STORY: PENZI GUMU EPISODE 09
Ila nikajipa moyo nikasema wacha nipokee tu nikapokea akasema "Halloo" nikaitikia "hello" akasema "Kwanini unafanya mambo ya ajabu?" Nikamuuliza "mambo gani?" Akasema "Nakupigia simu hupokei anakuja kupokea mwanaume ananambia umelala kweli?" Nikamwambia "Kelvy" akasema "Unasemaje?" Nikamwambia "Naomba tuachane" sikusema vile kwa sababu simpendi au kwasababu ananifikiria vibaya hapana nlisema vile kwasababu namuogopa yani nlimuogopa hata angesema twende wapi siwezi enda nae pahala sijui hata kazi anayo fanya wala nini tumekutana tu tukapendana basi aiseeh namuogopa baada ya kuongea vile nliona zikko kanigeukia kana kwamba haamini anacho kiskia kelvy aliuliza "Unasemaje?" Nikamwambia "naomba tuachane" akasema "Huyo jamaa ndo anakutia jeuri sio? Poa mwamba yeye" kelvy akakata simu..
Zikko akasema "chakula tayari nenda ukaoge upige mswaki uje kula mimi narudi dukani.." Nikamwambia "Naomba usiende naogopa kukaa peke yangu" akasema "kwanini?" Nikamwambia "Sijui ila nahisi kama kitu kibaya kitatokea" akasema "sawa" nikaenda kuoga na kupiga mswaki nikavaa kwasababu chumba ni kimoja basi zikko akiwepo huwa navalia bafuni kabisa. Nilivo maliza nikatoka zikko alikua amepika ugali na dagaa nika kaa tukawa tunakula ila moyoni mwangu sina amani kabisa najiuliza kelvy ni mtu wa aina gani na jana alikusudia kufanya nini? Ila majibu nakosa zikko akanambia "mbona kama una mawazo asia?" Nikamwambia "kweli yani akili yangu tu haiko sawa" akauliza "kwanini?" Nikamwambia "yan nna vitu vingi vinazunguka kichwani kwangu ambavyo sina majibu" akasema "kama vitu gani" nikamwambia "yani unajua sijui kelvy ananfanya kazi gani wala anaishi wapi yani sijui chochote kuhusu yeye" akasema "mna mda gani kwenye mahusiano nikamwambia huu ni mwezi wa tano" akasema "Duh mwezi wa tano hujui hata anaishi wapi wala kazi?" Nikamwambia "ndio" akasema "umewahi kukutana nae kimwili?" Nikamwambia "hapana maana wote tuko busy sana na hatuna haraka" akasema "kwanini umemwambia muachane?" Nikamwambia "namuogopa sana tangu jana" akasema "nini kilitokea?" Ikabadi nimuhadithie ukweli wote wa matukio ya jana akasema "Mgh huyo sio mtu mzuri kaa nae mbali" nikasema "sawa"
Tumemaliza kula nikarudi kitandani kulala maana nlikua bado siko sawa najiuliza ni pombe tu ile au kuna kingine nika anza kupata mashaka labda kuna kitu alinichanganyia nikamwambia zikko "naomba unisindikize hospital" akasema "sawa" tukaenda mpka hospital nikaelezea jinsi nnavo jiskia na nikachukuliwa vipimo badae majibu yanakuja daktari ananiuliza "huwa upati usingizi unapotaka kulala?" Nikamwambia "kwanini mbona huwa nalala vizuri tu?" Akasema "Vipimo vinaonesha ume ji over dose" nikamwambia " Dactari mimi siumwi wala situmii dawa nimeji over dose kivipi?" Akasema "umezidisha kipimo cha dawa za usingizi binti ndo mana mwili wako upo katika hali iyo nikwambie tu hii ni hatari sana inaweza kukufanya ukapoteza maisha kabisa" niliogopa sana kuskia vile ila kwa kumbu kumbu zangu sijawahi kutumia dawa za usingizi na jana nlikunywa pombe tu.. akasema pia "Hizo dawa ulizotumia huanza kufanya kazi kwanzia lisaa limoja baada ya kutumia" hapo ndo akili ikanijia kwamba inawezekana nilivo enda chooni kelvy alitia kitu kwenye kinywaji changu. Nilijiskia nguvu zinaniisha kabisa wakati huo zikko alikuwa nje ananisubiri nilitoka pale kinyonge sana.
Dactari alishauri ninywe maji mengi na nitumie glucose kwa ajili ya kupata nguvu niliwaza sana kelvy alikua na lengo gani? Kwanini anitilie dawa za usingizi? Wale alikua anaongea nao ni kina nani? Huwa anafanya shughuli gani? Dah maskin asia mimi nimejiingiza kwenye balaa gani tena hili?
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment