Ads Right Header

Buy template blogger

MBAPPE BWANA ALIWAHI KUOKOA PENALTI NJE YA 18

MBAPPE BWANA ALIWAHI KUOKOA PENALTI NJE YA 18


KYLIAN Mbappe, mshambuliaji namba moja ndani ya PSG mwenye ushikaji wa karibu na Neymar Jr, alifanya tukio ambalo watu hawakuamini macho yao kama angekuwa sahihi.

Wakati huo PSG ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Saint Etienne kwenye Ligue 1, wenyeji walipata penalti dakika ya 30 ambayo ilimfanya Mbappe afanye maajabu kwa kuokoa penalti hiyo kwa ishara akiwa nje ya 18.

Mbappe alitumia kidole cha mkono wa kushoto kumuonyesha kipa wake, Alphonse Areolo upande wa kulia wa goli lake hivyo asifanye makosa kuinasa.

Kweli bwana, mpigaji Remy Cabella alipiga upande uleule kipa akaucheza ngoma ikawa imeokolewa kimtindo na Mbappe nje ya 18.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4