Friday, 28 March

Ads Right Header

Buy template blogger

FOMULA YA KUFAULU MTIHANI YAPATIKANA

FOMULA YA KUFAULU MTIHANI YAPATIKANA
Mkuu wa shule ya sekondari Karatu iliopo Wilayani Karatu mkoani Arusha kushoto mwalimu Marko Anne na Afisa elimu sekondari karatu Kalista Maina na Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Karatu John Zakaria Tipee kulia wakiwa katika picha ya pamoja juzi shuleni hapo wakati afisa elimu alipoenda kuangalia maandalizi ya mitiani ya kidato Cha sita.
 (picha Woinde Shizza)

Na Woinde Shizza, michuzi Tv ARUSHA
PROPER preparation prevents poor performance hiyo ndiyo fomula ambayo wanafunzi wameusiwa kutumia ili kuepuka kupata matokeo ambayo hayaridhishi katika mtihani wa kitaifa wa kumaliza kidato cha sita mwaka huu.

Afisa elimu sekondari Wilaya ya KARATU Kalista Maina alisema hayo wakati wa akiwakabidhi wanafunzi, vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari kidato Cha sita katika sekondari KARATU ambapo alisema anaimani kabisa wanafunzi wa Karatu sekondari wamejiandaa vizuri.

Alisema Mtihani ni vita kati ya Muandaaji na anayeenda kufanya mtihani, lazima mwanafunzi ujiamini katika pambano kwamba unaenda kushinda, hukuakihimiza wanafunzi kusoma swali na kulielewa linahitaji nini kabla ya kuanza kujibu.

Aliwahimiza wanafunzi kuzingatia muda wa kujibu maswali na kumaliza kwa wakati, lakini kuangalia maswali mepesi na mswali yenye alama nyingi kwani mathalani unajibu swali la essay fuata utaratibu wa kujibu swali la essay kulingana na matwakwa ya swali.

Aidha Maina aliwapongeza walimu wa sekondari ya Karatu na kusema ni walimu wa pekee sana na wamejitoa mpaka hatua ya wanafunzi kumaliza kidato cha sita ,Wamemaliza mada za darasani na wanafunzi wamepata muda wa kurudia vizuri tayari kwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha sita.

Alisema anaimani kubwa na shule ya sekondari Karatu wanafunzi wengi wataenda vyuo vikuu ,huku Akifafanua kuwa kumekuwa na usumbufu mkubwa wa wazazi wanaotaka kuhamashia watoto shule ya sekondari Karatu kwani Shule hiyo imetokea kupendwa sana kipindi cha hivi karibuni kutokana na kuwa na walimu mabingwa wa kufundisha, wanaojikita katika ujuzi walionao vizuri katika kuandaa wanafunzi

Maina aliahidi kufuatilia changamoto zilizotolewa na mkuu wa shule ikiwa ni pamoja na huduma ya maji safi kutoka kisima cha bonde la kwa Tom,ambapo Alisema atawasiliana na idara husika ili liweze kupatia ufumbuzi wa changamoto ya maji. 

Kwa upande wa changamoto ya Walimu alisema bado wanaendelea kuomba walimu kutoka TAMISEMI ili kujaza nafasi zenye upungufu wa walimu ,huku alibainisha kuwa majengo yote chakavu katika shule ya sekondari Karatu yako katika Mpango wa kukarabatiwa.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya shule sekondari Karatu John Zakaria Tipee katika salamu zake kwa wanafunzi, alisema ilipotokeajanga la ugonjwa wa corona alipata hofu kwamba wanafunzi watamalizaje maada zao darasani ,Hasa ukizingati kwamba kuna wanafunzi wanatoka maeneo ya vijijini na hakuna mtandao au nyezo za kimawasiliano kama watu waliopo mjini,lakini alipozungumza na walimu walimuambia wao tayari wamemaliza mada za masomo jambo ambalo lilimpa faraja.

Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mkuu wa shule Marko Anne Alisema shule ilikuwa na watahiniwa 370 lakini kwa sababu mbalimbali watahiniwa wamebaki 366,Mtahiniwa mmoja ameenda kujisajili private na wengine watatu hawatafanya mtihani kwa sababu mbalimbali ikiwemo sababu za afya,Wanafunzi waliandaliwa vizuri, hata wakati wanaondoka kutokana na janga la ugonjwa wa corona walipewa material ya kutosha ambayo yaliwasaidia kujisomea.

Wanafunzi nao wameeleza matarajio yao Ginde Laizer mwanafunzi wa Taasusi ya CBA na Rashidi Muzola Ramadhani mwanafunzi wa Taasusi PCB walisema wamejianda vizuri, walikuwa wanasoma na walikuwa wanatumia wanafunzi wa kidato cha chini kuwalekeza ili yale waliyoyasoma yaendelee kukaa kichwani pia walitumia muda wao katika kusali ili kuomba mungu awajalie waweze kufanya vizuri katika masomo yao ya kidato cha sita.

Wamesema wanafunzi waliopita kiwango chao cha ufaulu kimewapa ari ya wao kufanya vizuri zaidi ili waweze kuvunja rekodi , ikitokea wakapata matokeo ya chini zaidi ya kaka zao inamaana rekodi haitakuwa imevunjwa ,Wao kama wanafunzi wamedhamira kuweka historia yao ili kuzidi kuipa heshima Karatu sekondari wamesema wamejiandaa vizuri hata kipindi cha changamoto za janga la corona walikuwa wanaweza kutumia website ya shule kupata maswali na maandiko mbalimbali lakini pia kutumia vipindi vya television ya taifa TBC.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4