Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

STORY: PENZI GUMU EPISODE 08


Top 7 African songs to woo your love this Valentine - Face2Face Africa
Yani nawaza nifanyeje ili hili janga liniepuke kila nikiwaza sipati jibu nawaza nijitapishe labda atanishusha nitapikie nje nashindwa niseme nimebanwa mkojo nikimbie nashindwa ghafla simu yake iliita akawa ameweka loudspeaker maana si anajua mimi nimelala nikaskia "Oyaa kaka huku jau kimeshanuka polisi wamesanuka mwanangu" Akakata simu fasta na kugeuza gari..akaendesha kwa mwendo wa kasi sana mpaka tukafika mjini hapo mimi naangalia kijicho cha chini chini nikaskia ananiita "Asia..Asia" nikaitika "Mmmgh" akasema "amka" nika kaa vizuri akasema "I'm sorry baby sitaweza kukupeleka nyumbani nna dharula kidogo si unaweza kwenda tuu kwa leo?" Nikajifanya kma nasikitika " Aah baby mimi nikajua tunaenda hata hotel jamani" akasema kwa utani " Agh ww mwanamke pombe zimeshuka chini nini" nikacheka tu nikamwambia "aya  sawa mimi wacha niondoke kesho kazini ujue "akasema "sawa"

Yaani nilivo shuka kwenye gari nilushusha pumzi kama nimetoka kukimbizwa vile hapo ishakua usiku mida ya saa 6 yani muda umeenda sana ikabidi nitafute usafili wakwenda nyumbani basi nikaamua kuchukua boda boda mpaka nyumbani kufika nakuta zikko yupo kwangu amekaa nje na nimelewa chakali kulewa nimelewa ila akili zimo yani najielewa najua hiki nini hiki nini kuniona tu akauliza "Asia vipi mbona umechelewa sana na simu yako hupokei?" Nikacheka tu akasema "unacheka? Ujue nilikua na wasiwasi sana nikahisi umekumbwa na kitu kibaya" nikamwambia "acha tu ndugu yangu sijui ningechunwa ngozi leo" akasema "Kwanini hebu fungua kwanza mlango tukaongelee ndani usiku sana saivi" nikatoa funguo nikampa amefungua mlango kuingia tu ndani nika anza kutapika nimetapika mpaka naskia nguvu zina niisha kabisa nimemaliza kutapika zikko akanitoa nje akanipa maji akasema "sukutua kwanza"  nikasukutua akasema "subiri nikuwekee maji ukaoge" akanipelekea maji bafuni mimi pale ndo naona kama network zina anza kupotea yaani naona ukungu ukungu tu zikko akaja akanambia "Maji yako tayari amka ukaoge ulale" ile nanyanyuka nahisi miguu haina nguvu mikono haiwez kushika popote nguvu zikaniisha nikaanguka chini..

Kutokea hapo sasa sikujua tena kilicho endelea nakuja kushtuka ni mchana sijui sangapi ila kwa kuangalia jua kupitia dirisha la chumbani nadhani ni sa saba au nane labda.. kichwa kinauma mwili umechoka na unauma vibaya sana mala naskia harufu ya dagaa kma mtu anapika dagaa ndo akili inakaa sawa "Mungu wangu leo ni jumatano mbona nipo kitandani muda huu kazini tasemaje mimi? Nakurupuka niamke nasimama miguu haina nguvu napepesuka tu..

Ndio namskia zikko anasema "hizo pombe zako hizo utaja fanywa vibaya" namuuliza " Umeingiaje ndani?" Akasema "Duh kweli we hata ngozi unachunwa" nikamwambia "kwanini?" Na simu yangu inaita akasema "umepigiwa mala 7 ya 8 nikaona nipokee mimi" nikamuuliza "nani alipiga?" Akasema "ameseviwa sugar in my tea" nikasema "Aah kelvy" akasema "utajua wewe" nilivo sema vile tu si ndo nikakumbuka matukio yote ya jana nilijikuta naanza tena kumuogopa kelvy..



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4