STORY: PENZI GUMU EPISODE 13
Basi wakati kelvy ndo anajaribu kunivua nguo ghafla mle ndani kukawa na hewa nzito tena inazidi kwa kasi kama kuna kitu kinaungua ghafla tukaskia mlipuko kama bomu boooooom kitendo kilichofanya kila mmoja ashituke kelvy akatoka na vijana wake kwenda kuangalia ile wametoka kwa kasi na zikko akanikokota ili tukimbie mimi miguu hata nguvu haina ananivuta tu tulijitahidi kukimbia mpaka kutoka pale maana kila mtu alikua anataka kujua nini kimetokea sisi hatukutaka kujua A wala B tulichotaka kujua kwa wakati huo ni usalama wa maisha yetu.
Tulivofanikiwa kutoka nje tukaenda upande tofauti na wao waliko elekea zikko ananivuta kama kiroba mweeh ghafla tunakutana na njemba inakuja upande wetu bila kabla sijakaa sawa zikko aliniachia mkono akaokota bonge la jiwe akalivugumisha mpaka kwa yule njemba likampata kifani akaja mpka pale aka anza kukunjana na zikko pigana pigana mimi nikaona huyu atatufanya tukamatwe nikaokota jiwe lingine nimpige kichwani si tukimbie yule jamaa akasema "Huko kwenye hicho kiwanda tumeskia mlipuko nakuja kusaidia nyie mnanipiga nyie mtakua si watu wema" nikampiga jiwe la kichwa wakati anagulia zikko akamkata mtama piga ngumi za kutosha kanishika mkono mama tukimbie huyu atakua mwenzao tukakimbia mpaka tukatoka eneo lile tumechoka nguvu hatuna njaa inauma yaani tuna hali mbaya kuna mti tukawa tumekaa na tumepumzika na maana jua limeshakua kali hatari kiu yani wakati mgumu mno ghafla tukiwa pale tumezungukwa na watu kama watano wamejazia nikasema duh tumeisha hatuwezi kukimbia wala kufanyaje kuangalia mmoja wao ni yule tulie kutana nae kule tukamshambulia akasema "Hawa wanaonekana sio watu wema" tuka ambiwa tusimame tukasimama ila mmoja kati yao alikua amevaa pensi kma ya jeshi hivi nikawa najiuliza au ni wajeda
Wakatuchukua kutupelek sehemu ambayo hatujui ni wapi ila sio kule tuliko tokea yule aliepigwa anahadithia "Nilikua maeneo ya kule kiwandani nikaskia kitu kama mlipuko sasa nawahi nikajue ni nini si ndo nakutana na hawa ndugu wananishambulia ah yani wameniuza unajua" mmoja akacheka "Hahah ukiambiwa uache pombe hutaki sasa hawa wanakupigaje?" Akasema "Uyo mwanamke kanipa jiwe moja huwezi amini nyie hadithieni mlivo nifanyia" tupo kimya maana tumetangulizwa mbele alafu wao wako nyuma yule mbaba akanisukuma "Sema unajifanya mpole" ile kanisukuma tu nika anguka mpka chini "Zikko akaniuliza uko sawa?" Nikajibu "Ndio" akanisaidia kusimama alafu akamkata jicho yule mbaba alie nisukuma. Mmoja wao akasema "Mbona watu wenyewe hawana hata nguvu" yule baba akasema "Wanajifanyisha hao" tukafika sehemu hapo ndo nikajua kuwa wale ni wanajeshi na pale ni jeshini tukaingizwa mpaka ofisi sijui ndo ofisi ya kiongozi basi tukakalishwa tuka anza kuulizwa maswali na tukaeleza kila kikicho tokea tulipewa chakula tukala tukanywa maji wakasema watupeleke nyumbani maaana tulijitambulisha kama mtu na mumewe hatujafunga ndoa ila tunaishi pamoja.
Nikasema "Kwakweli mimi naogopa sana kwenda nyumbani sijui itakuaje ila siwezi kwenda kwa sasa" yule alieonekana kama ndio kiongozi pale alituhurumia akasema tutakaa pale kwa muda ili wao wafatitie tulicho waambia na eneo hili litiliwe ulinzi. Kesho yake nilipelekwa kazini na wanajeshi ili kutoa taarifa na nikapatiwa likizo ya mwezi mmoja.
Walipanga mikakati yao wakasema tujifanye chambo kama tunaenda nyumbani maana wa vyovyote vile watakua wanatufatilia ili watuue kabla hatuja enda nyumbani ikaja taarifa kwamba kuna gari inaonekana mtaa fulani siku ya tatu sasa haitoki kuulizwa mtaa tunaokaa ndo huo huo sasa wao wakasema wakafatilie kwanza sisitubaki pale jeshini baada ya lisaa limoja tukaitwa kule ofisini macho kwa macho na kelvy huwezi amini alikua pamoja na vijana wake watatu wamekatwa kwenye ile gari tuli itwa ili kuthibisha nilivo muona tu miguu illishiwa nguvu nikaanza kuogopa machozi yanatoka nakumbuka matukio ya nyuma roho inauma kumuamini mtu kama yule.
Aliadhibiwa pale na akafunguliwa kesi katika uchunguz alikutanioa na makosa mengi mno pamoja na mauaji alihukumiwa kifungo cha maisha ya kama anatoka kutoka jela alipie kwa uhai wake maana iyo anyongwe.
Basi tulipata amani tukaruhusiwa kurudi nyumbani ila pale tuliamua kuhama na kuliamisha duka na hatimae tukaingia kwenye mahusiano sasa..
Nilijikuta moyo wangu unampenda sana zikko na kwakweli ni yule mwanaume ambaye ni ndoto ya kila mwanamke mapenzi yalipamba moto sana na tulipendana mno tunasikiliza tunaheshimiana yani kila kitu Kiko sawa.. Siku moja tukiwa tumelala aliniuliza kuhusu mipango yangu nikamwambia mimi nawaza ndoa tuu sahii tukacheka zikko hakuwa tena mfanyakazi wangu nilimpa mamlaka yote ya dukani na yeye ndo akawa msimamizi wa vitu vyote.
Siku moja nikakuta msg kwenye simu ya zikko akichat na mwanamke yule mwanamke ana mwambia "Bwana mimi mapenzi ya siri siwezi" Zikko anamwambia "Vumilia kidogo mpenzi wangu lakini si kila kitu unapata?" Yule mwanamke akajibu "I want more than that mimi nahitaji tuishi pamoja" zikko akamwambia "Sawa usijali" moyo ulipasuka na uliuma sana wakati huo zikko alikua bafuni ana oga maana tuliamua kupanga nyumba yenye vyumba viwili na ni self contained. Niliposkia anakuja nilijikausha ila moyo una uma sana najiuliza huyu zikko wa kunifanyia mimi hivi? Nilisahau kufuta zile msg ili asijue kama nimesoma maana kuna msg mpya alikua ametuma yule dada kamwambia awahi ana msubiri.
Aliposhika simu yake akafungua msg aliniangalia akasema "Umesoma msg zangu?" Nikamwambia "Ndio" akasema "Kwanini?" Nikamwambia "Kwani siruhusiwi kushika simu yako?" Akasema "Unaruhusiwa ila haimaanishi unaruhusiwa kusoma msg zangu lini umeona mimi nimeshika simu yako?" Nikamwangalia kwa jicho la hasira sana na siku mjibu akaendelea kuvaa huku anagomba gomba tu kisha akaondoka tena bila kuaga nilifunga mlango nika anza kulia kwa uchungu moyo wangu uliuma sana nimempa mapenzi yote kila kitu namhudumia mimi kwanini anifanyie hivi? Amekosa nini huyu mwanaume??
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment