Saturday, 15 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Wabunge 9 kati ya 69 wa CHADEMA wahojiwa na TAKUKURU Dodoma




Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Taasisi ya kuzua na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Makao Makuu Dodoma limewahoji wabunge tisa (9) kati ya sitini na tisa(69) wa chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wanaotarajiwa kuhojiwa dhidi ya tuhuma zinazokikabili  chama hicho ya matumizi mabaya ya fedha za michango ya wabunge.

Wabunge hao tisa waliohojiwa ni zoezi la kuwahoji wabunge wa chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa tuhuma zinazowakabili za matumizi mabaya ya fedha za michango ya wabunge wa chama hicho.


Zoezi Hilo lilianza majira ya saa mbili asubuhi ambapo  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye ameingia TAKUKURU saa moja dakika 55 asubuhi na kutoka saa nne kamili asubuhi akifuatiwa na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali ambaye ameriporti TAKUKURU saa mbili na Dakika 20 na kutoka saa tano na Dakika tano.

Zoezi hilo lilifuatiwa na Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA, Peter Msigwa ambapo ameingia saa nne na Dakika kumi na tano na kutoka saa Saba na robo mchana.

 Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, nae ameripoti TAKUKURU akiwa ameongozana na Mbunge wa Kawe kupitia Chama hicho Mhe.Halima Mdee, ambao wameripoti Makao Mkuu TAKUKURU majira ya saa saa nne na dakika hamsini na saba na kutoka saa Saba na Dakika kumi.

Baada ya hapo alifuatia  Mbunge aliyekuwa wa CHADEMA ambaye ameomba ni kujiunga na  CCM kutoka Momba David Silinde yeye ameripoti saa tano na dakika arobaini na moja na kutoka na kutoka saa nane na Dakika thelathini na mbili.


Akafuatiwa na Mbunge wa Tarime mjini Mhe Ester Matiko, na kufuatia na Mbunge wa Karatu Willy Kombaro na wamwisho kuhojiwa alikuwa ni mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Lwakatare.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4