SEPTEMBER 1 SEHEMU YA KUMI NA MBILI.
:max_bytes(150000):strip_icc()/iStock-637126086-5978d78f0d327a0011b429d4.jpg)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIOPITA..
Waliendelea kunywa na kufurahi, kwa kukamilisha sehemu ya mpango wao ambayo itahitaji utimizwaji tu waweze kufikia kilele cha mafanikio. Watu hawa walikuwa tayari kwa lolote, ilimradi tu wafikie malengo yao waliyoyaweka.
ENDELEA NAYO SASA..
AGOSTI 31
Kutimia saa sita usiku kuamka siku hiyo ya Agosti 31, Norbert alikesha kufanya kila mbinu ili Samo aweze kuongea ila haikufanikiwa. Alijaribu kila awezalo, mtu yule hakuwa tayari kufungua mdomo wake, hata kujaribu kumshika binti yake na kumtishia kubakwa napo haikuzaa matunda. Mtu huyu alijiweka kichwa ngumu haswa, tena ndiyo alizidi kumcheka usiku huo wa manane kwa jinsi anavyohangaika.
"Kaila you are loser, unajua maana ya kumalizika kwa Agosti 31 yaani muda kama huu kwa usiku unaofuata. Kunakuwa na nini?", Samo alisema huku akiendelea kucheka kwa dharau.
"Septemba Mosi ndiyo inafuata", Norbert alijibu kwa kidharau.
"Ok nashukuru kwa jibu lako, naomba nilale hapahapa unaponiweka kil a siku. Nashukuru sana kwa kunilisha siku zote hizo bila hata kuhangaisha mfuko wangu kutafuta chakula. Wewe ni mtu mwema sana sijawahi kumuona adui kama wewe, Mungu akubariki sana", Samo aliponena hayo alicheka kwa nguvu huku akimtazama Norbert.
"Asante kwa hongera yako, hata mimi nilishachoka kuendelea kulisha mzigo hapa, salamu zao Samo msaliti wa Tanzania", Norbert aliposema maneno hayo alichomoa bastola iliyopo kiunoni mwake na kumwelekezea.
"Woow! Ungefanya kama hivyo toka mwanzo wala usingefikia huku kunipa chakula bure. Wewe ni fala tena mjinga kupitiliza kwa kuweza kunilisha mimi ukitegemea nitaongea, nafikiri utatua mzigo huo wa kunilisha kama mtoto nikakujazia choo pia"
Norbert hakuweka msalie tena, aliifyatua bastola, alimpiga moja tu ya paji la uso ukawa ni mwisho wa Samo.
Aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona angehangaika sana, hakuwa na kawaida ya kutesa watu ambao hawana hatia hivyo asingeweza kumshika binti wa mbaya wake na kumfanyia vile. Video aliyowahi kumwonesha ilitengenezwa na Samo alilibaini hilo, ndiyo maana hakutetereka.
Huwa haangamizi asiyehusika labda kwa bahati mbaya, huu udhaifu ndiyo ulimfanya mateka wake akaendelea kuwa kiburi na hata asiende kwenye mstari ule autakao yeye. Ama kweli adui yako ukimjua udhaifu wake, basi unaweza kumtawala kwa kiasi kikubwa. Ndiyo ilivyokuwa kwake, aliwezwa haswa na jasusi huyo kibaraka cha wasaliti wa nchi.
Norbert aliamua kuuchukua mwili wa Samo na kwenda kuutupa mlangoni mwa nyumba yake usiku huohuo. Kisha akaondoka na kurejea nyumbani kwake ambapo alipatelekeza kutokana na kuishi kwa mpenzi kwa muda mrefu, aliishia Temeke kulekule ambapo yupo kwa muda mrefu kabla hajatanua na kuwa na familia.
Alipowasili alifikia kusafisha mwili wake, kisha akafungua jokofu na kutoa mvinyo usiyo na kilevi. Aliufungua na kuanza kupiga mafunda kadhaa huku akitafakari juuu ya hali halisi ilivyo, alishafikia hapo akili ilihitaji kutulia haswa. Kila kibaraka wa chini aliyeingia mikononi mwake, aliishia kumuua tu hakuna mwenye kujua chochote kingine. Mwenye kufahamu ni Samo na wa juu zaidi, ambao wamefikia hatua ya kumficha kabisa juu kinachoendelea.
Alipiga mafunda kadhaa na hatimaye akili yake ikatulia huku akiitazama chupa ya kinywaji. Fikira zake zote zilikuwa mbali na hapo, ingawa alionekana ni mwenye kuwazia hiyo chupa. Haikuwa hivyo kabisa, tatizo lenye kumtatiza ndiyo aliliweka mbele.
**
ASUBUHI
Majira ya saa moja asubuhi Mzee Mluva asubuhi hii moja kwa moja alifika kwenye ofisi za treni eneo la Pugu. Kutokana na miadi muhimu aliyokuwa nayo siku hiyo, alijikuta akiingia kwenye ofisi za kisasa zilizojengwa mahala hapo ambapo kutakuwa ni kituo cha usafiri huo mpaya wa kiteknolojia.
Alifika moja kwenye ofisi mojawapo ambapo alikutana na mtu mzima wa makamo, huyu alimkaribisha kwa bashasha mno na kummwonesha kwa kuketi kisha akaanza kupiga naye soga kwa muda mchache na hatimaye alieleza kile kilichomleta mahala hapo.
"Mluva kama nilivyokuahidi kuwa nitatunza tiketi yako kwa ajili ya safari hiyo, nimeenda sawa na ahadi yangu. Yaani hivi sasa ungekuwa ndiyo unakuja basi ungekosa nafasi, toka juzi tayari lilishajaa. Yaani watanzania kusikia mambo ya bure, unafikiri utawatoa basi wamewahi mapema. Ila kurudi Dar likigeuza waliyopo huko watalipia nauli kwa siku hiyo wafike safari yao. Tketi yako hii hapa, kesho safari ni saa mbili asubuhi ndiyo inaanza", Mtu huyo alimwambia huku akimpatia tikiti, Mzee Mluva aliipokea kwa mikono na kushukuru kuweza kufikiahapo.
"Msengi sijui nikushukuru namna gani, yaani Benjamin bado ana hasira sana kwa mambo aliyofanyiwa kagoma kabisa. Inabidi niende moja kwa moja kwa mdogo wangu nikamwombe msaada huenda atanisaidia kwenye hili. Sitaki nimpoteze Benson", Mluva alisema.
"Nachokushauri ni umsamehe mwanao tu, rafiki yake alinieleza alivyopitia tabu hadi akaja kufikia pale. Bila mfadhili kujitolea kumsomesha unafikiri angekwepo wapi hivi leo, kama si kuishi mtaani. Hasira hizo ndiyo zimemfanya awe vile, msamehe atarejea kwenye hali ya kawaida na litaisha"
"Yaani najuta kabisa kumsikiliza yule mwanamke, laiti kama asingekuwa yeye basi ningekuwa nipo mbali na mwanangu hivi sasa. Huyu ni nyoka kabisa"
"Kosa kubwa ulilolifanya ni hilo, mwanamke kumpenda mtoto ambaye hajamzaa ilihali wa kwake yupo. Hiyo ni nadra sana kutokea, ilipaswa uwe makini mno na hilo suala"
"Nishakosea tena siwezi kufanya liwe halijatokea, sasa hivi inabidi niwahi hospitali kwenda kuangalia hali ya mwanangu"
"Kila la heri rafiki yangu, tutaonana kesho panapo majawaliwa saa moja hakikisha uwepo hapa. Maana Mheshimiwa akishapanda kwenye behewa lake basi jua kinachofuata ni nyinyi kuingia, usichelewe habari za kukimbiza treni kama zamani hazipo. Ulinzi wa kesho ni imara mno hautoruhusu hilo"
"Nashukuru sana"
**
Hatimaye aliiwekea shaka kampuni ambayo anafanya kazI Besi, kampuni ya Kibolomngo ndiyo aliiwekea shaka ya kuianzia maana mmiliki wake alimwona akiwa ni mwenye kuhusika kuandaa watu waje kummaliza kule Ilala. Aliingia kazini na kuanza kufuatilia nyendo zote za Huze hadi majira ya mchana alipotoka ofisini ndipo alimuungia mkia. Mtu yule aliwasili kwenye mgahawa mmoja na kuketi chini akipata chakula, Kaila naye akafika mahala hapo akiwa na kofia kubwa iliyomfanya asijulikane. Alipitia mlango wa mbele wa kituo cha kuuza chakula, hadi alipofika wa nyuma ambapo alielekea moja kwa moja hadi chooni.
Huko napo hakudumu, alikaa sekunde kisha akatoka na kurejea nje hadi maegeshoni ambapo kuna gari aina ya toyota hilux toleo jipaya ambalo aliwasili nalo Huze. Alijifanya kama la kwake akabandika kifaa jirani na kitasa, hicho kilifanya taa za pembeni ziwake na kutoa mlio hafifu. Alifungua mlango wa nyuma kisha akakinasua na kuingia ndani, wingi wa magari mahala hapo ulimfanya hata ajaribu kufanya lolote lile huku akijiamini. Ni vigumu mno kuweza kumkariri mmiliki halisi wa chombo chochote, hiyoikwa nafasi kwa upande wake.
Aliingia na kuufunga mlango kisha akabonyeza kile akilichotumia kufungulia mlango, ikajifunga kwa mara nyingine ambapo alitulia tu na sehemu ya uwazi kidogo juu ya kioo ili kuondoa joto la humo ilimuwezesha kupumua huku akimngojea mtu wake.
Dakika takribani kumi na tano baadaye, Huze alirejea na kuingia garini akiwa hana habari kama upande wa kushoto kiti cha nyuma kuna mtu kajibana. Kioo cha kati chenye kuelekea upande wake hakikumuwezesha kugundua hilo. Aliwasha gari na kuliondoa mahala hapo kuelekea barabarani akiwa hana hili wala lile. Akiwa njiani ndipo akasikia kitu kikigusa kisogoni mwake, alipotazama kiti cha nyuma alimwona Norbert Kaila akiwa ameketi hana habari.
"Unashangaa kuniona hai siyo?". Norbert alimuuliza baada ya kuuona mduwao wake.
"Nashangaa kukuona umeshika silaha wakati siyo anga zako Norbert, hivi uliponaje?", Huze alisema na kuuliza swali ili kupoteza muda tu.
"Acha kutumia mbinu za kizamani ya kunizubaisha, ongoza moja kwa moja hadi Msasani beach na ingie ufukweni", Alipewa amri huku silaha ikikandamiza kichwa chake.
"Kama sitaki je?"
"Nasikitika kusema huo ndiyo utakuwa mwisho wa kuishi kwako"
"Ngoja tuone sasa, utaanzia wapi sipeleki Msasani na sitoogopa huo mdomo wa bastola. Najua huwezi kamwe kuniua utahitaji niwe hai ndiyo maana ukataka niende huko"
Norbert aliposikia kauli hiyo alijikuta akitoa tabasamu tu, ingawa haikuwa yenye kufurahisha mbele ya adui yake huyo. Muda huo Huze hakufuata maagizo yake kama alivyomwambia. Ndiyo kwanza alizidi kukanyaga mafuta kuelekea mahali ambapo hakuambiwa, Norbert aliona mtu huyo ni mwenye kuleta ubishi.
Ilimbidi achekeshe kichwa kwa haraka la kumfanya, lilipomjia kichwani ila kuchelewa alimpiga na kitako cha bastola Huze hakujali kama gari ni yenye kwenda. Kitendo hiko lilipelekea adui yake aangukie usukani na kupelekea ilie honi kwa ghafla. Kaila ilimbidi amuwahi kwa kumtoa kichwa huku akivuta breki ya mkononi ya gari lile na kupelekea lisimame ghafla hadi na yeye akavutwa mbele ila aliwahi kujishika kwenye kiti cha dereva.
Bila kuchelewa alimtoa kwenye kiti na kumuweka pembeni, halafu akamfunga mkanda. Usukani aliukamata yeye akawa anaenda upande ambao wilaya ya Temeke ipo, hakuwa na shaka yeyote kwani aliamini mtu yule ataamka ikitimu nusu saa hapo baadaye kwa kumgonga kisogoni namna ile. Aliendesha kiamani huku akimpeleka anapopajua yeye, ambapo pangeweza kumpa uhuru wa kutenda lolote alitakalo.
Alifanikiwa kufika hadi eneo la mzunguko wa kurasini akitokea barabara iendayo stesheni. Akiwa eneo hilo ilimbidi asite kwanza kuendelea mbele, kwani njia itokayo Kariakoo kulionekana magari yenye kufanana kila kitu na gari analoliendesha yeye yakiwa manne. Tendo la kukanyaga breki kisha akawasha taa za mbele na kuzima, akimwashiria anayetoka Gerezani apite. Magari mawili kati ya manne yalipita, kisha la tatu nalo likamwashia taa na kuzima, Kaila hapo hakuwa na jinsi zaidi ya kusonga mbele tu kwani ilimuhitaji kufanya hivyo kwa dereva huyo kumpa nafasi.
Ufafanano wa motokaa zile na ya kwake wala hakujali, kwani zile zilikuwa na namba binafasi tu huku ya kwake ikiwa ina jina kwenye kibao cha namba. Alikanyaga akselereta kuingia kwenye mzunguko akajikuta yupo katikati ya magari mawili mbele na nyuma. Alienda nayo sambamba hakuwa na hili wala lile, vioo vya giza vya gari analoliendesha vilimpa moyo ya kwamba hakuna aliyeweza kumwona.
Akiwa katikati ya motokaa nne, hatimaye alifika katikati ya daraja lenye reli nyingi chini. Mawili yaliyopo
mbele yalishavuka eneo lenye machuma marefu yanayozuia mgari kutoanguka chini wala kusogea kwenye upande wa vivuko vya watu. Hapo ndipo Kaila alipojikuta kiingia majaribuni, wale wa mbele kwa ghafla walipiga kona kali. Mmoja akafunga njia ya anayoitumia, mwingine akaziba sehemu ambayo hutumiwa na magari yanayokwenda kwneye mzunguko wa kurasini. Ikumbukwe hii barabara ni ya njia moja tu, ambapo magari mawili hupishana na hutenganishwa kwa mstari mweupe wa kati pekee.
Norbert akiwa hajakaa sawa, milio ya risasi kutoka nyuma ilianza kurindima na ikamlazimu kuinama kwa haraka kwenye kiti. Vioo vilipasuliwa hovyo na akaona bado hatari ipo upande wake. Milio ya risasi iliyokuwa inarindima ni bunduki ya SMG, waliapoanza kushambuliwa kwa kupiga vioo laiti kama wangehamisha na kumimina risasi chini kidogo asingesalimika. Banduki hii iliyotengenezwa nchini China huweza kusalia ndani ya mwili pekee na kujeruhi ikiwa italengwa umbali wa mita 1000 yaani kilomita moja. Ukaribu aliyopo ingefyatuliwa ingepita kwenye mabati ya gari na kutoboa ikaendelea na safari, hata ikamfikia yeye na kupita mwilini mwake ikatokea upande wa pili. Hiyo ni hatari nyingine ambapo angeweza kupoteza maisha, hakusubiri hilo litokee ilihali mbinu hazikuwa zimefika kikomo.
Akiwa ameinama vilevile alikanyaga akselereta, akakunja kona kuelekea upande wa pili wa barabara. Alivifuata vyuma vizito vya pembeni ya daraja, mithili ya mtu mwenye kuelekea kuvigonga lakini alipovifikia alipinda kona kali na kufanya gari lake liserereke kiubavu. Kabla halijaribia kugonga kingo imara za daraja kiubavu. Alifungua mlango wa dereva kwa haraka, tendo lililopelekea mlango ugonge kwenye vyuma hadi ukavunjika. Yeye alitumia upenyo huo kujirusha anakakamata chuma kimojawapo, bila ya kukawia alitumia uwazi uliyopo eneo lenye kingo. Daraja hili lina kivuko cha magari na cha waenda kwa miguu, katikati yake kuna uwazi ambao ndiyo una vyuma vya kingo. Kaila alijiingiza hapohapo ingawa alijigonga tumboni ila hakujali. Aliangalia kujiokoa tu.
KITU AMBACHO NORBERT HAKUKIJUA
Huze pamoja na kutawaliwa na hasira kwenye baadhi ya maamuzi yake, pia ni mwenye kujua kufanya jambo la haraka kama akili yake itakaa sawa kuendana na muda husika. Kitendo cha Norbert kuja kumuwekea bastola akiwa yupo anauongoza usukani, alishajua njia ambayo ingeweza kumsaidia kumuokoa. Ndiyo ambayo aliitumia kwa haraka, hata Kaila mwenyewe hakujua kama mwenzake alishamzidi akili mahali ambapo alijiona yeye ndiye ametawala mchezo.
Usukani wa gari lake kulikuwa na kitufe eneo la chini kama unaelekea kwenye magoti yalipo, hiko alikiboneza kwa upesi. Ambacho kilitoa taarifa kwa walinzi wa makampuni yao kuwa yupo kwenye hatari, ujio wa gari zile mbili pale mzungukoni ulitokana na yeye kuwapa habari na waliifuata motokaa yake kupitia mtam,bo maalum wa GPS(Global positioning system). Hapo ndipo Norbert alipojikuta majaribuni hadi akajaribu kutoka kwa kupitia sehemu yenye uwazi wa darajani.
Walinzi wale walipofanikisha hilo, kwa haraka zaidi kwa kila upande walizirudisha bunduki zao kwenye gari. Wale waliyokuwa nyuma waliziweka kwenye motokaa mojawapo, wale waliyopo mbele nao walifanya hivyohivyo. Waliyobeba bunduki waliondoka upesi eneo hilo, wakiacha wenzao pekee wamesalia hapo. Gari mojawapo ilifuata uelekeo wa bandarini, nyingine ikachukua njia iendayo Kariakoo ikiikwepa ile ifikayo stesheni ambapo ni karibu na kituo cha polisi cha kati, tukio lile wangeweza kukutana na maafisa wa jeshi la polisi wakaingia hatiani na kuchukulia hatua za kisheria.
Si kwamba hawakuwa na namna ya kuweza kuwafanya wasikamatwe, bali wamebeba vitu ambavyo hatakiwi kuwa navyo mtu wa kawaida au asasi nyingine tofauti na majeshi. Kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania, silaha inayomilikiwa na jeshi haitakiwa kuwepo mikononi mwa kampuni yeyote ile au mtu yeyote wa kawaida. Kuanzia bastola, bunduki za kawaida na hata zile zenye uwezo mkubwa. Inayotumika jeshini marufuku, mtu au kikundi cha watu mwingine kuwa nayo. Ndiyo maana walikwepa barabara ile ili kutorosha silaha aina ya SMG zilizotumika kwenye mchezo huo.
Hata jeshi la polisi lilipowasili eneo hilo, waliwakuta na silaha nyingine ambazo kimlio hazikutofautiana na bunduki za kichina zitumikazo jeshini. Hawakuwa na shaka nao baada ya kupewa maelezo walipambana na jambazi mwenye uwezo mkubwa ambaye alimteka bosi wao.
Huze alikimbizwa hospitalini, huku msako dhidi ya adui yao ukiendelea. Pamoja na hayo mzee wa kazi alishatoweka eneo hilo upesi, walimtafuta kila upande ila hawakuweza kumwona. Walibaki wakiwa kwenye mshangao kwa jinsi alivyotoroka, ilihali walimbana kila kona. Moyoni kila mmoja alikiri mtu yule ni mwenye uwezo mkubwa kuliko kawaida, hadi kaweza kutoka pale. Wapo waliyoweza kudhani ni mshirikina, maana kuokoka waliona ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
**
Garimoshi mali ya TRL ambayo ina matenki mengi ya mafuta, ndiyo pona ya Kaila baada ya kusikia ikipita kwa chini muda ambao yupo chini ya daraja kajishika kwenye vyuma. Maadui wakiendelea kushambulia yeye, alijiachia na kutua kwenye moja ya tenaki kisha akaingia uvunguni kwa haraka na kujishikilia kwenye vyuma vya chini. Ni mchezo hatari mno aliyoufanya ila kwa kuwa ni mwenye kuhitaji kuokoka hakuwa na jinsi, chombo hadi kilipofika eneo ambalo magari hupita ndiyo alitoka chini kwa haraka. Alijibana kwenye behewa hadi alipofika eneo la jirani na makutano ya reli yaliyopo barabara iendayo Machinga complex.
Hapo ndipo alipojirusha nje na kubimbirika, eneo hilo lenye miti mingi kwake ndiyo aliona njia stahiki ya kuweza kumfanmya atoke kwenye treni hilo. Ingawa aliuamia ila aliweza kumudu na kusimama, huku nguo zake zikiwa zimechafuka mno. Kuokoka kwake huko kulimfanya aweke ishara ya msalaba, halafu akajikung'uta nguo na kuanza kutembea taratibu kuelekea Ilala.
"Mungu yupo uoande wangu leo kwa siku nyingine", Alijisemea huku akikumbuka namna ambavyo alimiminiwa risasi akiwa kwenye gari lile.
Norbert alifika hadi kwenye soko la mitumba la Karume, hapo alinunua kofia nyingine kisha akaondoka kurejea katikati ya jiji mahali ambapo aliliegesha gari lake kabla hajaamua kumvamia Huze. Mpango wake wa kumteka nyara tajiri yule, ulishindikana hapo kwa jinsi alivyovamiwa na walinzi.
ITAENDELEA
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment