Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO:04


Review: 'Tyler Perry's Temptation' is very Perry, indeed - Los ...
Akavuta mara ya pili akakuta hali ni ile ile mlango umefungwa, akaanza kutafuta funguo sehemu zote lakini alizikosa moyoni alijua ni mkewe kazificha kumbe ni Linna?.Alichukia sana Baba Lina
maana alipanga akale kitumbua cha baby wake Joyce.
Baada ya muda
aliamua kurudi kulala,akiwa amelala simu yake iliingia massage kuangalia akaona jina la baby wake chumba cha pilli ambaye ndio Joyce.
Akafungua ujumbe ukasomeka,(JAMANI BABY MBONA IVO).
Baba Linna alichanganyikiwa sana akamjibu(baby mlango umefungwa yani sijui nani kafunga).
Baada ya muda ikaingia msg kutoka chumba cha pili.
"Mh! Baby we muongo au hunipendi."
"We nakupenda sana tatizo mlango kama huamini njoo ujaribu kufungua,"Baba Linna nae alizidi kujitetea.

"Nakuja kuangalia,maana hapa shida nipo hoi."

"Njo huenda funguo zipo kwa nje."

"Sawa baby."
Baby mtu aliamka kitandani,alishuka alifungua mlango akanyata mpaka kwenye mlango wa wenyeji wake.Alipofika alizungusha kitasa akakuta hakifunguki na muda huo huo akaamua kutuma massage.
"Baby nipo hapa mlangoni jamani hata funguo haipo."

"Dah! Kama haipo basi kesho,"Baba Linna alimjibu.

"Mh! Baby ebu njoo ufungue nione yaani mi siamini kabisa kwamba funguo haipo."

"Aya nakuja utaona kitasa kinazungushwa."
Kumbuka walikuwa wanajibizana kwa njia ya massage.
Baba Linna aliamka kwa mara ya pili akazungusha kitasa ili baby wake aamini kuwa funguo haipo.
Kweli baby mtu akakubali kishingo upande moyoni akijua Baba Linna hampendi,akatuma massage.
"Baby sijapenda ulichonifanyia asubuhi na mapema nataka unipe haki yangu la sivyo naondoka,"
Baba Linna aliupokea ujumbe huo,nae akajibu.

 "Wala usihofu mke wangu kipenzi nitakupa haki yako na aliye funga nitajua tu kama ni Linna nitamkomesha asubuhi,usiku mwema."
"Sawa baby nawe pia mwaaaaaaaaaaa!!!!"
Mazungumzo yao yaliisha na Baba Linna akalala.




Saa kumi kamili juu ya alama Linna aliamka alikumbuka usiku alifunga mlango.
"Mh! Kwa nikafungue kabla hawajaamka ili wasiseme ni mimi,"Alijisemea Linna moyoni, alishuka kitandani akachukua funguo zote tatu.Akatoa moja akaishika mkono wa kulia na mbili kushoto kisha akaenda
ulipo mlango wa chumbani wanakolala mama na baba yake.
Alipofika aliingiza funguo ile moja taratibu, alifungua akashika kitasa nakuzungusha kisha akasukuma mlango taratibu akaingia na Bahati nzuri alikuta wote wamelala fofofo.
Funguo akaiweka kichwani kwa mamake,ili baba ke akiwahi kuamka amuulize mamake na mamake ampe funguo,ionekane kama mama ndo kaficha funguo kumbe hamna na lengo yeye Lina asigundulike.Baada ya hapo alitoka mle chumbani taratibu akaufunga mlango na funguo zile mbili kisha akarudi chumbani kwake nakulala.
"Hapa nimemaliza sina kesi kwa Baba,"Aliongea Linna  peke yake  wakati anajifunika vizuri.






Saa kumi na mbili Baba Linna aliamka akamuamsha mkewe akaamka.
"Mme wangu za asubuhi."
"Safi tu mke wangu ebu kanichukulie mswaki kule stoo,"Baba Linna alimwambia mama Linna ili aone atafunguaje mlango,au nae atauliza funguo zipo wapi,na akiona anauliza funguo basi moja kwa moja anajua Linna ndio alifunga mlango.
"Sawa mme wangu,"Mama Linna alitoa shuka ile anashuka mkono wa kulia ukagusa funguo.Akaichukua bila mmewe kujua,akashuka kitandani akavaa kitenge akafungua mlango akaenda stoo kuchukua mswaki wa mmewe.



Mmewe huku nyuma akawa amepata jibu,kuwa funguo alificha ni mkewe na si Linna.
"Unaficha funguo kwa vile kaja mwenzio aa tutaona nani mjanja,"Alijisemea kimya? Kimya? Baba Linna.


Mkewe alirudi na mswaki akampa mmewe nae akaupokea akaingia bafuni.
Mama Linna alipanda kitandani akavuta shuka akajifunika akalala.
Baba Linna akaoga vizuri,akarudi chumbani akakuta mkewe kalala.
Bila kuchelewa akavaa taulo akatoka nje na kumfungia mama Linna akaenda kwenye mlango wa Aunt au baby wake Joyce akaanza kugonga ili amfungulie aingie ale kitumbua.




Linna akiwa chumbani kwake alisikia sauti ya babake ikisema (baby fungua nimelifungia.)
"Mh! Inamaana ameiona funguo mpaka kamfungia mama," Linna aliwaza.

Taratibu aliamka akafungua mlango akachungulia akaona mlango ndio unafunguliwa na babake yupo nje,bila kupoteza muda Linna alitoka Babake akamuona.

"We unaenda wapi? Linna aliulizwa.
"Naenda kwa mama shikamoo Baba,"Linna alimjibu Babake na kumsalimia.

"We mtoto sijui mchawi ebu kalale huko."
"Mi njaa inauma namtaka mama."

"Toka hapa ebu nenda kalale huko njaa gani usiku huu we mtoto mbona unanivurugia mipango,"Alisema Baba Linna.

"Baba mi sitaki kulala njaa inauma sana,"Aliongea Linna akianza kutembea kuelekea chumbani kwa mamake na lengo kweli ni kuvuruga babake asile kitumbua cha Joyce.


"Dah! Ishu ishabuma yani huyu mtoto sijui mwanga yani balaa kwakweli,"Aliambiwa Joyce na Baba Linna ni baada ya kuona Linna anaenda kwa mamake.

"Basi baby tutafanya baadae."

"Powa tufanye baadae."
Maneno ya baadae eti watafanya Linna aliyasikia wakati anafungua mlango chumbani kwa mamake.

Alipofungua aliingia chumbani kwa mamake na babake nae akawa anaingia na taulo lake kisha akaingia bafuni.


Linna alimwamsha mamake ili amwambie babake kuwa alitaka kuingia chumbani kwa Aunt huku kavaa taulo.
Mamake alipoamka alisalimiwa na mwanae shkamoo!!.
"Marahaba mwanangu hujambo."
"Sijambo,mama nikwambie kitu."
"Ee mwanangu niambie."
Linna alianza kumwambia mamake kuwa mwenzio baba ameingia chumbani kwa...


Inaendelea


  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4