Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 34


Here Comes The Movie About Africa's Most Scandalous Love Story ...


"Uwiiiii mamaaaaaa nakufaaaaaaa,"Baba Linna alipiga kelele kwa nguvu nakuita Mama na muda huo tayari alikuwa ametupwa pembeni ya barabara huku bodaboda iliyomgonga ikitokomea kusikojulikana.
"Jamani baby pole sana jamani msaada uwiiiii uwiiiii,"Joyce nae alipiga kelele huku akiomba msaada kinafki na muda huo Baba Linna alikuwa anaugulia maumivu pale chini.
Bahati nzuri watu wachache walikuja baada ya kusikia kelele za kuomba msaada,walipofika waliuliza nini tatizo Joyce akajibu kuna bodaboda imemgonga na kukimbia,"Alijibu huku moyoni akiwa na furaha tu sababu lengo lilikuwa linaenda kutimia.
"Dah! Poleni sana bodaboda hawana akili yani asubuhi asubuhi wanaamka wamelewa,ebu tumsaidie haraka inaonyesha ameumia,"Mwananchi mmoja ambaye jina lake halikufahamika aliongea.
Basi wale walimuinua Baba Linna nakumpakiza kwenye gari na safari ya kwenda hospital ikaanza huku Joyce muda wote akilia utafikiri ye ndio kaumia.
"Sasa tunaenda hospital ipi,"Dereva tax aliwauliza Joyce na wenzie ambao walikuwa wanamsaidia Baba Linna.
"Naona hospital ya meta hio karibu pia huduma zao ni nzuri,"Alijibu Joyce akisema hospital tofauti na ile ya rufaa ambayo aliendaga Mama Linna,hakutaka kabisa na Baba Linna apelekwe huko ndio maana alisema nyingine.
Basi hakuwa na neno zaidi ya kuongeza mwendo ili wawahi kufika.
"Iiiiiii mguu wangu na mkono iiii aah inauma sana uwiiiii uwiiii,"Baba Linna nae alizidi kulalamika mle kwenye gari inaonyesha aliumia sehemu hizo za mkono na mguu.
"Jikaze karibu tunafika,"Joyce alimfariji kinafki huku moyoni akisema hii trela tu picha lipo jikoni.


Baada ya dakika kadhaa walifika hospital wakapokelewa vizuri na huduma ikaanza,saa moja mbele tayari Madaktari walishajua kuwa Baba Linna kavunjika mkono pia kateguka mguu hivyo itabidi alazwe.
"Pole sana baby jamani,yani nakuonea huruma sana ila usijali utapona,"Joyce alimfariji kinafki Baba Linna wakiwa wodini.
"Asante sana baby dah ila yule bodaboda ningemjua mi ningemweka ndani."
"Achana nae baby kikubwa upo hai ni kumshukuru Mungu tu,"Alisema Joyce.
"Sawa baby basi nenda nyumbani ukampe mtoto chai halafu urudi na pesa kidogo maana hapa sina hata mia,"Alisema Baba Linna.
"Ok! Baby siunajua pesa sina lakini inabidi unipe card nikatoe bank,"Aliongea Joyce huku moyoni akisema akienda bank lazima ahamishe mzigo wote uwe kwenye account yake.
"Kweli card ingia kule chumbani utaiona juu ya dressing table,nenda katoe millioni2."
"Sawa baby basi nikuache narudi baadae na chakula,"Aliongea Joyce kisha akaondoka mle wodini,alipofika nje alikodi tax ikampeleka nyumbani na muda wote alikuwa na furaha sana.




Thanga Mobeto nae baada ya kumgonga Baba Linna alirudi pale kijiweni na kukabidhi ile pikipiki kisha akaenda zake hotelini kupumzika.
"Saizi naenda kuwa tajiri,"Aliongea Thanga mle chumbani ndani hotel.
Akiwa anaongea hayo simu yake ikaita,alipoangalia mpigaji alikuta ni Joyce Chibomoto mpenzi wake bibi plan.
"Baby niambie shwari,"Aliongea Thanga baada ya kupokea simu.
"Shwari kabisa aisee,kwanza nikupe hongera kazi umeifanya vizuri sana kwa nije nikupe kitumbua kisha twende bank tukahamishe pesa,"Aliongea Joyce.
"Wawoooo kipenzi ndio maana nakukubali sana,basi nakusubiri mwaaaaaaaaaaa,"Alisema Thanga nakukata simu.



Joyce Mobeto kule nyumbani alipofika kwanza alioga vizuri kisha akaenda kumuamsha mtoto Linna.
Alipoamka alimwambia huo muda sio wa kulala pia amsikilize kwa makini anachoongea.
"Sawa Aunt nimekusikia nitawahi kuamka kila siku,"Alisema Lina huku akifuta machozi.
"Kwanza kuanzia leo usiniite Aunt maana mi sio Dada wa Baba ako wala mdogo wa Baba ako hivyo niite boss,sijui umenielewa we mbwa,"Aliongea nakuuliza Joyce.
"Nimekuelewa boss,"Aliongea Linna huku usoni akionekana mnyonge kabisa.
"Ok! Jambo la pili nataka uchague moja ya mawili,moja uwe mfanyakazi wa humu ndani malipo yake kiwe chakula au uondoke hapa nyumbani ukawe mtoto wa mtaani,"Aliongea Joyce huku amemkazia macho mtoto Linna.
"Mama tayari yametimia na shule ndio basi tena,"Aliwaza Linna baada ya kuambiwa vile huku akitafakari  achague kipi.
"Lakini boss Baba alisema naenda shule,kwanini usitafute mfanyakazi wa humu ndani,"Alisema Lina kwa upole.
"Baba gani yupi unamsema,"Aliulizwa Linna.
"Baba huyu wa kwangu,"Linna alijibu.
"Nafuu umenikumbusha maana nilisahau,kuanzia hivi tunavyoongea yule siyo babako ni boss wako na hivi tunavyoongea yupo hospital,"Alisema Joyce akikaa sofani.
"Lakini ni babangu usinifanyie hivyo,mi ni yatima saizi nitakuwa mgeni wa nani ukisema Baba nimuite boss."
"Linna sihitaji maswali ebu chagua haraka kuna sehemu naenda na ukithubutu kutoka nje ya hii nyumba nakuua nakwenda kukutupa,"Aliongea Joyce nakumtishia Linna.
Linna akafikiria akaona kwenye yale mambo mawili bora achague kuwa mfanyakazi wa ndani ili akiona mambo yamekuwa magumu atoroke.
"Nimekubali kuwa mfanyakazi wako boss,"Linna alimwambia Joyce.
"Wawoooo hapo vizuri,sasa naondoka mara moja nikirudi nikute nguo zangu umefua,vyombo umeosha,nyumba ipo safi na nikute upo kumwagilia maua,"Aliambiwa Linna.
"Lakini kazi nyingi nitaweza kweli,"Aliongea Linna.
"Ndio maana yakuwa mfanyakazi,tukutane baadae,"Aliongea Joyce akiinuka nakutoka nje.
Nje alimuita Masai nakumwambia chai ipo ndani atakunywa pia ahakikishe Linna hatoki kisha akaingia kwenye gari la Mama Linna nakutoka nalo.
Break ya kwanza ilikuwa ni hotelini kwa Thanga,alipofika kilichoendelea ni Simba na Yanga uwanja wa fundi selemara mkwakwani.




Kule jijini Dar Es Salaam Mama Linna na Sophia mke wa Dokta saa1 kamili walikuwa wameamka wapo kuandaa kifungua kinywa huku wakipiga story za hapa na pale.
Ilipofika saa3 tayari walikuwa wamekunywa chai pia wamejiandaa vizuri huku Mama Linna akiwa amevaa nguo nzuri na hijabu ili watu wasimgundue.

Saa4 na robo tayari walikuwa njiani kuelekea bank kutoa pesa za mmewe Baba Linna nakuweka kwenye account yake ili yule mkewe aliyemuoa hata akienda akukute kuna linda account tu.
Wakati Mama Linna na Sophia wanaenda bank Joyce nae ndio alikuwa anaanza safari ya kwenda bank kuhamisha pesa ili ziwe chini yake,hakuwa pekeake bali na Thanga.
Iliwachukua robo saa tu mpaka kufika bank,walipofika Joyce hata hakupoteza muda aliingia ndani nakupanga foleni.

HAYA SASA WOTE WANATAKA KUTOA PESA NANI ATACHANA MKEKA WA MWENZIE JOYCE AU MAMA LINNA TUKUTANE SEHEMU IJAYO

Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4