Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 35


Here Comes The Movie About Africa's Most Scandalous Love Story ...


Wakati Mama Linna na Sophia wanaenda bank Joyce nae ndio alikuwa anaanza safari ya kwenda bank kuhamisha pesa ili ziwe chini yake,hakuwa pekeake bali na Thanga.
Iliwachukua robo saa tu mpaka kufika bank,walipofika Joyce hata hakupoteza muda aliingia ndani nakupanga foleni.

Mama Linna na Sophia nao tayari walikuwa wamefika bank,na kwa kua Sophia alikuwa mhasibu basi Mama Linna hakupanga foleni badala yake alienda ofisini mwa Sophia na Sophia akaanza kushughulikia akisaidiana na manager wa bank pamoja na cashier yule wa dirishani maana walikuwa marafiki sana ukiacha kuwa wanafanya kazi pamoja.
Kilichofanyika nikutoa pesa kwenye account ya Baba Linna zaidi ya milioni 800 kisha kuziweka kwenye account ya Mama Linna na mchezo ukawa umeisha na wakaseti vizuri ili Baba Linna kule siku akiangalia akute pesa ilitolewa na si huhamishwa.
Baada ya hapo Mama Linna akawa na furaha sana,wale waliomsaidia akiwemo Sophia akawapa milioni 10  kumi kila mmoja kisha akakaa mle ofisini na Sophia mpaka muda wa kurudi nyumbani ulipofika wakarudi wote na maisha ya Mama Linna kule Dar Es Salaam yakawa hivyo raha mstarehe,pesa ipo na ujauzito unaenda vizuri.






Joyce nae pale bank zamu yake ilifika,akatoa maelezo vizuri kuwa anataka kuhamisha pesa zote kwenye account ambayo alimtajia,yule mtu wa dirishani akampa karatasi aandike maelezo fulani.
Joyce aliandika akampa,ajabu baada ya dakika nne yule mtu wa dirishani akamwambia account anayosema ina elfu30 tu.
"Kaka unasemaje,"Joyce aliuliza kwa mshangao asiamini alichosikia maana tayari Mama Linna alishafanya yake inamaana nae angechelewa tu basi ingekula kwake.
"Nimesema hivi account unayotaka pesa itoke iende kwenye account yako ina elfu 30 tu,"Alijibu yule mhudumu huku akicheka.
"Mh! Sawa kakangu basi acha tu,"Alisema Joyce nakutoka nje huku akiwa na hasira kali mno maana alijua Baba Linna kamdanganya kumbe wala mama lao mamake Linna amewazidi akili.
"Vipi baby mambo ni safi ee mzigo upo ngapi?,"Thanga alimuuliza Joyce baada ya kuona anaingia mle kwenye gari.
"Mambo safi wapi yani baby siamini kabisa nilichokiona,supu imeingia nzi,shilingi imepinduka,"Joyce aliongea huku machozi yakimlengalenga.
"Supu imeingia nzi kivipi tena,mbona sikuelewi baby,"Thanga aliuliza.
"We nae maanake account pesa haina ina elfu 30 tu,"Joyce alijibu.
"Utakuwa umekosea bhana,tajiri kama yule hawezi kuwa na elfu 30.Mi naona atakuwa na account nyingine anayoweka pesa,"Alisema Thanga.
"Inawezekana ee,"Alisema Joyce.
"Ndio inawezekana ebu nenda kamuulize vizuri pesa ziko wapi,"Thanga alimwambia Joyce.
"Sawa twende wote."
Joyce na Thanga waliondoka pale bank nakwenda hospital,walipofika walienda sehemu alipolazwa Baba Linna VIP chumba cha pekeake.
"Baby pole huyu ndio mdogo wangu anaitwa Thanga,ameona aje akuone,"Aliongea Joyce akimtambulisha Thanga.
"Ooh! Sawa sawa nashukuru kukufahamu shemeji,"Alisema Baba Linna akimpa mkono Thanga.
"Asante sana Shem pole sana kwa ajali,"Aliongea Thanga huku moyoni akisema unabahati wewe ungekufa.
"Asante aisee,"Alisema Baba Linna.
"Sasa mme wangu ile account uliyoniambia nikachukue pesa nimeenda nimekuta kuna elfu30 tu hivyo sijachukua nimeacha tu labda kama ipo account nyingine unayowekaga pesa tukachukue,"Aliongea Joyce akimwambia Baba Linna.
"Mke wangu kuna elfu 30 kivipi wakati kuna pesa nyingi mle zaidi ya milioni 800 na mi sina account nyingine ni hio hio na ndio tulikuwa tunatumia mi na mke wangu,"Aliongea Baba Linna huku machozi yakimlengalenga maana alijua tayari kaibiwa kama kweli hazipo.
"Haaa!! Baby unasema account ndio hio hio yani hamna nyingine,"Joyce alishangaa nakuuliza.
"Ndio moja tu,"Baba Linna alijibu.
"Basi ndio hivyo ina elfu 30 tu labda tuombe ruhusa ujikaze twende bank ukaangalie mwenyewe maana mi siwezi kukubali kuwa na wewe kama account ina elfu 30 labda uuze mali zako uwe na pesa,"Aliongea Joyce huku akiwa amenuna.
"Usihofu mke wangu naenda mwenyewe kuangalia tena mida hii hii muite Dokta niombe ruhusa,"Aliongea Baba Linna,Joyce nae haraka akamuita Dokta.
Dokta alipofika Baba Linna akamwambia ukweli kuwa anaomba ruhusa,kwa kuwa alikuwa mtu mkubwa na tajiri Dokta wala hakukataa zaidi ya kumwambia aende pia kesho yake arudi pia akampa na dawa.


Baba Linna baada ya kuruhusiwa na kulipiwa pesa na Joyce wakatoka mle hospital nakwenda bank.
Walipofika Baba Linna ye mwenyewe akaenda kuangalia account yake inashilingi ngapi jibu likawa lile lile account ina elfu 30.
"Inamaana pesa zangu nimeenda wapi jamani iiiiiii iiiiiii ,"Aliongea Baba Linna huku akianza kulia mle mle bank.
"Boss account yako inaonyesha pesa ulitoa,"Alijibiwa Baba Linna.
"Hii hujuma jamani mi sijatoa kabisa iiii iii pesa zangu sasa itakuaje."
"Itakua hivyo hivyo na pesa zenu za manyoka,"Yule mhudumu wa bank alitukana kimya kimya?.
Basi Baba Linna Linna hakua na jinsi zaidi ya kutoka mle bank akichechemea nakwenda walipo Thanga na Joyce.
Alipofika alimwambia Joyce kuwa ndio hivyo pesa imebaki elfu 30 tu na anahisi kuna mtu ameiba.
"Baby sasa itakuaje maana mi sikuelewi kabisa,"Joyce baada ya kumfariji mwenzie ye akaanza kuuliza itakuaje maanake wataishije bila pesa maana aliona kabisa ndoto zake zinayeyuka kama barafu juani.
"Mke wangu hapa nimechanganyikiwa sana sijui hata nifanyaje au ni wewe umetoa hizo pesa,"Aliongea Baba Linna nakuuliza.
"We koma kabisa nichukue nipeleke wapi,siungeziona ninachotaka sasahivi uuze magari yote mawili libaki moja hili ambalo naendesha pia uuze vituo vya mafuta ili tuwe na pesa ya kutosha au unasemaje mdogo wangu,"Aliongea Joyce nakumuuliza Thanga.
"Ni kweli Dada unayosema ni kweli,shemeji msikilize anachoongea Dada,"Aliongea Thanga kwa sauti ya upole ila ndani yake ya kinafki.
"Sawa nimewaelewa nitafanya hivyo tutabaki na hotel mbili tu na nyumba ile tunayoishi,"Baba Linna aliongea kiunyonge huku akilia.
"Ndio hivyo anza kufanya taratibu mida hii hii mpaka jioni pesa iwe imepatikana,"Alisema Joyce.
"Sawa mke wangu basi twende nyumbani."
Joyce aliwasha gari wakaanza kwenda nyumbani huku Baba Linna akiwa mnyonge sana.
Walipofika nyumbani walikuta Linna yupo kumwagilia maua.
Linna nae alivyomuona babake nakuona anachechemea akaacha kumwagilia nakumkimbilia  ili amuulize nini tatizo,ajabu alimpofikia alisukumwa na Babake akaanguka chini puu!!.
"Baba nimekukosea nini unanisukuma,"Aliuliza Linna akiwa pale chini lakini hakujibiwa.
Alivyoona Babake anaingia ndani pamoja na Joyce nae akaingia na muda huo Thanga alikuwa ghetini anapiga story na Masai.
Baba Linna baada ya kufika sebuleni alianza kumpigia moja ya marafiki zake nakuanza kuongea nae kuhusu kuuza magari mawili na vituo vya mafuta ambavyo alikuwa anamiliki.
"Kaka kama nilivyokwambia nauza magari mawili na vituo vyote nataka nibaki na hotel tu,"Aliongea Baba Linna simuni na upande wa pili na Linna maongezi hayo aliyasikia kwa uzuri kabisa maana alikuwa pale pale.
"Hio haina shida pesa ngapi sasa jumla,"Yule wa upande wa pili aliuliza.
"Jumla ni milioni 752,"Alijibu Baba Linna.
"Sawa sema toa 2m hapo nitakupa 750m,sema inabidi tutafute wanasheria tuandikishane ili usijenigeuka."
"Ondoa shaka kuhusu hilo nadhani kesho saa5 tufanye makabidhiano tu."
"Sawa haina shida,"Aliongea Baba Linna nakukata simu.
"Baby siumesikia lakini kesho tutakuwa na m750,"Aliongea Baba Linna akimwambia Joyce na Linna alisikia kabisa sema hakutaka kutia neno.
"Eeh baby uza tubaki na nyumba hii pamoja na hotel zinatosha sana kuliko kuwa na mibiashara mingi inachosha,"Aliongea Joyce.
"Mh! Kumbe ndio mipango yao subiri kesho nitaangalia kwenye bahasha aliyonipaga mama nifiche juu ya dari nione nini kimeandikwa,"Aliwaza Linna akiondoka pale sebuleni.


Siku hii Linna hakunyanyaswa kabisa sababu kazi zote alizifanya ingawa alichoka sana,hata chakula alikula vizuri kabisa.


Siku ya pili Baba Linna,Joyce pamoja na Thanga waliondoka pale nyumbani kwenda kuuziana magari na vituo vya mafuta huku Linna akibaki pale nyumbani na Masai ambaye alikuwa ghetini.
Linna wala hakupoteza muda kabisa akaenda chumbani kwa Babake akapanda juu ya dari nakuchukua ile bahasha kisha akafunga vizuri nakwenda chumbani kwake.
Huko akaifungua nakukata hati original za nyumba yao ya kifahari imeandikwa jina lake pamoja na zile hotel mbili za ghorofa nne 4 zimeandikwa jina lake.Baada ya kujua kumbe siku ile mamake alimpa kitu cha maana basi akapata plan ama kitu cha kufanya ili kuzinusuru zisiuzwe maana ni mali zake kabisa.

Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4