STORY: PENZI GUMU EPISODE 11
Gari lilikimbia umbali mrefu nilikua naogopa kwa mawili kwanza ni ile kasi mpk nawaza yani hapa gari linapinduka muda wowote.. Pili nawaza gari likisimama linasimama wapi jamani? Baadae hatimae gari lilifika na tukashushwa tulikua mbele ya jengo moja zuri sana kwa nje na inaonyesha ni kama eneo la biashara labda tukapelekwa mpka nyuma ya lile jengo kulikuwa na kimfuniko kma cha sink kikafunguliwa kisha nikaingizwa mimi akaingizwa zikko na wao wakafata kulikua na ngazi tukafata ngazi mpka zilipo tuongoza mwisho hamadi kelvy huyu hapa..
Daaah woga ukanizidi na moyoni nilijilaumu sana kumwamini mtu haraka haraka aiseeh akasema "Oh noo kwanini mmewaumiza wageni wangu jamani?" Mmoja akasema "walikua wanaleta ubishi" kelvy akasema "niliwaagiza mumlete huyu mwamba imekuaje mmemleta na malkia wangu?" Akasema "Alikuepo eneo la tukio" kelvy akanisogelea huku ananipapasa usoni "My queen umejiingiza matatizoni mwenyewe look how beautiful you look right now hahahahaha" nikamtoa mkono maana mimi nlikua sijafungwa chochote zikko akasema "Toa hiyo mikono yako michafu" kelvy akacheka akamsogelea akamwambia "unajua uko sehemu gani? Yani hapa hata ukipewa kipaza sauti upige kelele hakuna atakaye kuskia" akacheka sana zikko akamwambia "tuachane tuondoke" kelvy akamfata tena akamwambia huku anajikuna kichwani kwa dharau "Skia wewe hunipi mimi oda mimi ndo naamua cha kufanya panzi wewe" akamtia kofi la uso..
Nikamwambia kelvy "tatizo ni nini mpaka unatufanyia hivi?" Akasema "Moyo mama moyo" nikamwambia "Niko chini ya miguu yako kelvy tuache tuondoke nitafanya chochote unachotaka" akanifata akanishika kidevu akasema "Oh pole ubaya ni kwamba ukisha ingia hapa huwezi toka ukiwa hai na ubaya ni kwamba wamekuleta bila kukuziba macho kwaiyo unajua kila kitu there's no way you'll get out of here alive" Daah nguvu ziliniisha kelvy alimfata zikko akamfungua mikono na miguu akachukua mjeredi aka anza kumchapa nao yani akichapa anamchana alafu ye kelvy anachekelea sanaaa huku akinambia "njoo njoo umsaidie bwana ako njoo" mimi ni kilio tuu nnalia mno akamaliza akamsimamisha akampa ngumi ya uzito akamwambia "hii ni ngumi yako nimekulipa" akampiga ngumi ingine akasema "Hii ni ya kwangu nimekupa na hizi ni nyongeza" alimshindilia ngumi na mateke jamani mpka nikaona zikko anakufa nikashika kelvy mguu huku nalia namuomba amsamehe akasema "chagua mmoja kati yetu" nikamwambia "ni wewe kelvy" akanipiga teke la uso akasema "Kwanini unaniongopea na wakati najua una niongopea?" Akanivuta akanikaba shingo akasema "leo ndo mwisho wenu nyie si mnapendana sana sasa mtakufa pamoja ki mahaba kabisa" nikaona dah hapa hatuna msaada tena basi nikawa nasubiri tu yule kelvy afanye anachotaka..
Akamwambia zikko "mtu mwenyewe huna maisha una lelewa na mwanamke alafu unajifanya una mapenz ya dhati.. mapenzi ya dhati unayajua wewe? Na wewe unajifanya una sura nzuri eeh leo takufurahisha na hiyo sura yako taizidisha uzuri" wakatoka nje mie na zikko tukabaki mle ndani kila nikimuangalia zikko naona kama mimi ndo nimemuingiza kwenye lile balaa nimebaki tu kuomba samahani.. Anasema "Hapana Asia usifikirie hivo" basi nikajisogeza karibu yake na kumkumbatia zikko huku nikiwa nalia maana kiukweli sikuwa najua tena cha kufanya.. ilisha kuwa usiku sijui hata ni saa ngapi na usingizi ulitupitia tukawa tumelala.. badae najigeuza nakuta nimelala miguuni mwa zikko nikamuuliza "Hee ilikuaje we hujalala mie nimelala miguuni kwako?" Akasema "Nliona unapata tabu sana ndo mana usijali hata ivo usingizi sina lala tuu" nikabaki namwangalia tuu usema ukweli natamani nimkiss au nimwambie neno lakini naona sio mahala sahihi nikiwa bado nimelala miguuni pake huku namwangalia bila kusema chochote zikko ali inama pale na kunikiss mdomoni.. niliskia kama mwili wote umepigwa shoti yani nilisisimka hatari najua kabisa sitakiwi kuwa hivi lakini siwezi kujizuia weeeh je ndo nikifa leo yani itakuaje kama ndo kelvy anakuja kutuua yani nife nalo rohoni?
Niliamka nikamshika zikko mashavu nikamsogeza karibu kisha nika anza kumkiss sasa ile deeep kiss wanaita denda eeeh?..
Akha mwenzangu kama nna kufa nife tu ila na mimi nimetoa la rohoni bwana weeeh..
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment