kimya kimya piga kila dua nnayo ijua mimi
Nikajigeuza najifanya usingizi umekolea hapo nafikiria cha kufanya na sijui bado umbali kiasi gani tufike loooh..
Sijui ilikuaje nikamwamini mwanaume ambaye sijui hata anafanya kazi gani jamani.. 😪
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment