MAJEMBE MAPYA YA YANGA KUTUA MAPEMA KABLA YA SEPTEMBA SITA
Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said ndiye amekamilisha mpango wa nyota hao kuibukia ndani ya Yanga.
Mukoko Tonombe ambaye ni mshambuliaji na mwenzake Tuisila Kisinda wote walikuwa wanakipiga ndani ya Klabu ya AS Vita, ya Congo.
Agosti 20, ambayo itakuwa ni siku ya Alhamisi wachezaji hao wanatarajiwa kutua timu Bongo kuungana na nyota wengine ambao walianza mazezi Agosti 10.
Septemba sita, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza na Yanga itaanza kurusha kete yake ya kwanza mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.
Leave Comments
Post a Comment