Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 37


Here Comes The Movie About Africa's Most Scandalous Love Story ...

Mama Linna baada ya kuambiwa vile hata hakupoteza muda,aliingia kwenye simu yake akaangalia salio kweli akakuta inasoma 750m.
"Wawoooo kwa niwasiliane na Sophia ahamishe sasahivi aache m50 tu hio watakunywa soda,"Aliongea Mama Linna kwa furaha nakumpigia simu Sophia amwambie atoe pesa aingize kwenye account yake kama walivyofanya mwanzo.
Sophia nae alipokea simu mama Linna akamwambia kuwa atoe pesa kwenye account ya mumewe aingize kwenye account yake,Sophia wala hakukataa muda huo huo simu ikiwa hewani aliangalia kweli akakuta kuna 750m.
"Niache ngapi kwenye account ili wasishtuke mapema,"Sophia alimuuliza Mama Linna.
"Bakiza 50m nyingine fanya kama nilivyokwambia,"Alijibu Mama Linna.
"Sawa Dada baada ya nusu saa chungulia utakuta tayari,"Aliongea Sophia.
"Sawa asante sana,"Alisema Mama Linna nakukata simu huku akiwa na furaha.
"Yani huyu mwanaume bure kabisa anauza vituo vya mafuta ili pesa ale na huyo hawara wake sasa imekula kwake zile mali ni za mtoto wetu Linna na atakoma,"Aliongea Mama Linna pekeake akiwa sebuleni.
Nusu saa ilipofika simu ya Mama Linna ziliingia massage zikimjulisha kuwa account yake ile ya siri zimeingia pesa,alipofungua nakuangalia alikuta ni 700m zimeingizwa.
"Wawoooo hapa imekula kwao,pesa hizi nitanunua mjengo wa kifahari nchi nitakayohamia na wanangu Linna na huyu kijacho,"Aliongea Mama huku akituma massage kwa Sophia kumjulisha kuwa pesa zimeingia.
"Sawa Dada basi baadae leo nawahi kurudi,"Sophia alijibu kwa massage na hivyo ndivyo Mama Linna alipochukua pesa kwa mara ya pili kiulaini.






Joyce na Baba Linna walikuwa na furaha sana ya kupata pesa,Baba Linna hakutakiwa kuwa na furaha sababu ameuza kitu kinachoingiza pesa tena kwa hasara lakini kwa kua tayari alishakula limbwata hakuwa na namna zaidi ya kufurahi wasijue mama Linna ambaye wao wanajua ni marehemu tayari ameshalamba mzigo karibu wote kawaachia 50m tu.
"Mke wangu nakuomba sana nikikutuma bank uchukue pesa ninayosema,zile pesa inabidi tutumie kwa umakini na saizi nenda kachukue laki5 ya matumizi,"Aliambiwa Joyce na Baba Linna.
"Sawa baby kwa niende na mdogo wangu akachukue nguo zake,"Alisema Joyce huku moyoni akisema hizo 750m ni zangu zote wewe nakuua tu muda si mrefu.
"Sawa muende."
Joyce alijiandaa kisha akatoka na Thanga kwenda bank kisha kuchukua nguo huku wakiwa na furaha sana maana tayari pesa walishaziona na Joyce kwa muda huo hakuwa na akili ya kusema ahamishe pesa ziwe kwenye account yake,ye alitaka atumie ile ile ya Baba Linna asijue Mama Linna anaijua vizuri kabisa.Lakini kingine hakuwa na hofu sababu Joyce alijua mama Linna amelala milele,hatoamka.
Walipofika bank Joyce hakutaka kuingia ndani badala yake alienda tu kwenye mashine ya ATM akatoa pesa laki5 akarudi na Thanga wakaenda hotelini kula burudani maana bado walikuwa wanadai,alilipia mwezi na zilibaki siku 21.
Hotelini walifanya kilichowapeleka,walipotosheka waliongea kuhusu penzi lao na namna watakavyokuwa wanaishi pale kwa Baba Linna kwamba wawe wanalala chumba kimoja.
Hilo walilipitisha sababu mpango wa Joyce ulikuwa ni kumfanya kipofu hivyo Baba Linna mengi asingejua wakati wanafanya yao.
Baada ya hapo walimuita mhudumu wa reception wakamwambia wao wanaondoka hivyo ahakikishe hicho chumba analala mtu pesa watagawana siku21 zikitimia.
Mhudumu wala hakukataa,alikubali nakuahidi siku21 zikifika atamjulisha.
Hilo likaisha Joyce na Thanga wakaenda kwenye gheto lake maeneo ya Sai,huko walichukua nguo nakurudi nyumbani kwa Baba Linna ambapo ndipo patakuwa makazi yao sababu nyumba wanaenda kuimiliki baada ya kumuua Baba Linna na kumfukuza Linna.
"Jamani mbona mmechelewa sana kurudi saa11 jioni toka saa7 duh,"Alisema Baba Linna baada ya kuona Joyce na Thanga wanaingia wakionekana wamechoka sana,hakujua kuwa wenzie ni wapenzi na hapo wanamchora tu.
"Baby mbona unakela hivyo we tukichelewa kinakuuma nini jamani,vitu vingine viwe vinakupita sio kila kitu unaongea shauri yako,"Aliongea Joyce nakuenda chumbani kwake huku akimwacha Baba Linna akitingisha kichwa tu kumaanisha ameelewa alichoambiwa.
"Shem usiwe unamuudhi Dada,"Thanga alimwambia Baba Linna maana ye wakati Joyce anaingia chumbani ye alibaki sebuleni.
"Nimekuelewa shem huyu Dadako ni mkali sana,"Alisema Baba Linna kiunyonge huku akimwangalia mwanae Linna ambaye alikuwa pembeni.
"Eeh! Kuwa makini la sivyo uandike umenoa,"Aliongea Thanga.
"Unamaana gani kusema hivyo?,"Baba Linna aliuliza.
"Sina maana yoyote ila muda utaongea tu yangu macho,"Aliongea Thanga akiinuka nakumfata Joyce chumbani huku akimwacha Baba Linna mdomo wazi.
"Baba hivi unajua huyu si mdogo wake bali ni mpenzi wake na wanapendana sana,"Linna alimwambia Babake akijua huenda akachukua hatua.
"We mpumbavu koma kabisa kuongea hivyo,yule ni shemeji yangu anaitwa Thanga na sitaki usinifatilie niache na maisha yangu na ukiendelea nitakufukuza hapa nyumbani muone kule paa!!!!!,"Aliongea Baba Linna kwa ukali nakumpiga mwanae Linna asijue mwanae yupo sahihi.
"Sawa Baba we nitukane tu nakunipiga ila jua nitakayeteseka ni mimi na kitu Baba ambacho hujui unatakiwa ujue ni hiki,mchezo uliomfanyia mama wa kumdanganya kuwa Joyce ni mdogo wako na mwisho kumuua mama ndio Joyce anakufanyia wewe huyo sio mdogo wake ni mmewe we wanakuchora tu mwisho wanakuua,"Aliongea mtoto Linna kwa huzuni nakuondoka pale sebuleni.
"Huna lolote mnoko wewe na kwa taarifa yako Joyce ananipenda kuniua hawezi na yule ni shemeji yangu we utabaki hivyo na majungu yako mjinga wewe,"Aliongea Baba Linna akimsifia Joyce nakumtukana Linna,hakika limbwata lilikuwa on Doro Kakema husema ni hivi.Baba Linna alikuwa haambiwi wala hasikii kuhusu Joyce,Joyce alimteka haswa.
Baada ya Lina kuondoka pale sebuleni,alivyomjinga yale aliyoambiwa na mwanae alimuita Joyce nakumwambia.
Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4