MAMA WA KAMBO 36

Siku ya pili Baba Linna,Joyce pamoja na Thanga waliondoka pale nyumbani kwenda kuuziana magari na vituo vya mafuta huku Linna akibaki pale nyumbani na Masai ambaye alikuwa ghetini.
Linna wala hakupoteza muda kabisa akaenda chumbani kwa Babake akapanda juu ya dari nakuchukua ile bahasha kisha akafunga vizuri nakwenda chumbani kwake.
Huko akaifungua nakukuta hati original za nyumba yao ya kifahari imeandikwa jina lake pamoja na zile hotel mbili za ghorofa nne 4 zimeandikwa jina lake.Baada ya kujua kumbe siku ile mamake alimpa kitu cha maana basi akapata plan ama kitu cha kufanya ili kuzinusuru zisiuzwe maana ni mali zake kabisa.
"Asante Mama kwa zawadi hii nitaitunza isiuzwe wala isiporwe na Aunt na hata ikiporwa hati nitaficha nikiwa mkubwa nitairudisha mikononi mwangu,"Aliongea Lina pekeake akienda stoo ya magari ambako Babake alikuwa anahifadhi vitu vya magari,Lina alipofika alitafuta box la chuma dogo Bahati nzuri akalipata.
Alilichukua nakurudi nalo chumbani kwake,mle chumbani mwake alichukua nguo ya mamake akaweka ndani ya box,pia ile bahasha yenye hati akahifadhi kwenye mfuko na rambo zile ngumu kisha akaweka vizuri ndani ya box la chuma.
Baada ya hapo akafunga vizuri nakutoka nalo nje pamoja jembe ambalo alichukua stoo.
Alipofika nje alitafuta sehemu isiyofikika wala kugunduliwa na mtu kuwa chini kuna box akachimba shimo nakuingiza lile box lililohifadhi hati kisha akafukia vizuri na juu akapanda maua miba.
"Saizi hata wanifukuze wajue tu siku nikiwa mkubwa mali zangu zitarudi labda waniue kama Mama,"Alisema Lina akiondoka pale alipofukia hati nakwenda stoo kurudisha jembe.
Baada ya kurudisha jembe alienda ghetini kwa Masai kumuuliza muda ili akamalizie kazi alizopewa na Joyce.
"Mi saa aina,mi huangalia muda kupitia jua,"Masai alimwambia Linna huku akiendelea kutafuna ugolo wake.
"Mh!,"Aliguna Linna nakurudi ndani?.
Joyce,Baba Linna na Thanga walifika sehemu waliyopanga kukutana na yule rafiki yake ambaye ananunua vituo vya mafuta na magari ya Baba Linna,walipofika walikuta tayari mwenzao ameshafika yupo na mashaidi.
Walisalimiana vizuri na kabla ya yote moja ya mashaidi ambaye pia ni mwanasheria akaomba wakaone kwanza vituo vya mafuta na hayo magari.
Wote wakakubaliana kweli waangalie kwanza mali ndio biashara ifanyike,walianza kwenda kituo kimoja kisha kingine mpaka cha mwisho ambacho na magari yalikuwa pale.
"Bila shaka umeona na umeridhika,"Aliongea Baba Linna akimwambia yule rafiki yake.
"Nimeona ndugu yangu basi tuandikishane kabisa tuende bank tukalipane,"Alisema rafiki yake.
"Sawa."
Baada ya hapo waliandikishana pamoja na taratibu zingine zilifanyika ikiwemo kukabidhi nyaraka za TRA na Ewura.
Walipomaliza walienda bank,huko bila kupoteza muda walihamisha pesa 750m zikaingia kwenye account ile ile ya awali ya Baba Linna na muda huo wakati pesa zinaingia Joyce alikuwa sambamba kabisa na Baba Linna lengo lake aone mzigo unavyoingia.
"Ndugu yangu bila shaka umeona na tumemalizana,"Aliongea rafiki yake Baba Linna.
"Ndio ndugu asante sana,"Aliongea Baba Linna huku wakishikana mikono na baada ya hapo wakaachana na hivyo ndivyo Baba Linna alivyouza vituo vitatu vya mafuta na magari mawili huku akibaki na nyumba ya kifahari moja,gari moja v8 pamoja na hotel mbili ambaye mmiliki halali ni Linna mwanae sababu hati zimeandikwa jina lake na ndio zile amezificha Linna chini ya ardhi.
"Mke wangu kipenzi turudi nyumbani maana pesa umeona,"Baba Linna alimwambia Joyce.
"Ndio baby wangu ndio maana nakupenda sana jamani sitokuacha mpaka pale kifo kitakapotutenganisha,"Aliongea Joyce kinafki huku moyoni akisema.
"Hili wiki lazima ufe nyau wewe shida yangu kwako ni pesa,mapenzi yangu yapo kwa Thanga mwanaume ninayempenda tangu tunanyonya."
Hivyo ndivyo alivyosema Joyce moyoni akiwasha gari la Mama Linna nakuondoka pale bank.
Wakiwa njiani kuelekea nyumbani moyoni Joyce aliwaza namna ya kumuua Baba Linna,alitaka kifo cha Baba Linna watu wasijue kuwa ye ndio mhusika yani waone kabisa.
"Hapa huyu inabidi kwanza niende kwa mganga amroge macho awe kipofu,akiwa kipofu nitakuwa namfungia ndani namnyima chakula.Akianza kupungua mwili atakuwa anatoka nje mara kwa mara na watu watasema mawazo kifo cha mkewe ndio maana anakonda kumbe ni plan zangu afe na hapo nitamuua kiulaini na kwa kua hana ndugu mbona raha nitamtupa porini,"Joyce aliwaza na mwisho akapata plan namna ya kuanza kumuua taratibu.
"Hahaha jamani,"Joyce alicheka baada ya kumaliza kuwaza nakupata majibu.
"Jamani mke wangu umefurahi nini?."Aliuliza Baba Linna huku akishuka kwenye gari nakuingia ndani?.
"Ah! Aah mme wangu jamani nimefurahi tu,"Alijibu Joyce huku akimkonyeza Thanga.
"Aya bhana,"Alisema Baba Linna kinyonge,basi waliingia ndani nakukaa sebuleni.
Dokta Magnus akiwa kazini kwake na muda huo alikuwa free aliamua kumpigia Mama Linna nakumwambia mmewe ameuza vituo vitatu vya mafuta na magari mawili hivyo kupitia simu yake aangalie salio la account ya mmewe huenda pesa zimewekwa humo na kama zipo ahamishe aache m100 au 50m.Dokta alimaliza kumwambia Mama Linna.
"Jamani asante sana Dokta kwa taarifa hio kwa niangalie sasahivi,"Alisema Mama Linna.
"Ndio angalia mi ameniambia mchungaji muda si mrefu,"Aliongea Dokta nakukata simu.
Mama Linna baada ya kuambiwa vile hata hakupoteza muda,aliingia kwenye simu yake akaangalia salio kweli akakuta inasoma 750m.
"Wawoooo kwa niwasiliane na Sophia ahamishe sasahivi aache m50 tu hio watakunywa soda,"Aliongea Mama Linna kwa furaha nakumpigia simu Sophia ili atoe pesa nakuweka kwenye account yake kama walivyofanya mwanzo.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment