Mchunguzi wa Umoja wa mataifa aonya kuhusu matatizo ya chakula Korea kaskazini
Idadi kubwa ya Wakorea kaskazini wanataabika kutokana na ukosefu wa chakula kwa sababu ya kufungwa mipala na China kutokana na janga la virusi vya corona, na vikwazo vya Umoja wa mataifa, mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa anayehusika na kuiangalia nchi hiyo ameonya leo.
Familia zinaendelea kula milo miwili tu kwa siku, wakati wengine wanakula nafaka tu na baadhi hawana kabisa chakula, mratibu wa Umoja wa mataifa kuhusu Korea kaskazini Tomas Ojea Quintana amesema.
Pia kumekuwa na ripoti ya ongezeko la idadi ya watu ambao hawana makaazi, ikiwa ni pamoja na watoto, katika miji mikubwa, mtaalamu huyo wa masuala ya haki za binadamu raia wa Argentina amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Geneva.
Kwa mujibu wa Ojea , kufungwa kwa mpaka kati ya China na Korea kaskazini mwezi Januari kumeongeza mzozo wa chakula, kwa kuwa biashara mpakani imepungua kwa zaidi ya asilimia 90, na wafanyabiashara hawana kipato.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment