Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO:03


Review: 'Tyler Perry's Temptation' is very Perry, indeed - Los ...

"Mama mi nakula ila baba na Aunt wanashi....hata kabla hajatamka neno ka mamake
alimkatisha.
"Linna ebu kaa kimya kama umeshiba ondoka nenda kacheze,"Aliongea mamake asijue lengo la mwanae kuongea vile nikutaka kumuokoa yeye.

"Mama nataka nikwambie ukweli niskilize kidogo,"Alisema Linna.

"Halafu Linna saizi umekuwa mnoko hivi kwanini lakini,"Alizungumza mamake,Babake nae akadakia.

"Kweli mke wangu saizi Linna amebadilika sijui yupoje"
Linna baada ya kuona hapati ushirikiano alizira kula nakwenda kucheza.
Baada ya dakika tano akiwa anacheza Aunt yake au Joyce alienda pale sebuleni akakaa kwenye sofa nakumuita Linna.
Linna alivyoenda
akaambiwa ampe juice anywe.

Linna alienda kwenye  friji akachukua juice, akamimina kwenye glass nakumpa.
Alivyompa ajabu Joyce alimkamata akamfinya kwa nguvu?.
Linna alipiga kelele za maumivu?.
"Mamaa wee!"

Wakati Linna anapiga kelele Joyce alijimwagia  juis ili mama Linna aseme ni mwanae na Bahati nzuri akawa anafika.
"Wifi angalia mwanao alichofanya,"Aliongea Joyce akionekana kusikitishwa na kile kitendo.
"Wifi kafanyeje tena huyu mtoto,"Mama Linna  alimuuliza wifi kwa mjibu wa mmewe.

"Amenimwagia juice,mwanao ana dharau sana,"Alijibu Joyce maneno ya uongo mpaka mtoto Linna alishangaa wakati ye mwenyewe kajimwagia.

"Linna kwanini umemmwagia mgeni juice,"Linna aliulizwa na mamake.

"Mama sio mimi ni ye mwenyewe tena kanifinya bila kosa?"Alijibu Linna.

"Muone pua tena angekufinya kwa nguvu maana huna adabu."

Baada ya mamake kuongea hivyo Linna alianza kulia.
"Mama anamtetea wifi yake mi mwanae ananitukana,"Aliwaza Linna huku akiendelea kulia.
Mama Linna alichukia sana kusikia mwanae kammwagia mgeni juis, ilikuwa ni aibu kwake na mmewe mgeni angeona wamemshindwa kumlea mtoto wao.Alitoka nje akarudi na fimbo akaanza kumchapa mwanae,laiti angejua yaliyonyuma ya pazia wala asingemchapa.Alimchapa sana, babake nae alimchapa.Walivyoona wamelizika waliniacha.

Linna alilia sana,bora angekuwa amefanya kosa sawa.Sasa ye alionewa.
"Kwanini unanichapa bila kosa,"Linna alimuuliza mamake.

"Nimekuchapa kwa sababu huna adabu,umemmwagia mgeni juice na hiyo tabia ukome,"Alijibu mamake.

"Ila umenionea laiti ungejua ukweli hata usingenichapa,"Aliongea Linna.

"Toka hapa ukweli gani nijue kwanza nenda chumbani kalale tena fanya upesi."

Linna aliondoka sebuleni akaingia chumbani kwake.
Alivyoingia alitega sikio mlangoni ili asikilize wanaongea nini?.

"Yani wifi huyu mtoto msiwe mnamdekeza hata kidogo."

"Mi simdekezi ni babake yani anamlea kama yai."

"Mke wangu usiseme babake kwani we huwa humdekezi,"Baba Linna alidakia.

"Mme wangu we umezidi."

"Saizi naacha kumdekeza."

"Kweli bora muache tu ona mi mgeni kanimwagia juis,angekuwa mtu baki ingekuwaje sema tu mi ni Aunt yake."

"Wifi pole sana kwa nipashe maji ukaoge,"Mama Linna alimwambia wifi yake asijue ni mke mwenzie muda si mrefu anaenda kumpindua.

"Kweli wifi yani hapa nanukia juice tu."
Mama Linna aliondoka sebuleni akaenda kuwasha Hita ili maji ya kwenye tank yapashwe.Sebuleni alibaki baba Linna na mchepuko wake Joyce.

"Mwanao kaniudhi sana,"Alisema Joyce akimwambia Baba Linna.

"Pole sana yani huyu mtoto saizi hana adabu sijui mamake anamtuma hata sielewi."

"Inawezekana mkeo anamtuma anifanyie vituko."

"Kweli atakuwa anamtuma,maana hapo awali huyu mtoto alikuwa na tabia nzuri."

"Mh! Hii tabia kaanza lini?"

"Kaanza ulivyokuja wewe."

"Mh! Haya baby lakini atanyooka tu kwangu."

"Kweli tena bora abadilike maana bila hivyo fimbo kila siku."

"Kwa hiyo baby usiku utakuja."

"Ndio nitakuja."

"Mh! Sawa usinidanganye."

"Wala usihofu baby yani leo nita..Ghafla akiwa anataka aongee Mama Linna alitokea,ikabidi baba Linna abadili mada.Akajifanya anauliza eti yale mashamba ya marehemu babu hivi yapo kweli.

"Ah! Yapo sema kuna baadhi waligawa kwa wananchi,"Joyce nae akajibu kinafiki ili mama Linna asigundue walichokuwa wanaongea hapo awali.

"Wifi twende nikakuonyeshe bafu na chumba cha kulala,"Aliongea Mama Linna.

"Aya wifi."
Joyce aliinuka wakaelekea chumbani.

Baba Linna akabaki peke yake,akaanza kuongea peke yake.

"Yani leo huyu mtoto nitamk..sana?."Maneno hayo mtoto Linna aliyasikia vizuri kabisa.
"Lazima niwakomeshe,"Aliwaza Linna akienda kitandani nakujilaza.


"Linna unalala umeoga,"
Mamake aliingia mle chumbani nakumuuliza mwanae baada ya kutoka kumuonyesha mgeni chumba.

"Mama nitaoga kesho,"Alijibu Linna.

"Hapana embu amka kaoge fanya upesi."

Linna alitii amri ya mamake,aliamka akavua nguo nakuvaa taulo kisha akaingia bafuni.
Alioga vizuri akarudi chumbani nakujipaka mafuta kisha akapanda kitandani nakujifunika shuka.

Akiwa amelala akakumbuka babake alisema atamtoroka mamake ili akalale na Aunt yake.
"Lazima nifanye kitu la sivyo mama ataibiwa na huyu mpuuzi?"Aliongea Linna akiamka nakushuka kitandani.Alifungua mlango nakwenda chumbani kwa mama na babake,alipofika aligonga mlango punde babake alifungua.

"We nini usiku,"Aliulizwa Linna?.

"Baba mi nataka biskuti yangu nilisahau,"Linna alimdanganya babake.

"Haya chukua ulipo weka."

Linna alienda kwenye kabati la nguo akaangalia angalia halafu akamuuliza babake eti kwanini hazipo,lengo lilikuwa ni kuchukua funguo ili afunge mlango kwa nje Babake asitoke.

"Unamuuliza nani ebu kachukue sebuleni acha si tulale,"Mama Linna alimwambia mwanae.

Babake nae akaongezea.
"Kachukue sebuleni zipo juu ya spika pale."

"Sawa mi naenda,"Aliongea Linna baada ya kuiona funguo kwenye kitasa imechomekwa upande wa ndani?.

"Aya mwanangu usiku mwema."

Linna akiwa anatoka alichomoa funguo bila babake kujua na bila kupoteza muda akaingiza funguo kwenye kitasa akazungusha funguo akawa amefunga mlango?.
Baada ya kufanikiwa haraka akaenda chumbani kwake nakujitupa kitandani.






Saa saba kamili usiku Baba Linna aliamka nakumuangalia Mkewe akakuta amelala fofofo,taratibu alishuka kitandani nakwenda mlangoni.Akashika kitasa akakizungusha ile anavuta mlango akakuta umefungwa.


Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4