Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Kesi za virusi vya corona zatarajiwa kuripuka India


Maambukizi ya virusi vya corona nchini India yatapanda kwa zaidi ya nusu milioni ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai na haina uwezo wa mahospitali kushughulikia mripuko wa aina hiyo, naibu waziri mkuu wa nchi hiyo amesema leo.

Tahadhari hiyo inakuja wakati kuna ripoti za kutisha za watu kuweza kupata kitanda hospitalini katika mji mkuu wa India, ikiwa ni pamoja na baadhi ambao wanasema wapendwa wao wanafariki mlangoni mwa vituo vya matibabu ambavyo vimekataa kuwachukua.

Licha ya amri ya kuwataka watu wabakie majumbani mwao iliyowakumba watu wapatao bilioni 1.3 iliyowekwa mwezi Machi, ugonjwa huo unasambaa nchini India kwa kiwango kikubwa duniani wakati nchi hiyo ikifungua uchumi wake ulioathirika.

Idadi ya maambukizi imefikia 266,598, ikiwa ni nchi ya tano duniani kwa maambukizi na inatarajiwa kuipita Uingereza katika siku chache zijazo.

  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4