MAMA WA KAMBO 33

"Kuhusu kuja kukaa hapa wala usihofu kwanza hivi tunavyoongea ndio umehamia tayari na ishu niliyokuitia ni hii.Nataka kesho asubuhi ufanye juu chini upate bodaboda umgonge Baba Linna yani hakikisha mguu umevunjika au mkono,"Aliongea Joyce nakumwambia Thanga ishu aliyomuitia.
"Mh! Kumgonga na bodaboda,nitamgongaje mtu mwenyewe boss halafu kila muda yupo kwenye gari,"Thanga aliguna nakuuliza.
"Sasa nisikilize mimi Master Plan,iko hivi leo lala hapa asubuhi saa11 ondoka katafute bodaboda naimani mpaka kufika saa2 utakuwa umepata na ukipata kwa kua unajua kuendesha hakikisha saa2 kamili upo maeneo haya unaangalia ghetini maana mi nitamshawishi tutoke tunyooshe miguu,ukituona tunatembea we njo kwa kasi mgonge yani hakikisha anavunika mkono au mguu,"Joyce alimaliza kumwambia Thanga.
"Sawa hapo nimekuelewa vizuri kabisa pikipiki nitapata sema nahofia je hatoweza kunigundua,"Thanga aliuliza.
"Kukugundua hawezi bhana we utavaa nguo za kufanyia tukio huku umevaa helment,"Alijibiwa Thanga.
"Basi sawa na vipi kwanini umeplan hivyo?"Joyce Aliulizwa.
"Lengo langu nataka aumie wakati anajiuguza awe tu mtu wa kukaa nyumbani na mimi nianze kusimamia biashara zake na hapo ndipo nitazijua zote pia pesa bank nitatoa zote maana anazo nyingi mno si chini ya m800 sambamba na hayo akipona tu nitamfanya kipofu anaishi ishi kisha tunamuua nakwenda kumtupa,"Joyce alimjibu Thanga.
"Dah! Hapo nimekupata kweli unaplan kali na vipi kuhusu Police na Linna itakuaje."
"Thanga usiwe mshamba hivyo ,police tukiwa na pesa wanakuwa upande wetu na kuhusu Linna wala usihofu huyu mawili nitamuua mwili wake zile mbwa au nimfukuze maana hana chake saizi,"Aliongea Joyce akiinuka nakumkumbatia Thanga.
"Sawa baby basi nimekuelewa."
Walikumbatiana kama dakika 3 kisha wakaachiana na kuingia ndani,huko waliingia chumba cha wageni wakaanza kula burudani kwa raha zao huku Baba Linna akikoroma kwenye chumba chake ambacho alikuwaga analala na Mama Linna.
Joyce na Thanga walipeana burudani mpaka saa8 usiku ndipo wakalala maana walichoka balaa,saa11 kamili Thanga alimuamsha Joyce akamwambia aondoke pia nayeye arudi kwa Baba Linna ili asishtukiwe.
Joyce aliamka kwanza walioga haraka haraka kisha wakatoka nakuvaa nguo.
Walivyovaa akatoka Joyce nakuenda chumbani kwa Baba Linna nakumchungulia,alipokuta bado anakoroma tu akarudi nakumtoa Thanga huku akimpa pesa laki2 za kukamilisha kazi aliyompa ya kumgonga Baba Linna na pikipiki.
Alivyomtoa alirudi ndani nakulala pembeni ya Baba Linna na muda mtoto Linna bado alikuwa amezimia.
Saa1 kamili asubuhi mtoto Linna ndio alizinduka pale sakafuni,akajikuta anamaumivu mwilini na michubuko.Alichofanyiwa alikumbuka vizuri kabisa,alilia sana Linna huku akimuomba Mungu amrudishe Mamake lakini ndio hivyo amefariki dunia amelala milele hatorudi tena duniani na mbaya zaidi kwa macho yake alishuhudia jeneza ambalo ndani yake yupo mamake likishushwa kaburini na mwisho kufunikwa na zege.
"Mungu wangu nionee huruma kiumbe wako,sina ndugu Baba amenigeuka si yule aliyenipenda kwa dhati,upendo wake uliokuwa kwangu kauhamishia kwa Joyce mi si chochote kwake ,si kitu na ndio maana anathubutu kunipiga mpaka napoteza fahamu.Mungu wangu nionee huruma juu ya mateso haya,"Aliongea mtoto Linna akimuomba Mungu amuonee huruma kwani mateso aliyoyatabiri kipindi anamwambia Mamake ndio yameanza na hio ni kama trela tu picha kamili bado.
Baada ya Linna kuongea na Mungu wake,taratibu aliinuka nakwenda chumbani kwake huku akilia.
Alivyoingia alipanda kitandani nakulala.
Thanga nae baada kutolewa na Joyce pale kwa Baba Linna moja kwa moja alienda mitaa ya Sai kwenye gheto lake alipofika alilala kidogo,saa1 kamili aliamka akanawa uso nakupiga mswaki kisha akaenda kupata supu nzito ya kuku na chapati za kutosha.
Alipomaliza alienda kwenye kituo cha bodaboda kwa kua alikuwa anafahamika basi haikuwa shida kupata pikipiki,alidanganya tu kuwa kuna mahali anaenda.
Alilipia pesa akavaa helment nakwenda karibu na nyumba ya baba Linna,sehemu aliposimama palimfanya aone gheti la Baba Linna na sehemu ya mbele na yeye alipo asionekane na mtu.
Basi aliendelea kukaa pale huku akivuta muda saa2 ifike amalize mchezo.
Joyce na Baba Linna mpaka saa1 na nusu tayari walikuwa mezani wanapata chai nzito peke yao,licha ya kujua kuwa Linna aliamka lakini hawakumuita hakika ilikuwa ni roho mbaya.Walijali tu matumbo yao.
Walipomaliza kunywa ilikuwa saa1 na dakika 45 ndipo Joyce akamwambia Baba Linna anaomba watoke nje wanyoshe miguu kidogo,Bahati nzuri Baba Linna alikubali asijue anachoenda kufanyiwa.
Basi walitoka mpaka nje ya gheti wakaanza kutembea.
Thanga nae akiwa pale alipojificha akawaona,basi bila kupoteza akaiwasha pikipiki nakuanza kuwafa kwa nyuma bila wao kujua.
Alipowakaribia alivuta mafuta nakumfata Baba Linna kisha akamchota mzima mzima.
"Uwiiiii mamaaaaaa nakufaaaaaaa,"Baba Linna alipiga kelele kwa nguvu nakuita Mama na muda huo tayari alikuwa ametupwa pembeni ya barabara huku bodaboda iliyomgonga ikitokomea kusikojulikana.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment