STORY: PENZI GUMU EPISODE 10
Zikko aliniuliza tatizo ni nini nilimueleza kila kitu bila kumficha akasema "Asia huyo anaonekana ni mtu hatari pengine hata jambazi" nikasema" Sawa" ila moyoni mwangu nlikua na wazo lingine maana kelvy nilisha anza kumuona katika hali ya tofauti kabisa tulirudi nyumbani sasa ilikua jioni nikamwambia zikko aende akafungue labda atapata hata wateja wawili watatu wa jioni jioni akawa ameondoka mimi lengo langu niende polisi nikachukue hata rb litakalo tokea niwe nimejisogeza kidogo kwenye sheria nikaenda nikaelezea wakawa wamenielewa na nikapewa rb kwamba huyo bwana akikufanyia chochote toa taarifa mapema.
Nikarudi nyumbani wakati narudi nimefika maeneo ya nyumbani nikaona gari ya ya kelvy imepaki moyo ulipasuka ghafla nikawaza Mungu wangu huyu mtu anataka nini na nimesha mwambia tuachane? Nikabadilisha njia nikaenda dukani zikko akaniuliza "Mbona umekuja huku si ulisema unataka kupumzika?" Nikamwambia "Ah nmejaribu kulala usingizi sina" akasema "Aya sawa" tumekaa sana pale dukani badae usiku tukafunga mida ya sa nne tukaenda kwenye kibanda cha chips tununue chips tule kila mtu aka lale kwa wakati huo kila mtu ana kaa peke yake.. basi tumemaliza kula tukaondoka tukafika njia panda ambayo kila mtu anashika njia yake tukawa tumeagana ila sio mbali mbali yani.
Kufika nyumbani nikakumbuka nimesahau funguo ya nyumbani kule dukani na funguo ya dukani anayo zikko kwaiyo ikabidi nirudi kwa zikko kufika kwa Zikko nikakuta mbona kama kuna watu wengine nje mgh kunani mimi nikasimama kidogo niangalie naona zikko nae anafungua mlango ile anatokeza tu watu wakazama ndani hee mimi nataharuki ila wazo likaja tu yani kama Mungu piga simu polisi napiga kabla sijaongea nikaskia kitu kizito kama chuma kimetua usoni nikashindwa kujishkilia simu kule mimi kule nikavurutwa mpka sehemu ya wazi Kisha nikabebwa na kuamini kama naingizwa kwenye gari maana hisia ndo zilikua zinanituma hivo hapo nimefumba macho naugulia maumivu yani nahisi kama navuja damu kuskia naskia ile zzzz kama kuna mdudu maskioni.
Baada ya dakika kadhaa naskia mwili wa mtu mwingine umeingizwa kwenye gari naskia harufu ya zikko kabisa unajua mtu ukikaa naye karibu kwa muda anakuja unajua hata harufu yake basi nikaona nifumbue macho tobaaaaaa yani nafumba macho zikko huyu naye kaingizwa siti ya nyuma majamaa wamewasha taa ndani ya gari alafu mmoja ambae ndo alika dereva alikua anaongea na simu mwingine kakaa siti ya mbele na huku nyumba nipo mimi pamoja na zikko na majamaa wengine wawili walio kaa kulia na kushoto namuona zikko uso umevimba yani hatamaniki kafungwa mikono na miguu yani hatamaniki mimi sijafungwa kokote ila damu zinanitiririka kwenye paji la uso nikauliza "Nyie ni kina nani?" Yule alokua anaongea na simu akasema "Tulia malaya we na twende kwa amani" yule wa nyuma aliekaa pembeni yangu akasema " Agh usimuite hivo huyu ni malkia bwana" gari lika anza kuondoka kwa kasi ya ajabu najitahidi kupiga kelele "Msaada.. tunakufaaaa" nlipigwa Kofi moja nikahisi kama nimechomwa sindano ya ganzi zikko akawa anafurukura huku anatukana yule mtu alie kaa karibu nae alimkaba shingo na kuanza kumtukana gari iko mafuta mbaya mbovu tusijue tunapelekwa wapi jamani.
Hofu imejaa ninaogopa kiasi cha mwisho naogopa mno nawaza hili balaa mbona zito sana..
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment