SEPTEMBER 1 SEHEMU YA KUMI NA SITA.
:max_bytes(150000):strip_icc()/iStock-637126086-5978d78f0d327a0011b429d4.jpg)
"Sasa sikilizeni kwa umakini, mimi nimepata wazo hivi saa. Mfuruki na Benjamin nyinyi nendeni kambini mjue mtalitatua namna gani. Mimi ninaelekea makao yangu ya kikazi hivi sasa, mjigawe hakikisheni wengine wanafika kule kwenye makao ya kina Huze tubahatishe kama wapo au lah. Tusidharau kitu, kukiwa na jipya mimi nitajua ni namna gani tunaweza kulitimiza", Kaila alisema huku akitoka kwa haraka, wengine nao walimfuata kwa nyuma huku wakiwa hima kuokoa maisha ya wasiyo na hatia.
ENDELEA NAYO SASA..
**
Robo saa baadaye Kaila aliwasili kwenye makao yake ya kazi, alifika hadi ofisini akiwa na haraka kubwa. Moja kwa moja akikimbia alfika kwenye dawati la Norene akamkuta akiongea na simu ya mezani, ujio wake mahala hapo ulimfanya binti huyo aweke simu chini na kuvuta kiti jirani na meza kubwa ambayo anatazama moja kwa moja na mwandani mwake.
"Nor mbona hivyo kwema huko?",
Norene aliuliza
"Nasikitika sitokuwa na muda wa kukujibu, huyo babu yupo humo ndnai?"
"Yupo sasa hivi hana mtu ofisini, pita ukawone"
"Nitakusimulia nikirejea ila kwa ufupi tu",
Norbert alisema huku akiingia ofisini kwa CE.
Norbert aliuendea mlango wa ofisi ya mkuu wake wa kazi, aliufungua kwa pupa na kuingia ndani akiwa hata mkubwa wake hajui kuna ujio wake upo hapo. Alimkuta CE akipangua mafaili kwenye kabati lililopo humo ndani, ujio wake ulimfanya ainue kichwa kwa upesi na alipomwona aliweka mikono kiunoni. Haijawahi kutokea akarejea bila taarifa na kuingia humo akiwa hajui, hiyo ndiyo mara ya kwanza na hata bosi alimshngaa haswa.
"N001 ndiyo uingiaji gani huo humu ndani?', CE aliuliza huku akiacha kufanya alichokifanya na kusogea hadi jirani na meza yake. macho yote yakawa ni kwa Kaila, ambaye yupo mita takribani moja toka alipo.
"Mkuu niwie radhi ila imenibidi, nahitaji ufanyike uamuzi wa haraka hivi sasa ndiyo maana nikafika kwako. Bomb squad wote wapo huru hivi sasa, na aliyefanikiwa kukomboa ni mtegaji wa bomu lile. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba hata mkitii masharti italipuliwa, msipotiii ni vilevile. Hakuna makubaliano kati ya magaidi na serikali, nahitaji nimuwahi kiakili"
"Kivipi?"
"Mtu akikuwekea kisu cha kwenye pumbu, wewe muwahi shingoni mwake. Nina jambo nataka kulifanya hivi sasa, kama mkiwa upande wangu naamini sitoweza kuwaangusha nyinyi nyote mahala hapa. Niamini, pia umweleze mkuu Dodoma juu ya hili, sijawahi kuwaangusha na haitotokea kama Mungu yupo upande wetu"
"Norbert are you sure?"
"Nikiongeacho nina uhakika nacho Mkuu, wale wana emotion man kule. Hiyo ndiyo great weakness ambayo ipo kwao. Unajua ukiujua udhaifu wa adui ni ushindi tosha, sasa itakuwa kete nzuri kwetu"
"Ok rejea kazini sasa hivi, naongea na
AE"
"Mkuu"
Norbert alitoka ofisini kwa mkubwa hadi kwenye ofisi ya Norene, alipofika aliweka mikono mezani huku akihema kinamna ambayo si kawaida. Binti huyo alijikuta akiinuka na kumtazama asielewe mwenzake kimemkuta, alitamani kumuuliza ila kabla hajafanya hivyo Kaila alimkatiza.
"Watimize masharti, au wasitimize lazima treni ilipuliwe password ya kutegua ipo kwa Huze tu. Nahitaji kumsaka kwa gharama yeyote ile"
**
Ilitumia dakika takribani ishirini kuweza kufikia makubaliano baina ya wakubwa wa shirika la EASA. Hatimaye wakaruhusu Gera atolewe gerezani, kibali cha hilo jambo kilitumwa kwa haraka kwenye treni ile kwa njia ya faksi. Ikamfikia DG Moses akiwa yupo chumba cha dereva wa treni pamoja na wenzake. Ilihitajika kupatikane nakala kama hiyo ndiyo uamuzi ufikiwe, maamuzi ya mdomo hayakuweza pekee kutimiza hilo jambo lisitokee.
"AE wa EASA ameridhia kuachiwa huru kwa Gerald Ralond. Muda si mrefu atatuma helikopta ya EASA ikiwa na rubani tu kwenda kumchukua huko.
Kinachotakiwa hivi sasa ni Mheshimiwa kuweka saini hii karatasi tu", DG Moses alisema huku akiwaonesha wenzake.
"Siamini kabisa EASA wamelegeza msimamo wao, wale watu ni wabishi wakishikilia kitu", CG Mwambe alisema na muda huohuo simu ya Belinda iliita, ilimbidia pokee hapohapo na kuongea na upande wa pili. Alipomaliza alimgeukia Jenerali Marwa na kumwambia, "Bomb squard wote wamepatikana wakiwa kamili, hivi sasa wapo kazini. Tutarajie mazuri kutoka kwao.
"Oooh! Yes! Sasa haya masharti mengine yenye kuhitaji ruhusa ya Mheshimiwa itakuwa vipi?", Jenerali Marwa aliuliza.
"Kwa mujibu wa AE amesema tusichukue uamuzi mwingine wowote kuanzia hivi sasa. Inabidi aitwe Mheshimiwa na kuelezwa aongee nao na kuwaambia wamefikia kukubalia kumwachia Gera. Kamwite
Mheshimiwa, hili suala limalizike kimyakimya bila ya kujua yeyote yule", DG Moses alisema halafu akamwagiza mmoja wa vijana wa TISS waliyopo humo kwenda kumwita Rais Zuber.
Dakika takribani moja Rais Zuber alifika humo ndnai kuelezwa kila kitu, tabasamu lilianza kurudi usoni mwake ingawa aliingiwa na shaka kwa kutokubali kufikiwa makubaliano mawili yaliyosalia. Hakuelewa kwanini aliambia asitoe amri ya kufikia mambo hayo, alichoamua kukifanya ni kuongea na magaidi kupitia simu ya upepo iliyopo humo ndani.
"Tumefikia uamuzi wa kumwachia Gerald Ralond hivi sasa helikopta ipo njiani kwenda kumchukua gerezani", Rais Zuber alisema.
"Vizuri, masharti mengine mawili imekuwaje. Mkumbuke saa zinazidi kuyoyoma muda ukitimia huo hatuna msalie na nyinyi nyote", Aliambiwa.
"Tupeni muda tutatoa uamuzi, hivi sasa tulikuwa tukilishughulikia suala hilo tu"
"Muda wa bomu ndiyo muda ufaao kwa nyinyi kujadiliana juu ya jambo hilo, hivi sasa tunawaacha ila hatutongeza hata sekunde moja. Kariri hilo", Mawasiliano yalikatika papo. Rais Zuber aliwageukia wanausalama na kuuliza, "hilo suala la dhahabu na almasi itchukua muda gani?"
"Mheshimiwa tusubiri hili liishe kwanza, ndiyo tufuate jingine hilo. Walivyotwambia hivyo huwezi wana malengo gani. Hawa ni wapo kwa ajili ya usalama wa kila mmoja kwenye ukanda huu", Belinda alisema.
"Sasa hivi rejea tu walipo wakuu wengine, sisi tunaendelea kuchakarika", DG Moses alimshauri.
**
Norbert aliwasili hadi eneo ambalo ndiyo kina Huze walikuwepo, huko hakukuta wahusika zaidi ya kulakiwa na maiti nyingi za walinzi. Askari wa JWTZ waliyotumwa walishatimiza kazi zao ipasavyo na majira hayo wamezngira kila upande huku Besi na Luteni Mfuruki wakiwepo eneo ambalo ndipo kina Watason walikuwepo. Kaila aliwakuta humo, kila mmoja akiwa haamini kama wamewakosa.
"Niliwaambia mimi hawa watu si wajinga wabaki hapa. Sasa hivi ni muda wa kwenda kule ilipo treni na si vinginevyo. Tujue ni namna gani tutashughulikia hili", Norbert alisema.
"Aisee hata ile kompyuta yenye kuongoza bomu wameondoka nayo, tuwahini huko haraka sana", Besi alisema hukua akitoka nje, nyuma aliuatwa na kina Mfuruki.
Walifika eneo ambalo kuna helikopta mbili za kijeshi zikiwa zimeegeshwa, waliingia kwa pamoja ndani na vyombo hivyo vikapanda angani kwa kasi kuwahi huko ilipo Treni.
**
Amri ya kuachiwa kwa Gera napo ikafika kwenye gereza la nyumba ya giza, majira ambayo CP Nkongo yupo kwenye kikao na maafisa wengine wa chini yake. Ilikuwa ni jambo ambalo hakuhitaji litokee, kwa jinsi alivyokuwa ni mwenye kutaka kuona mtu yule akifa kuliko kwa uraiani. Kwakuwa ni amri iliyotoka ngazi za juu ikieleza kulikuwa na lengo maalum ya kufanya hivyo, hakuona ulazima wa kuendelea kumshikilia.
Alisimamia mwenyewe gaidi yule akiandaliwa hadi alipovalishwa nguo zake kisha akaletwa akiwa na pingu hadi kwenye chumba cha mkutano. Machoni alibaki ni mwenye hasira huku akimtazama mtu huyo, ambaye ndiyo kwanza anacheka akiwaona ni wajinga sana kumuweka humo ndani na kumpa kila kitu muhimu kwa binadamua kuisha.
"Kamishna hivi unajua ni raha iliyoje, umeniweka humu nakula chakula cha bure kazi nafanya kuiweka misuli yangu imara. Hatimaye naachiwa na kurejea tena uraiani, you are loser CP, haya napenda unisindikize mwenyewe nienda kwenye helikopta si nasikia ishafika huko juu", Gera alisema kwa dharau, CP Nkongo alishikwa na hasira akataka hata kumvamia, Teddy aliwahi kumzuia asifanye jambo kama hilo.
"Una bahati sana wewe, humu siku ya leo ungemaliza ningekuja kukuua kwa mkono wangu mwenyewe. Hufai hata kupumua kwa sekunde hizi nyang'au wewe, ushukuru nipo chini ya CG kikatiba na siwezi kupinga amri zake. Ukatubu dhambi zako na umwabudu Muumba wako kwa kuifanya kikatiba niwe chini ya mheshimiwa Rais la si hivyo ningeweza kukumaliza hapahapa halafu tuone nani atanigusa"
"Ndiyo hivyo huwezi CP, ila nikupe shukrani kwa kunilisha mtu mbaya kama mimi ambnaye unasema sikustahiki kuishi duniani. Huoni ni dhambi kubwa sana hio umeifanya, ukatubu na wewe kwa kumlisha anayetakiwa kufa"
"Vijana mwondoeni mahala hapa haraka
iwezekanvyo, mpelekeni huko juu anaposubiriwa na helikopta ya EASA", CP Nkongo alisema na aliondolewa hapo huku akicheka, asilimia kubwa ya maaskari walivimba mno kwa hasira. Ila hawakuwa na kauli mbele ya maamuzi ya ngazi za juu, utiifu wa amri ni wajibu wao.
Gera alipandishwa kwenye helikopta ambayo ni ya kisasa kuliko ile aliyochukuliwa nayo kuja huko Iringa. Mlango ulifungwa na ikaanza kupanda juu kwa taratibu, hatimaye ikafika angani na kwenda kwa kasi kubwa. Muda huo alipohakikisha ipo sawa inaenda, alifungua pazia la nyuma lenye kutenganisha rubani na mtu aliyekaa nyuma. Matarajio yake ni kumkuta mwongozaji, ila alikuta kiti pekee huku chombo kikienda tu, ilionesha wazi ni chenye kuongozwa kwa mtambo maalum. Pamoja na hayo alikaa akidhani huenda rubani ameruka na chombo kipo mfumo wa kujiongoza wenyewe, alivaa vipachika masikioni kisha akahakikisha haipo mindo wa 'auntopilot'.
Pamoja na hayo chombo hakikuwa chenye kuongoza, bali kilienda chenyewe tena kikiwa kwenye mwendo usiyo wa kawaida. Gera alianza kuingiwa na hofu baada ya kuona suala hilo, hakutarajia kama angeweza kuingia mtegoni.
"Gera unapaswa utambue upo kwenye helikopta iliyotegwa bomu la kielektroniki. Ukisimamisha unakufa, ukitoka nje ya mpaka wa Tanzania vilevile tunakulipua. Ukifungua kioo upepo ukipita hutopona, salama yako ni kutulia hapo ulipo hadi sisi matakwa yetu yatimizwe", Sauti ilitoka kwenye spika iliyopo ju ya dashibodi.
**
"Hureee! Hivi sasa Gera yupo angani anakuja nafikiri ni muda mwafaka wa kumtafuta kwenye rada tujue yupo wapi?", Huze alisema kwa furaha, hakuwa na habari ndugu yake yupo hatarini.
Utafutwaji wa helikopta iliyomchukua Gera hatimaye waliweza kuziona nyingine mbili zikienda sambamba na treni. Hapo ndipo walitambua ni mali ya kamandi ya anga ya JWTZ, pamoja na hayo walipuuzia na kuendelea kuisaka hadi wakaipata ikikata anga ikiwa inamaliza eneo la Morogoro ikielekea upande wa Dodoma.
"Gera anaenda wapi huyu, hebu muweke kwenye line tuongee naye", Watson alisema na jambo hilo lilitimizwa mara moja, wakamwelekeza upande wa kwenda.
"Kaka helikopta hii ni sawa na drone tu, pia ina bomu pia nikijaribu kuisimamisha jua sitopona pia sitakiwi hata kufungua kioo niruke nje", Sauti ya Gera ilisikika kwenye simu ya upepo.
"What?!", Kila mmoja alijikuta akitamka akiwa haamini tayari mtu wao muhimu kachezewa mchezo mchafu namna hiyo.
"This is Besi, anaanza kuitumia taaluma yake vibaya upande wetu. Nasema hivi unganisha na kwneye treni niwape onyo wakishindwa kutimiza lipua reni yote najua hawawezi kumfanya chohote", Alpha alisema.
Punde waliunganishwa na kuanza kutoa vitisho kwa wanausalama waliyopo mule, wakaelezwa kama hawatomwachia huru basi itakuwa ni kifo kwao. Jambo hilo lilipelekea wote hapo wajue jeuri iliyowavaa upya wanausalama hao tena alipokuja Rais Zuber ndiyo kabisa aliwajibu kijeuri.
"Zima bomu la kwenye treni hili, lizimwe bomu la kwenye helikopta. Ukishindwa tambua hamtompoata huyu", Kauli hiyo ilimfanya Huze akate mawasiliano kwa hasira.
"Sasa jamni tutafanya nini hivi sasa?",
Watson aliuliza baada ya kuona wote wameshikwa pabaya.
"Tukumbuke bila ya Gera kuweka fingerprint kwenye mtambo wa kutafuta yalipoangukia makontena ya almasi bahari ya Pasifiki. Hatutoweza kupata mali yetu, ni wa muhimu kuwa hai kuliko hochote. Yeye ndiyo aliamua kuficha namna hiyo kabla ya kukamatwa, tulipanga tukitoka huku ni moja kwa moja kule. Tutumieni akili tusije tukakosa mali yetu", Alpha alisema
ITAENDELEA
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment